Mtaani ni kama hakuna Corona watu wanacheza draft kama kawaida, Malaya wapo vijiwe vyao kama kawa, watu wameacha kuvaa mask
 
We are doing that, but with this kufunga, ndipo utaamini msemo kuwa religion abhors science! Naona nyumba zimejaa saa kabla ya futuru!
 
Huu ni wakati wa Chama Mbadala kutoa mwongozo nakuwaongoza wananchi katika mapambano dhidi ya Covid 19. Kama wananchi walichanga zaidi ya 310Million kutoa wapendwa wao magerezani,

Je, watashindwa kuchanga Billion kununua machine na PPE kuwezesha utoaji huduma na wagonjwa wanaozidiwa kupumua kuokoa wapendwa wao?

Katibu mkuu Yuko kimya, mwenyekiti yuko kimya.

Namwona Heche Twitter akikazana kulaumu mamlaka, ni jambo jema maana yeye ni mbunge kazi yake nikukosoa serikali.

Ila waunganisheni wananchi tupeni mwongozo wa kichama tutachanga mkanunue hizo machine na PPE kwa wahudumu wa afya hasa maeneo yaliyoainishwa na serikali kukabiliana na Covid 19.

Kama serikali imekimbia wajibu katika hili then ni nyinyi mnaopaswa kuchukua hatua kuongoza mapingano kimbinu zaidi bila kuleta mgongano na mamlaka husika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…