Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?


Nitachangia cho chote ninachokijua ili ufikie malengo yako. Nimekutumia mail yangu kama una maswali binafsi, lakini yale ya kawaida tutapeana hapa hapa jamvini. Karibu tuanze kujadiliana.

Kwa Sumbawanga, nashauri anza na nafaka ( Mahindi,mtama,ngano,ulezi), au mazao yatoao mafuta,kisha anza kufanya utundu wa kujua namna ya kusindika nafaka hizo au mazao hayo. Nakuibia wazo, nenda pale Ihemi Iringa, kuna Wazungu wanasindika sembe, na wanaiita SEMBE TOFAUTI,na kweli ni sembe tofauti. Nenda kaibe ujuzi pale, hasa ujue mashine zao wamezitoa wapi mpaka ziwe tofauti na zingine. Usilime ili uwauzie mazao wenzako, sindika mwenyewe mkuu.

Njoo kwenye miti, najua utakimbilia mitiki kwa huko Bungu, je umejaribu Msederela, au acrocarpus. Navuta subira ili nijue miti fulani iliyooteshwa pale Msata msimu huu kama itafanya vizuri.

Nimekujibu jumla sana, lakini inabidi utoe sifa za ardhi yako ili wengine pia watoe mawazo yao sawa na wanacho kijua.
 
Ukisoma ushaur wa kila mtu unaweza kupata wazo pia maana naona kila mkoa umeguswa

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 




Dah kweli wewe ni mtu ndugu yangu, maana sisi wengine tuliokwepo nje tuna taka kurudi makwetu laki hatujui cha kufanya, unaambiwa tu kunabiashara nyingi za kufanya lakini watu hawa weki uwazi hizo biashara. Mimi nilipendelea sana mifugo, kama ngombe na kuku, lakini naona kuku watakua wa kienyeji, nitawafuga kwa njia ya kisasa, Watakua nje mchana kama kawaida, ni huduma ya chakula tu ndio nitaboresha, chapili ndio hiyo ya ngombe. Sasa ni kwamba kila mtu anasema lake, kuna mtu kaniambia ngombe anaweza toa lita 20 kwa siku, je kweli wapo hao, na hao ngombe wanapatikana kiurahisi au mpaka usubiri miezi au mwaka?
 

wapo mpk wanaotoa lita 24 kwa sku ninao
 
fungua hardware, ila mwanzoni inataka moyo mambo yakishachanganya inakua poa sana
 
Anzisha mradi wa kufuga kuku wa kienyeji wilaya za nje ya mji wa dar es salaam utapiga hela mpaka umnung'unikie mumgu kwa nini hukujiunga JAMII FORUM mapema???
 
Kama uko Dar nenda Mkuranga kijiji cha Shungubweni au Funza au Mwalusembe utakuta ardhi haina mwenyewe. Inafikika mwaka mzima,tatizo wenyeji wavivu sana. /

Huko Funza nk sh ngapi ardhi?
 
Mkuu Mbu,

Sisi hatuchomi ndizi kwa biashara ya kumsubiri mteja tusiemfahamu, hatuhitaji matangazo wala utambulisho. Sisi ni wateja na wao pia ni wateja, hivyo kwa pamoja tunachoma ndizi.

Wow!! Hili ni bonge la biz!! Niuzie nikuuzie.
 
nunua viwanja baada ya muda unaviuza
 
Nimesoma hii thread nimeishia page ya 10, nawahi sehemu nitaendelea nikirudi.
Mbu upo UK au Bongo? tuwasiliane nina good ideal, regardless hii thread ni muda mrefu lakini inaweza kuwa bado ni relevant.
 
Reactions: Mbu
Huko Funza nk sh ngapi ardhi?

Mkuu sasa hivi ni maumivu sana, bei imepanda sana kutoka 250 mpaka 500 kwa eka, sababu kuna waarabu wamenunua mapande makubwa sana, mchina kaingia anachimba madini, kuna beach ya boza nayo imevamiwa, eka moja 16M tzs,na yule jamaa mwenye zoo kalamba mapande, wenyeji wameshituka vibaya. Ila ukitumia wenyeji bado unaweza pata kwa laki nne kila kitu kwa eka moja.
 

Inabidi utupe contacts sasa maana hapa karibu weekend unaenda fasta.
 
Malila shukrani sana,najipanga nitakutafuta...Wana JF mbarikiwe sana kwa ideas ambazo si rahisi kuzipata sehemu nyingine
 
wadau ikiwa nataka kuimport bidhaa kutoka nje na kuziuza ndani ya nchi hapa,je ni bidhaa ipi itanilipa? mtaji kuanzia milioni 50 kwenda hadi milioni 200.
au kama una successfully business plan yoyote nisaidie ndugu yangu, sitakuacha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…