#COVID19 Mtazamo, Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Serikali na Wananchi kuhusu Ugonjwa wa Corona - COVID-19
Wanadamu mabingwa wa kusingizia wengine. Hatupendi kuwa accountable (kuwajibika). Corona (Covid-19) ni ugonjwa wa Kirusi (Virus) kama Ukimwi (HIV) au Avian Influenza (HPAI). Tulishaamua kuishi na magonjwa mengi tu ya aina ya Ukimwi au Homa ya Ini.

Leo Covid-19 imekuwa gumzo. kila mmoja mtaalam. Na juhudi zinapigwa kupata Dawa (Tiba) au kinga (Vaccine). Ukweli mchungu ni kuwa inawezekana tusipate chanjo kwa miaka mingi ijayo (Tiba usiwazie). Hofu imetujaa. Tutakufa na hofu. Tuendelee na maisha. Ukipata covid-19 tumia lolote au chochote na Mungu (Omba sana) atakusaidia upone. Ukipona hiyo imetoka. Kula vizuri (First line defensive mechanism): balanced diet ukiweza na usisahau Vitamins and Minerals.

Jenga kinga ya mwili ndiyo imekuwa ikitulinda na Malaria ama Homa za matumbo ilihali wenzetu wageni wakija wanashambuliwa vibaya. Usiogope, fanya mazoezi ya kutoogopa. This invisible enemy covid-19 is different from other Virus, be vigilant but courageous to face the enemy. Usikate tamaa. Atapita kama wengine na tutakuwa tunaishi naye kama Dengue au Homa ya bonde la Ufa.
 
Ni nini hiki serikali inafanya? kila anaekufa anazikwa na serikali kwa gharama na usimamizi wake, hii ina maana serikali imetenga fedha kuhudumia maiti na haiko tayari kutenga fedha kuboresha sekta ya afya ikiwemo kununua PPE kwa ajili ya wahudumu wa afya na mashine za upumuaji kupambana na corona? MICHANGO inayotolewa kila siku na wadau inaenda wapi?

kwa sasa kila dk ukiingia mtandaoni utaona kuna taarifa ya kifo tena za watu maarufu, hii inaashiria kuna walalahoi wengi wanakufa na serikali haitoi taarifa, kuna faida gani kuficha hizi taarifa?

Wananchi wapowapo hawajui washike ni kama hamna ugonjwa wowote hapa nchini, hakuna tahadhari, kwenye daladala watu wanakaa level seat sawa, lakini kupanda wanasukumana ili kugombania kuwahi seat, hakuna wa kuwapa elimu Serikali ni kama haipo,NYIE mnasubiri wafe ili mgharamie kuwazika maana budget hiyo mnayo..AIBU YENU VIONGOZI.

Wewe mwanachi chukua tahadhari CORONA IPO NA INAUA, maana mpaka sasa sitaki kuamini serikali ipo kusubiri mwananchi afe ili imzike na si kumhudumia na kumpa taarifa sahihi ya hali ya ugnjwa na maeneo yaliyoathirika zaidi yatafutiwe suluhu ili yasiambukize maeneo mengine.
 
Mko wapi, mnasemaje sasa?
Mliosema ngozi nyeusi tuna kinga madhubuti, mmebadili mahubiri?
Na wale walitushambulia kwa kusema tunaleta taharuki mnatwambia nini leo
Bado mko na msimamo wenu huo?
 
Kwa namna tunavochukulia mambo rahisi rahisi Tanzania, itageuka kisiwa cha vita ya kufa bila kukabwa wala kuuawa.

Tunakimbilia kusema tuna maisha magumu ni kweli kabisa maisha yetu ni magumu lakini tulipofika sasa, maisha magumu ya mwingine yasikuuwe na wewe.

Tuliona kabisa uongozi wetu haukuwa makini kuchukua hatua za haraka kwa kufunga mipaka na viwanja vya ndege na tunaona kabisa hawataki kuzuia wala kulazimisha cha zaidi tunaona wanataka tufe TRA wanatangaza kudai mapato yao

Tunakosa nidhamu ya kujipenda na kuwapenda wengine mtu anaona bora akazunguke hata kama ataambukiza wengine kuliko kukinga wengine, tunaona uhalisia namna watu wanavyokufa wengine wanaanguka tu mabarabarani, unadhani kuna kupona? Wengine wanakimbia isolation station wanamozunguka humo mitaani wanaachia wangapi magonjwa.

Tumeshindwa social distance

Tumeshindwa kujifungia

Misibani tunaenda vizuri tu tena tunasimama zero distance.

