Nashauri shule na vyuo viendelee kufungwa lakini kwa upande wa vyuo vikuu, wakufunzi waanze kufundisha kwa njia ya mtandao.
Hii inawezekana hasa kwa masuala ya theory, na practical zinaweza kufanyika siku wakirejea vyuoni. Tutumie mitandao kuwafundisha kwa vile wapo majumbani.
Kwa kuanzia, kuna wawakilishi wa wanafunzi (CRs) na viongozi wa wanafunzi vyuoni, hawa wanaweza kutumiwa notes na wakufunzi kwa mtindo wa SLIDES na VIDEOS na kusambaza kwa wenzao na hivyo muhula wa masomo kuendelea kama kawaida.
Kwa wale wenye mikopo (BOOM) wanaweza kupewa nusu kwa mfano sh.250,000/= ili zingine wapewe wakirudi vyuo baada ya kusaini.
Nimeshuhudia vyuoni baadhi ya wanafunzi hawahudhurii darasani ila wanachukua slides na kujisomea na wamekuwa wakifaulu hata kuzidi wale wanaohudhuria.
Vyuo vitakapofunguliwa, wakufunzi wanaweza ku-HIGHLIGHT kile walichofundisha na baadae kutoa TEST ONE.
Ili kiepusha msongamano, usumbufu katika vituo vya mabasi, na kukosa usafiri, siku shule zikifunguliwa, wapishane kwa wiki moja. Kwa mfano, wanaweza kutangulia wa shule za msingi na sekondari na baada ya wiki moja wafuatie wa vyuo vya kati na vyuo vikuu.
Wanafunzi wa vyuo vikuu wana viherehere hasa wakati wa uchaguzi, hivyo si vyema uchaguzi ukawakuta wakiwa vyuoni.