#COVID19 Mtazamo, Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Serikali na Wananchi kuhusu Ugonjwa wa Corona - COVID-19
Ni vema waziri Ummy Mwalimu akawa anatupa up dates za Corona kila siku au kila baada ya saa 24 ili kuyafanya mapambano kuwa hai.

Kadhalika kwa jiji la Dsm RC Makonda angeweka utaratibu madhubuti wa kufuatilia maagizo yote aliyoyatoa ys kudhibiti Covid 19.
Leo nimepanda daladala kutoka Posta hadi Makumbusho nusu ya abiria walikuwa hawajavaa barakoa akiwemo na kondakta.

Viongozi wetu fuatilieni haya mambo kwa karibu, Corona ni janga hatari.

Ramadan kareem!

Maendeleo hayana vyama!
Speech ya Chato ya juzi imeondoa confidence ya viongozi kutoa up dates kuhusu Corona.
 
Ni vema waziri Ummy Mwalimu akawa anatupa up dates za Corona kila siku au kila baada ya saa 24 ili kuyafanya mapambano kuwa hai.

Kadhalika kwa jiji la Dsm RC Makonda angeweka utaratibu madhubuti wa kufuatilia maagizo yote aliyoyatoa ys kudhibiti Covid 19.
Leo nimepanda daladala kutoka Posta hadi Makumbusho nusu ya abiria walikuwa hawajavaa barakoa akiwemo na kondakta.

Viongozi wetu fuatilieni haya mambo kwa karibu, Corona ni janga hatari.

Ramadan kareem!

Maendeleo hayana vyama!
Wengine kuvaa barakoa na wengine kuacha kuvaa haisaidii, kwasababu ukivaa barakoa peke yako na wengine hawavai haisaidii. Unakuwa unawaprotect wenzako lakini wenyewe hawajali kuhusu wewe. Ndo maana kwa wenzetu kabla ya kufungua sehemu za kazi wana mandate issue kama masks.
 
Muhimu tuhimizane lishe bora kuongeza kinga ,tiba asili kufukiza na kuwakinga wale dhaifu pekee.Maisha yaendelee tutavuka salama.Tusisahau maji tiririka tutaondosha maradhi mengi ya uchafu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu tumetofautiana sana bwashee...... ndio maana hata Marekani wanataka kufunguliwa wakati wanakufa kila siku!
Hata marekani siyo kiurahisi, ni kutapatapa tu kwa baadhi ya governors kwasababu ya uchumi. Ndo maana unakuta gavana anafungua, mayor anafunga mji wake anasema “nope, a little too quick”
 
Aliyevuruga ni Magufuli na ile hotuba yake. Sijui aliwaza nini
 
Wakuuu, ninawaambia kabisa kuwa huu ugonjwa ni hatari tuchukue hatua na tusaidiane na wataaalam wa Afya na serikali iwajibike pale ambapo haichukui hatua madhubuti tuiambie pasipo kumumunya maneno, corona haina chama wala cheo, haina masikini wala tajiri, tunapopiga kelele ni Kwa ajiri ya kukunusuru wewe Mimi na Yule, usifikiri hiii ni siasa no, Leo hiii unaweza kujikuta inaingia kwenye kituo cha polisi, halafu polisi wanaanza kutafutana kwa tochi, haitajari mabunduki wala mabomo itaingi itaumiza Ndugu zetu.

Corona inaweza ikaingia kule lugalo hospital ikatafuna had mabrigedia, corona haijali mizinga, mnaweza kujikuta wanajeshi huko vikosini wanatafutana kwa tochi, korona haina chama tushirikiane pasipo kubaguana kuingiza siasa wala vitisho, maaana unaweza kuwatuma polisi kuwa nenda mkawasghugulikie watu kwenye mitandao pasipo kujiuliza kuwa hivi polisi si ni watu Kama hao, corona si nao inaweza kuwaiingilia?

Tuache vitisho na siasa kwenye Jambo la kuokoa uhai wa watanzania tuuungane wataalam wa Afya watuongoze na tusifiche vifo, hiii corona ni mziki mzito mnaweza kuja kujikuta kila mtu analala mbele kujificha mkakosa hata wa kumtuma kukamata watu

Sasa unadhani ikiingia vituo vya polisi ikaingia kwenye makambi ya jeshi unadhani watakusikiliza? Nchi Kama nchi ichukue hatua haraka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizo hofu na uongo mnaolishana kuhusu corona Acheni mara moja

Corona inaelekea kuthibitiwa Tanzania

Chadema acheni kutumia corona kisiasa mtaaibika
 
Wenye busara wanajua korona siyo jambo la kisiasa, wasio na busara wanatumia fursa hii kutangaza siasa na kugawanya watu utafikiri wao hawawezi kuipata.
Wasamehe bure kuna wanasiasa wengine wanajifunza polepole ama kufanya vitu polepole 'slow learners and slow doers'
 
Wakuu,

Tuache mzaha msidhani yanayotokea duniani huko ni hadithi hapana tuanzie na hapa jukwaani tuwaelimishe ndugu zetu walio vijijini na mijini juu ya janga hili na tuwakumbushe kila wakati wachukue tahadhari muhimu ikiwapo kuepuka misongamano, kunawa mikono mara kwa mara tuhakikishe tunawasisitiza juu ya hayo ili kuepusha vifo, na wasitoke bila sababu

Ukiiokoa familia yako basi umeokoa taifa kwa ujumla, #Sema na familia yako juu ya Janga La CORONA#
Watanzania Tusiishi Kwa Mazoea.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom