#COVID19 Mtazamo, Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Serikali na Wananchi kuhusu Ugonjwa wa Corona - COVID-19
Mi sijielewi nipo upande gani! Nikiwaza jinsi ugonjwa huu ulivowatikisa wazungu napata mashaka na kumpinga Mr stone kwa hatua anazochukua, pia nkifikir kuhusu the new world order na jinsi mabeberu wanavoipelekesha Dunia, natamani MAGUFULI apate zaidi ya nguvu alizokuwa nazo MUAMAR GADDAFI au MUGABE

Tusonge kivyetuvyetu tuachane na hao waharibifu wa Dunia ingawa sio rahisi na maisha yatakuwa magumu kwelikweli

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo kwenye new world order mnamaanisha nini!??
 
Sasa ndugu yetu Magufuli ametukimbia Dar es salaam na amekimbilia mafichoni huko kwao chato akijua kuwa kule corona haiwezi fika,kwa nini hajakaa na sisi DSM atufariji na ashirikiane na viongozi wengine kusaidia janga hili?
Kwani Tanzania ni Dar tu?
Rais yupo kwenye mapumziko ya pasaka,acha nongwa
 
Heri ya pasaka kwa wakristo wote na Watanzania wote kwa ujumla.Nianze kwa kufanya mrejeo wa tamko la wizara ya Afya kupitia waziri wetu Mh.Ummy Mwalimu ya kuwa tujiandae na maambukizi ya ndani kwa ndani,ikiwa kama ndiyo hivyo.Mimi kama mtanzania nashauri yafuatayo ili kuweza kukabiliana na maambukizi hayo
1.Ikiwa kama serikali yetu tayari au tuna vifaa vya kutosha,basi visambazwe kwenye hospital zote,maabara na vituo vyote vya afya serikali na vya binafsi pia kwa idadi maalumu.
2.Mgonjwa yeyote atakayekuwa ameenda sehemu zote hizo kupata huduma za kimatibabu na akiwa na kifua,mafua au kama haelewi anachoumwa basi apimwe Corona tu.
3.Kama wagonjwa hao watapimwa na watakugundulika wana maambukizi au wana Corona basi watengwe kuanzia siku hiyo baada ya kugundulika na kupelekwa kwenye wodi mojawapo katika hospitali katika mkoa husika ambayo itatengwa kwa ajili ya wagonjwa wa Corona.

Nini faida ya hayo yote kwa mtazamo wangu
1.Tutapata kuwajua wagonjwa ambao wana corona na wapo mtaani lakini hawajijui.
2.Tutaweza kudhibiti maambukizi ya ndani kwa ndani kwani wagonjwa waliopatikana watakuwa wameshatengwa sehemu maalumu.
Mimi nimewaza hivyo kama mtanzania mwenzenu.
mazagaone@gmail.com
Mhitimu UDOM,
Job Seeker,
Mwanasayansi.
Sawa job seeker!
 
Akishakutwa na corona mkamweka kslantini je wale ambao aliishi nao alikotoka je?
 
Katika hili mimi nipo na rais Magu
Mafua hayajawahi kumsumbua mtu mweusi
New World Order inataka kutupelekesha ili wauze sanitization chemicals na masks
Mitusi ruksa
Hao waliokufa na waliokarantini tz ni weupe?
 
Nimekuwa nikifuatilia mijadala humu hasa ile ihusuyo ugonjwa hatari dunia ni Wa covid-19.

Mara baada ya ugonjwa kutangazwa umeingia nchini, Serikali ilikuwa imeshajua na kuona ni halali kututangazia ili tuanze kujilinda,siku Moja kabla ya kutangaza Magufuli aliondoka DSM kwa njia ya barabara tukiaminishwa alikuwa anakagua miradi na madaraja yaliyovunjika na kuwatumbua watu kwa kile kilichozaniwa ni uzembe kazini,tuliaminishwa Magufuli anakwenda Dodoma kwani tayari alishasema yeye anahamia huko na watu tulikuwa tukisubiri yeye kuhamia huko kama ambavyo alikuwa amelieleza taifa.

Baada ya kufika Dodoma akalihutubia taifa akisema corona ni ka ugonjwa ka mlipuko kama ilivyo kwa ugonjwa wa kipindupindu au mengine na tena akasisitiza kuwa hana mpango wa kufunga mipaka kama wafanyavyo nchi zingine na majirani zetu limbukeni,akasema sisi tujilinde kwa kunawa na kumuomba MUNGU tu jambo ambalo liliwavutia sana viongozi wa dini na akasifiwa na viongozi hao,kwa nini wamsifie?tutajua baadae.

