Yaani hata manyeusi wenzao hawawatibu? Kuwa serious mkuu.Nina jamaa yangu pale Minneapolis Minnesota ni daktari na juzi juzi alikuwa ananiambia anataka aende The Empire state kuchukua zile dollsr 10,000 kwa wiki zilizotangazwa na meya wa Empire state
Utakuwa hujapata habari ya kile kinachojili kule mpaka wamelalamika. Hiyo unayosema ya dollar 10,000 basi itakuwa mikakati ya kuongeza huduma. Hata Trump mwenyewe amelalamikia hiyo hali!
 
Ni Bora kusubiri maelekezo ya serikali kuliko kutoa ushauri wakati shule zinafunguliwa 20/4/2020
 
Huyo CORONA wenu kama atahimili kishindo cha jua la kuanzia mwezi Mei na kuendelea (yaani kiangazi) basi atakuwa mwanaume!
 

Halafu?

Kama alichopendekeza mwenzako haliwezekani kwa sababu ulizotoa, badala yake wewe unapendekeza option gani?

å Shule na vyuo vifunguliwe, masomo na misongamano iendelee hivyo hivyo?

å Au Shule ziendelee kufungwa hadi hali ya maambukizi itakapokuwa imedhibitiwa kabisa na tukubali tu kupoteza muda huu na kisha uwe compensated huko mbeleni?

å Au shule na vyuo vifunguliwe kwa mafungu na wanafunzi/vyuo wawe wanaingia madarasani kwa mafungu kwa mkao distance inayokubalika ikiwa ni pamoja na sehemu zao za kulala?

Nini pendekezo lako hasa?
 

Nakubaliana na wewe kwa dunia ya sasa na kadri tunavyokwenda matumizi ya tehama kwenye elimu hayaepukiki. Kinachohitajika ni uwekezaji wa kwa walimu kama ulivyosema. But all in all kwa mtu ambaye hajaexperince mfumo huu (Virtual Learning/Classes) ni rahisi kuona kama ni jambo lisilowezekana.
 
Kama serikali ilidhani kufunga vyuo mwezi mmoja itazuia huu ugojnjwa basi ilikosea. Kwa sasa mambo ya online bado hatujafikia hizo teknolojia.

Kinachotakiwa ni kuanza mafunzo kwa njia ya posta. Wanafunzi wa vyuo wajiandikishe watumiwe printed lecture notes na syllabus. Pia online sources ziwekwe kwenye mfumo wa tehama ili wale wenye access wakapitie.

Waanzishiwe magroup ya whatsapp waendelee kuuliza walimu wao maswali ikiwezekana.

Mambo yakitulia basi wapewe mwezi mmoja wakakamilishe mambo ya test, assignment na mitihani.

Sekondari na shule za msingi zinaweza kuahirisha hata mpaka mwisho wa mwaka. Mwakani wanavushwa kwenda darasa linalofuata. Ila watafundishwa mara mbili mpaka jioni ili ku-cover contents za nusu mwaka uliopotea.

Darasa la saba na form four watafanya mitihani yenye maswali mpaka pale walipoishia darasani kuendana na ratiba ya wizara ya elimu. Sasa hivi wanapaswa watangaziwe mapema kuwa wajiandae na mitihani ya kuhitimu wakiwa nyumbani.

Nawasilisha.
 

Vizuri. Hapo umeeleweka vyema....

Nakubaliana na pendekezo lako....

Kwa wanafunzi wa vyuo vya kati na vya juu, utaratibu wa TEHEMA unawezekana japo unaweza usiwe successful kwa 100% kwa wanachuo wote....

Kwa vyovyote wengi hususani wa vijijini wanaweza kuikosa fursa hii kwa ukamilifu wake...

Kwa shule za msingi na sekondari, there's no way kufungua shule kwa sasa iwapo serikali inajiridhisha kuwa maambukizi bado....

The schools (pre-primary, primary & secondary levels) can be delayed for more time again until when the situation is under control....

Thank you
 
wakati nipo chuo mwaka wa kwanza mwaka 2000 tulikuwa tunafundishwa somo la kompyuta application, tena tulikuwa tunachekana sana watu wanavyopata shida kutumia mouse. Chuo kilikuwa kina library ya kompyuta ambayo iilikuwa connected na internet hivyo wanachuo wakawa wanaenda kutumia na ku surf mitandao na hivyo kuendelea kuwapa uwezo zaidi wa kutumia TEHAMA. Inanisikitisha sana kusikia kwamba miaka 20 mbele mwanachuo hawezi kutumia teknolojia ya TEHAMA na wala hajawezeshwa kumiliki laptop na smart phone/tablet kwa ajili ya shughuli zake za kujifunza. Hii nchi tunatia aibu, utaishia kusikia huyu kapewa milioni 200 ili akaunge mkono juhudi....what a mess!!
 
Ndiyo nchi yako mkuu. Just pray for it. God will intervene
 
Ea in the e in

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wataweza kweli hawa wanyoa viduku?

Muda wote wako instagram na facebook wanaangalia video za ambaruti na ponografia.

Ukiwaambia kuhusu online learning watageuka kuwa wakali kama mbogo aliyejeruhiwa!

Mnawaonea tu. Hawa wanyoa viduku wanachoweza ni kudanlodi video za ngono tu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndiyo nchi yako mkuu. Just pray for it. God will intervene
Kwa kweli inahitajika divine intervention, kama tunaweza kutumia matrillioni kununua ndege cash, hivi tunashindwa kutoa laptop kwa wanachuo as a special requirement kwa ajili ya kuwarahisishia shughuli zao za kujifunza.
 
Kwa kweli inahitajika divine intervention, kama tunaweza kutumia matrillioni kununua ndege cash, hivi tunashindwa kutoa laptop kwa wanachuo as a special requirement kwa ajili ya kuwarahisishia shughuli zao za kujifunza.
Ghadafi na jangwa lake aliweza kutoa mpaka mahari.
 
Shida ipo kutikana na uelewa was viongozi wetu na wananchi wa nchi hii,,tuwashinikize hawa viongozi watende sawasawa na hitajio la wananchi,,ni aibu kusikia kila siku kwamba huyu kaunga JUHUDI mara huyu kalipwa million mia tatu kama kishawishi cha kuhama chama kwenda kuunga juhudi. Tuwekeze kwenye vitu vya msingi kama nchi na vitu vya msingi kwa ajili ya kuwekeza ni ELIMU na UTAFITI
 
Utakuwa hujapata habari ya kile kinachojili kule mpaka wamelalamika. Hiyo unayosema ya dollar 10,000 basi itakuwa mikakati ya kuongeza huduma. Hata Trump mwenyewe amelalamikia hiyo hali!
Ila new York hakuna manyeusi wengi kihivyo
 

Siombi na naomba isiwe hivyo, lakini tatizo ni kubwa sana kuliko tunavyofikiria, kuomba ni sawa, ila jitihada za kibinadamu pia zinahitajika kupunguza madhara.
 
Kwa kweli inahitajika divine intervention, kama tunaweza kutumia matrillioni kununua ndege cash, hivi tunashindwa kutoa laptop kwa wanachuo as a special requirement kwa ajili ya kuwarahisishia shughuli zao za kujifunza.
Na wagonjwa wanazidi kuongezeka pamoja na vifo
 
Hali imeshakuwa tete, tuzidishe maombi
 
Mawazo ni mazuri lkn kwa nchi yetu ni ngumu kutekelezeka kwa kuwa wanafunzi wengine hawana vitendea kazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…