Samahani bwana Malila nahisi nimechelewa sana hii thread ni toka 2009 lakini nahisi ntafaidika na usaidizi wako,nimeacquire hekari 100 sumbwanga Rukwa na hekari 20 hapo Bungu mkoani Pwani na nina vision ya kilimo kikubwa.....nimefikiria miti natarajia usaidizi wako mkuu wa kiushauri na connections.Email yangu ni willynyakua@gmail.com
Nitachangia cho chote ninachokijua ili ufikie malengo yako. Nimekutumia mail yangu kama una maswali binafsi, lakini yale ya kawaida tutapeana hapa hapa jamvini. Karibu tuanze kujadiliana.
Kwa Sumbawanga, nashauri anza na nafaka ( Mahindi,mtama,ngano,ulezi), au mazao yatoao mafuta,kisha anza kufanya utundu wa kujua namna ya kusindika nafaka hizo au mazao hayo. Nakuibia wazo, nenda pale Ihemi Iringa, kuna Wazungu wanasindika sembe, na wanaiita SEMBE TOFAUTI,na kweli ni sembe tofauti. Nenda kaibe ujuzi pale, hasa ujue mashine zao wamezitoa wapi mpaka ziwe tofauti na zingine. Usilime ili uwauzie mazao wenzako, sindika mwenyewe mkuu.
Njoo kwenye miti, najua utakimbilia mitiki kwa huko Bungu, je umejaribu Msederela, au acrocarpus. Navuta subira ili nijue miti fulani iliyooteshwa pale Msata msimu huu kama itafanya vizuri.
Nimekujibu jumla sana, lakini inabidi utoe sifa za ardhi yako ili wengine pia watoe mawazo yao sawa na wanacho kijua.