Kama hatuchukui hatua za haraka serikali sio baba yako kwamba italinda watoto wako watabaki yatima tena wa kutupwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1588072370336.png
 
Walimcheka wakamkebehi pale aliposema jamani tusitangaze idadi ya vifo wala maambukizi ya corona tutangaze wanaopona tu lakini takribani week moja mbele ushauri wake unafuatwa kimyakimya na heshima ya nchi yetu imeongezeka sana in a week.

Dunia nzima inapigwa na butwaakwa namna gani Tanzania kwa mwezi na nusu ina vifo kumi tu ingawa wanatudharau wamesahau kwamba awamu hii imeboresha mnooo tena mnooo sekta ya afya zimejengwa hospitals na zahanati 257,maboresho ya kazi lwa madoctor na ajira mpya za madoctor zimemwagwa, matter of fact HIJAWAHI KUTOKEA TANGU NCHI IPATE UHURU SHUKRANI SANA KWA JPM NI KISHINDO KIKUU.

Ukiachilia mbali umahiri pia wa jeshi letu pendwa la polisi kuwa na uwezo mkubwa wa kiintelejensia kuhusu mkusanyiko gan (press conference) utakuwa na maambukizi na upi hautakuwepo lakini pia ushauri wa Mwigulu vyote kwa pamoja vimesaidia kuleta heshima hiyo.

Mwigulu Nchemba arudishiwe uwaziri wake. PhD yake kaitendea haki na Kitila Mkumbo apigwe marufuku kumsumbuasumbua huko Iramba. Vilevile, it is high time jeshi letu tukufu la polisi lifanye sharing ya knowledge yake ya CORONA COUNTER INTELLIGENCE(CCI) ili kusaidia nchi zilizoko kwenye lockdown zinazovutana na raia wasiotaka lockdown ili wajifunze kutambua mikusanyiko itakayokuwa na uwezekanao wa maambukizo ya coronaama la.

Tumeshuhudia jinsi polisi kule dodoma walivyomuokoa Mbowe Freemana asipate maambukizi ya corona kwa kuzuia press conferenc yake,ule ni ushujaa na display ya hali ya juu ya uweledi.
 
Walimcheka wakamkeehi pale aliposema jamani tusitangaze idadi ya vifo wala maambukizi ya corona tutangaze wanaopona tu lakini takribani week moja mbele ushauri wake unafuatwa kimyakimya na heshima ya nchi yetu imeongezeka sana in a week
Dunia nzima inapigwa na butwaakwa namna gani Tanzania kwa mwezi na nusu ina vifo kumi tu ingawa wanatudharau
Neno linalostahili hapa ni Takataka!
 
Ha ha ha wee jamaa uandishi wako bana mtu anaweza kwenda chaka

Btw utoaji wa taarifa ni muhimu sana ili kujua maambukizi yapoje yanaongezeka au yanapungua maana watu wanaweza kuacha kuchukua tahadhari wakiamini ugonjwa umeisha kumbe hali bado tight
 
Hivi hakunaga wale international observers kama wakati wa uchaguzi waje watuupe ripoti kamili ya namna janga hili lilivyoweza kushughulikiwa vizuri na Tanzania? Yaani kama wale wa 'uhcaguzi ulikuwa huru na wa haki'?
 
Kwa sasa hv hakuna solution zaidi ya, self isolation, na social distancing. Jiokoe mwenyewe uokoe wengine hakuna dawa chukua tahadhari.

Sent using Jamii Forums mobile app

Nitayapata vipi mahitaji yangu kwa kujifungia na kukaa mbali? na kodi si nitashindwa kulipa na mapato kupungua? Hali ni mbaya sana ila kama imekwisha hivi..mbona hawatangazi tena
 
Ongeza limao na tangawizi kisha jifukize mkuu, kulialia haitokusaidia katu.
 
Nashindwa kuielewa serikali ya nchi hii inayoongozwa na rais Magufuli, tena ni serikali iyowajaa wasomi kuanzia rais, mawaziri na makatibu wakuu wote wamesoma, kiufupi phds zimejaa serikalini

Lakini ajabu kubwa na hii ipo Tanzania pekee, serikali yetu umechukulia ugonjwa wa corona ni kama aibu kwa serikali
Mtu akiathirika na covid19 serikali inapata fedheha na aibu kubwa

Mbaya zaidi inapotokea viongozi wa nchi hii wamekutwa na corona na kupelekea vifo hapo ndio kabisa serikali haiwezi kuiweka wazi aibu hiyo

Shida ni nini hapa Tanzania? Huko Ulaya na duniani kote mambo ni tofauti, waziri mkuu wa nchi kuumwa corona ni kawaida na dunia nzima hutaarifiwa, Uingereza ni kawaida na waziri amepona kwa sasa yupo kazini

Tanzania tunakwama wapi, Je corona ni aibu kwa nchi na serikali?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom