Wakuuu, ninawaambia kabisa kuwa huu ugonjwa ni hatari tuchukue hatua na tusaidiane na wataaalam wa Afya na serikali iwajibike pale ambapo haichukui hatua madhubuti tuiambie pasipo kumumunya maneno, corona haina chama wala cheo, haina masikini wala tajiri, tunapopiga kelele ni Kwa ajiri ya kukunusuru wewe Mimi na Yule, usifikiri hiii ni siasa no, Leo hiii unaweza kujikuta inaingia kwenye kituo cha polisi, halafu polisi wanaanza kutafutana kwa tochi, haitajari mabunduki wala mabomo itaingi itaumiza Ndugu zetu.
Corona inaweza ikaingia kule lugalo hospital ikatafuna had mabrigedia, corona haijali mizinga, mnaweza kujikuta wanajeshi huko vikosini wanatafutana kwa tochi, korona haina chama tushirikiane pasipo kubaguana kuingiza siasa wala vitisho, maaana unaweza kuwatuma polisi kuwa nenda mkawasghugulikie watu kwenye mitandao pasipo kujiuliza kuwa hivi polisi si ni watu Kama hao, corona si nao inaweza kuwaiingilia?
Tuache vitisho na siasa kwenye Jambo la kuokoa uhai wa watanzania tuuungane wataalam wa Afya watuongoze na tusifiche vifo, hiii corona ni mziki mzito mnaweza kuja kujikuta kila mtu analala mbele kujificha mkakosa hata wa kumtuma kukamata watu
Sasa unadhani ikiingia vituo vya polisi ikaingia kwenye makambi ya jeshi unadhani watakusikiliza? Nchi Kama nchi ichukue hatua haraka
Sent using
Jamii Forums mobile app