Mara baada ya hotuba hiyo hakukaa tena kwa wagogo mara huyo akakimbilia chato ambapo ndipo alipo mpaka sasa.
Na hivi majuzi amesisitiza na kusema kuwa hawezi funga mipaka maana majilani zetu wanatutegemea sana,sasa sijajua majilani wapi wanatutegemea ili hali wao wamefunga mipaka?

Waziri wa afya ametoa msisitizo na kuonyesha hofu ya ugonjwa kulipuka sasa lkn siku kadhaa baada ya kuonyesha hofu hiyo ametutangazia ongezeko la wagonjwa na vifo jambo ambalo limetushitua kwa kiasi kikubwa sisi wananchi lkn cha kushangaza ndugu Magufuli yeye halikumshitua na wala hayaongelei kabisa hasa pale anapokuwa anahutubia taifa na wala hatoi pole kwa wafiwa ni kama jambo la wananchi kufa kwa ugonjwa wa corona ni la kawaida kwake,ninapata wasiwasi sana hapa.

Niwarudishe Nyuma kwenye historia ya wana wa Israel wakati wanatoka utumwani kuelekea kaanan,waliongozwa na kiongozi wao Musa ambaye alikuwa bega kwa bega nao,alilala walipo lala,aliwafariji pale walipohitaji wafarajiwe,hakuna mahali aliwaacha peke yao wakipambana,pale yalipotokea magonjwa alikuwa mstari wa mbele kusaidiana nao.

Sasa ndugu yetu Magufuli ametukimbia Dar es salaam na amekimbilia mafichoni huko kwao chato akijua kuwa kule corona haiwezi fika,kwa nini hajakaa na sisi DSM atufariji na ashirikiane na viongozi wengine kusaidia janga hili?

Kumekuwa na watu wanaounga mkono hotuba zake za kutochukua tahadhali zaidi ya ugonjwa huu,miungoni mwa wapiga mapambio ambao binafsi nawaiata wajinga ni viongozi wa dini ambao wao kukosa sadaka ni zaidi ya corona.

Kama walituletea dini wao wamefunga majumba yao ya ibada ili kuepusha maambukizi sisi tulioletewa tena kwa Njia ya utumwa bado tumeshupaza mashingo na kujifanya sisi ni taifa teule la MUNGU wendawazimi mkubwa sana.

Ni Muda sasa tunahitaji Magufuli aje Dar es salaam tuungane naye ktk mapambano haya na sio yeye kutoa hotuba zake akiwa uhamishoni au huko alikojificha kwa kuogopa corona,asijidanganye hakuna MTU aliyeweza kuukimbia mkono wa MUNGU.
Aje achape Kazi pamoja nasi na sio yeye kujifungia kuogopa corona wakati anahamasisha wananchi wake wasiogope wachape Kazi,aje aanze na ziara za kushtukiza bandarini,tra na maofisi mengine mengi ili tuchape Kazi kwa pamoja.

Kama ndugu Magufuli akija na kukaa dar es salaam na tukamuona anafanya ziara za kikazi na kutuonyesha mfano wa kupiga Kazi bila kuogopa corona wengine wetu tutaamini sasa akisemacho anakimaanisha na hana mpango wa kututoa kafara,lkn asiporudi hapa bongo wengi wetu tutaamini hana nia njema na wananchi wake na atakuwa ameshiriki kwa Njia Moja ama nyingine kuwatoa kafara.

Watanzania tuache umbumbumbu tupende kuhoji wenyewe achana na viongozi wa dini wanaomezea sadaka zetu na wanaona waumini kikatazwa kwenda makanisani au misikitini ni pigo kwao.

Magufuli njoo Dar es salaam/nenda Dodoma tuchape Kazi kwa pamoja ili uwe na ufanano na Musa wa wana Israel ktk utendaji kwa watu wake tofauti na hivyo hutaaminika kamwe.

NB: corona covid-19 yaweza fika hata chato,kama imetoka China na kutembea nchi zote itashindwaje kufika huko hasa kwa nchi ambayo wananchi wake hawajadhibitiwa?

Niishie hapo kwa Leo.

Swelana.

