Jenga mkuu, usisubirie uko baadae. Mana uko mbeleni utapunguziwa mshahara na uchumi utashuka na bado majukumu yatakuwa pale pale ya kulipa kodi ya nyumba na mengine. Lakini ukijenga ata km uchumi ukishuka bado utakuwa uko kwako ulipi kodi na una uwezo ata wa kuiuza pia.
 
Ha ha ha. Mwanangu hiyo ya sound labda 2022
 
Jenga usiogope maana iyo hela itaishia kwenye kodi pia.........kama utapata lidandasi utapata na akili zaid cha kufanya ili uendelee kupata hela.

mara nyingi watu huwa tunaridhika tukipata ila ukikosa utahangaika tu mpaka upate, na kizuri ni kwamba utakuwa huna stress ya kulipa kodi.

ebu piga hesabu na (NSSF / PPF) yako uone kama baadae utakuwa na hela ya mtaji hata kidogo???
 


Hakuna kitu nakwazika kama nyumba kuwa na madirisha madogo!...pia zile ramani za korido huku vyumba kama shule asichukue
 
Mkuu, jenga usiogope; fikiria hivi pia, hiyo kazi ikiisha leo then familia utaipeleka wapi? Ni afadhari familia iwe kwenye kivuli chao/nyumba na wewe ukiwa kwenye mishe mishe za kutafuta wao wapo somewhere salama kuliko manyanyaso ya nyumba ya kupanga (huna uhakika wa kupata kodi ) na pesa ya chakula huna. Ungekua tayari unayo biashara then could think kwamba, stop it for now or ongeza mtaji kwenye hiyo biashara yako.
 
Mkuu natofautiana na wachangiaji wengi, hii corona ni vita isiyokuwa na kelele na kabla vita haijaisha nani awezaye kujua kama atabaki salama au laa?Pamoja na kuwa una kiwanja hiyo 9m haiwezi kujenga na kumalizia nyumba unayoitamani unless unataka kujenga banda, kwani ukijenga nyumba unayoitaka utaishia mahali flani na utajikuta hela huna na kuishi kwenye hiyo ambayo haijakamilika pia huwezi ( faida yake ni nin?)

Ushauri wangu kwa kuwa wew ni mtunzaji mzuri na umeweza kutunza mpaka ikafika 9m endelea kutunza ili hali itakvyokuwa itakusaidia kujikimu na familia kwa kipindi ambacho hali itakuwa imekaa vbaya kutokana na janga hili la corona, usidanganyike na maneno ya kuwa corona itapita ndio itapita lakini itapita na nani? ukimwi unaua kwa miaka 30 corona inauwa kwa miaka mingapi? Nungana na mkuu hapo juu alieshauri kuhusu social distancing fikiria kuhusu familia yako kwa sasa na sio kitu kingine kwa sasa corona ni hatari kuliko kitu kingine chochote.ukitaka kupona """"""""kaa nyumbani kwako""""""
 
Afya kwanza mengine yapo tu
Weka fedha yako itulie bank....muda huu sio muda mzuri wa kuwekeza chochote iwe kwenye biashara au majengo,ni muda wa kutetea uhai wako wewe na familia yako.Kuna fedha inaweza kuhitajika kwa dharura ili uokoe afya yako au ya jamii yako.Uchumi wa dunia unayumba kwa sasa kutokana na hili janga...na kila mmoja anapambania afya yake aweze kuishi.
 
wazo lako lingekuwa zuri kama angekuwa hana familia. Ukisha kuwa na familia makazi ni kitu cha kwanza.

Kuhusu kujenga nyumba kwa pesa aliyonayo anaweza kujenga nyumba ndogo ya kawaida na akahamia sema finishing ndio atamaliziaga akiwa hapo.
Kuna uzi humu jamaa kajenga na kuhamia bila finishing kwa mil7.
 
Jilinde na corona tuuuu we na familia yako maendeleo HAPO Shukuru una cash ya kujikimu
 
Ni wazi kwamba Dar imechafuka kutokana na corona.

Pia kuna malalamiko ya wadau kuhusu uwepo wa Sera rasmi na mkakati wa kupambana na corona. Ni vigumu ukienda mkoa wowote wa Tanzania,mbali na Dar es salaam,kujua mahali gani utapata kipimo cha corona.

Tahadhari hii naitoa kwa sababu makampuni ya kimataifa ya usafirishaji pamoja na makampuni ya meli yanausoma mchezo na hayataki kupoteza watumishi wao wala biashara zao kukwama kutokana na ugijwa huu hivyo yanaweza kuchagua nchi inayopambana kwa umakini na corona, ni wazi wataenda Mombasa

Ni wazibpia Uganda na na Rwanda wataanza kuwekea ngumu kampuni zao na mizigo kupitia Tanzania ili kudhibiti maambukizi kutokana hapa nchini



Natoa tahadhari tu
 
Mleta mada,makampuni kote ulimwenguni mpaka sasa hayana uhakika na kesho yao,achana na hali ya Tanzania bali hali iliyopo dunia nzima.mashirika ya uchimbaji mafuta yameshaipata fresh ya unga,hayajaipatia hapa tz bali ulimwenguni kote.

Wakati unawaza madhara ya corona tz hasa dsm,yenyewe inagonga dunia nzima kwa ujumla,so achana na ndoto za mombasa sijui mmaputo nk.
 
Sawa
 

Asante boss, Kuna watu wengine Ni Kama Wametumwa na Shetani au wana asili ya uchawi.. yaan watu bado wanawaza Kama Korona itawaacha salama Mwingine anaamka na hypothesis zake Sijui ili iweje... We have enough problems already, hebu kaa na speculations zako kwanza utatukumbusha badae
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…