Msaada wa kisheria kuwapata watoto baada ya kuhitilafiana na baba yao

Kingine mleta mada umezungumza kitu kama kuna wakati mumeo alikuwa anakataa watoto siyo wake na kwamba wapeleke kwa baba yao,unaposema mlikuwa na migogoro ya hapa na pale yumkini alikuwa anakuhisi kupungukiwa uaminifu?
Kuna maelezo tunamdai mtoa mada hapa. Ndio maana uko juu nimekwambia usitoe hukumu kwa kusikiliza maelezo ya mwanamke pekee. Silaha ya mwanamke kuinewa huruma na kukwepa kuwajibika ni ku-play victim, na kutokana na victim status waliyonayo huwa wanaaminika kirahisi. Ukishakijua ilo mwanaume unachotakiwa kufanya ni kimoja tu: usimuonee huruma mwanamke
 
Marriage was invented to protect women's interests. Huu ndio ukweli ambao kila mwanaune anatakiwa kuwekwa wazi kabla ya kusaini ule mkataba.
naam, kila kitu kiwekwe wazi na kukubaliana kabla - maisha hayatokua magumu
 
Kwasheria za bongo mtoto ni wa mwanaume wewe fanyayako wao watakuja kujitaftia mamayao
 
Na je utajitegemea kwA kila kitu kuwa tunza watoto hao ,pasipo kuomba hela ya matunzo kutoka kwA baba Yao!? Kama Iko hivyo basi wachukue
 
Jamaa ameona mbali na anajua uhalisia wa akina nyie mnaofanya kazi. Mkishaanza kupata visenti mnabadilika, mnaota mapembe na kumdharau mwanaume. Binafsi jamaa hajakurupuka.
Kama unamnyima fursa mwanamke ya kwenda kujitafutia kipato hakikisha unampatia mahitaji yote anayohitaji hasa ya muhimu.

Kama unatumia kigezo cha yeye kukosa kazi na kipato ili kumnyanyasa huo ni unyama na ushamba wa kizamani.

Bad enough ni wanaume wachache ambao wataweka nje tofauti zake na mwenza wake linapokuja suala la matumizi.
Sio mwanamke mmekwaruzana halafu humpi pesa ya chakula, huo ni ujinga na ushenzi, ni ugaidi na unyama wa kiwango cha juu sana.

Kama huna uwezo wa kuziendesha hisia zako muache mtoto wa watu akatafute kazi na sio kumfanya kama mtumwa wako, hayo ni masuala ya kitumwa.

Hizi tabia na mafundisho tunayopeana mitandaoni si kwa kila mtu, kuna watu ni vichwa maji na bado hawajawa wanaume, hivyo acha mkeo akafanye kazi, pesa ikimpumbaza akakudharau, achana nae, yanini kulazimisha mapenzi?
 
Katika ilo suala la kazi bila shaka dada alikubali kuwa mama wa nyumbani labda kwa sababu ya shinikizo la kutaka ndoa kutokana na rika, presha ya jamii au uchumi duni wa nyumbani.

Msimamo wa kutaka kazi na kwamba na yeye ana malengo yake amekuja kuibuka nao ndoani
 
Kivyovyote vile kwenye mgogoro lazima iangaliwe namna ya kum-favor mwanamke. Suluhisho ni mwanaume tu kutosaini ule mkataba wa ndoa
ni kufata nyayo za john cena tu 🤣 , sikupingi mkuu
 
Naona mpaka muda huu Team Kataa ndoa wako mbele kwa goli 9-1!
 


Narudia tena kusema, kama unahitaji mkeo asifanye kazi hakikisha una uwezo mkubwa wa kuziendesha hisia zako maana kukwaruzana na kutofautiana hakuepukiki, waswahili wanasema hata vikombe kabatini hugongana, sasa ukileta masuala ya ugomvi kwenye kutoa matumizi familia ipate mahitaji muhimu wewe ndiye unakuwa umeshindwa kutimiza wajibu kama baba.

Sasa hutaki mkeo afanye kazi, mkitofautiana kidogo unawanyima matumizi hapati chakula, mtoto wa watu anaanza kukopa huku na kule eti unamnyoosha apate adabu, huo ni ujinga na ukatili.

Na hapa nazungumzia sio tu kutokutoa matumizi bali hata kupunguza matumizi haipaswi, kama jumapili huwa mnakula biryani ya kuku na juice inapaswa iwe hivyo, sio ugomvi wenu inapelekea kumkomoa mwanamke na watoto.
 
Reactions: Lax
Mpeleke ustawi wa jamii ataitwa na utarudishiwa watoto.
 
Tumesikia Kwa Upande Wako.....Kwa Upande Wangu Siwezi Sema Lolote... Hadi Nitakapojaaliwa Kusikia Upande Wa Pili Wa Mumeo
 
Soma comment yangu vizuri. Hajuna popote nilipounga mkono mwanaume kukataa kuwajibika kutoa huduma na ulinzi kama mume. Msingi wa hoja yangu ni kwamba, kuna maelezo dada yetu hajatuweka wazi
 
Kama alikubali masharti hayo kipindi cha uchumba then baadae uanze kua na demand nje ya yale ya mwanzo, kosa ni lako. Kama mwanaume hana uwezo wa kuhudumia ukoo wa mwanamke akaibe? Hakuna sheria inayomlazimu mwanaume kuhudumia wazazi wa mke exept asipohudumia familia yake aliyoianzisha yeye hapo ndo hata sheria itakubana
 
Achana nae kwanza ishi maisha yako, ukileta ufala utakufa maskini kujitakia, watoto hao wakubwa acha akae nao utapata wengine, focus na kazi kazi ndio maisha
 
Kumshauri mwanamke kiburi, zuzu na mbumbumbu ni kazi sana, kama IQ yako ndogo ushauri wa kwamba tulia piga kazi Anza maisha mapya, borozi zipo zimejaa utatulia, zingatia usibebe mimba , weka kijiti au choma sindano
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…