Ni nini hiki serikali inafanya? kila anaekufa anazikwa na serikali kwa gharama na usimamizi wake, hii ina maana serikali imetenga fedha kuhudumia maiti na haiko tayari kutenga fedha kuboresha sekta ya afya ikiwemo kununua PPE kwa ajili ya wahudumu wa afya na mashine za upumuaji kupambana na corona? MICHANGO inayotolewa kila siku na wadau inaenda wapi?
kwa sasa kila dk ukiingia mtandaoni utaona kuna taarifa ya kifo tena za watu maarufu, hii inaashiria kuna walalahoi wengi wanakufa na serikali haitoi taarifa, kuna faida gani kuficha hizi taarifa?
Wananchi wapowapo hawajui washike ni kama hamna ugonjwa wowote hapa nchini, hakuna tahadhari, kwenye daladala watu wanakaa level seat sawa, lakini kupanda wanasukumana ili kugombania kuwahi seat, hakuna wa kuwapa elimu Serikali ni kama haipo,NYIE mnasubiri wafe ili mgharamie kuwazika maana budget hiyo mnayo..AIBU YENU VIONGOZI.
Wewe mwanachi chukua tahadhari CORONA IPO NA INAUA, maana mpaka sasa sitaki kuamini serikali ipo kusubiri mwananchi afe ili imzike na si kumhudumia na kumpa taarifa sahihi ya hali ya ugnjwa na maeneo yaliyoathirika zaidi yatafutiwe suluhu ili yasiambukize maeneo mengine.