Sent using Jamii Forums mobile app
post haina mashiko... utaanzaje kufananish Musa wa biblia na Magufuli ww... Mambo ya mungu hayausiani na hii kitu
 
Thubutu Magufuri afanane na Musa? We shika adabu yako marijuana na Musa wapi na wapi?
 
Heri ya pasaka kwa wakristo wote na Watanzania wote kwa ujumla.Nianze kwa kufanya mrejeo wa tamko la wizara ya Afya kupitia waziri wetu Mh.Ummy Mwalimu ya kuwa tujiandae na maambukizi ya ndani kwa ndani,ikiwa kama ndiyo hivyo.Mimi kama mtanzania nashauri yafuatayo ili kuweza kukabiliana na maambukizi hayo
1.Ikiwa kama serikali yetu tayari au tuna vifaa vya kutosha,basi visambazwe kwenye hospital zote,maabara na vituo vyote vya afya serikali na vya binafsi pia kwa idadi maalumu.
2.Mgonjwa yeyote atakayekuwa ameenda sehemu zote hizo kupata huduma za kimatibabu na akiwa na kifua,mafua au kama haelewi anachoumwa basi apimwe Corona tu.
3.Kama wagonjwa hao watapimwa na watakugundulika wana maambukizi au wana Corona basi watengwe kuanzia siku hiyo baada ya kugundulika na kupelekwa kwenye wodi mojawapo katika hospitali katika mkoa husika ambayo itatengwa kwa ajili ya wagonjwa wa Corona.

Nini faida ya hayo yote kwa mtazamo wangu
1.Tutapata kuwajua wagonjwa ambao wana corona na wapo mtaani lakini hawajijui.
2.Tutaweza kudhibiti maambukizi ya ndani kwa ndani kwani wagonjwa waliopatikana watakuwa wameshatengwa sehemu maalumu.
Mimi nimewaza hivyo kama mtanzania mwenzenu.
mazagaone@gmail.com
Mhitimu UDOM,
Job Seeker,
Mwanasayansi.
[/QUOTE
Wazo zuri sana
 
Wazo zuri
 
Nimesoma tu huko mwisho... Hiyo Email ya nini ndugu yangu?

Ili kupata projection ya uhalisia wa athari za Corona nchini kwetu kwa siku za usoni, ninaishauri serekali iwe ina monitor hii kitu inaitwa "Fatality Rate" ambayo inapatikana kwa ku calculate idadi ya vifo gawanya kwa jumla ya maambukizi.

Kwa kigezo hiki, takwimu hadi leo asubuhi zinaonyesha kuwa Tanzania ina "COVID-19 Fatality Rate" kubwa kuliko nchi zote katika EAC block, kama hesabu hizi hapa chini zinavyothibitisha:

Tanzania 1/20 = 5.0%
Kenya 3/110 = 2.7%
Rwanda 0/84 = 0%
Uganda 0/45 = 0%
Burundi 0/3 = 0%

Ili tuweze ku improve kwenye score hii, inabidi tuongeze uwezo (in terms of testing centres & equipment) wa upimaji ili tuwe na sample size kubwa.
updates ...

hadi kufikia leo hii tarehe 12 April, Tanzania bado inaongoza kwa "Fatality Rate" katika ukanda wa EAC kama takwimu zinavyoonekana hapa chini.

in fact, Tanzania ipo juu mara 2 zaidi ya Kenya and also ipo above the world average of around 6%.

Tanzania 3/32 = 9.4%
Kenya 8/197 = 4.1%
Rwanda 0/102 = 0%
Uganda 0/49 = 0%
Burundi 0/5 = 0%

nakazia tena ushauri wangu kwa serekali yetu kufanya monitoring ya takwimu hii kwani ndiyo kipimo muhimu cha uwezo wa nchi kukabiliana na hili janga especially kwa hizi nchi zetu ambazo uwezo wake kupima watu wengi ni mdogo.
 
Moja ya mabadiliko makubwa yatakayo baki hata baada ya corona kupunguza mashambulizi ni tabia ya kunawa mikono. Usishangae kukuta kila seat ya basi la luxury kuwa na chupa ya sanitizer. Hata kwenye ndege sanitizer kutolewa kwa wasafiri.

Kiwango cha malipo ya kadi ya benki bila kuweka nywila kuongezeka. Malipo ya contact less yameonekana kuwa salama zaidi katika maambukizi.

Madukani mengi yatafungwa kwa kukosa pango na mishahara ya wafanya kazi. Manunuzi mengi yatafanyika ki electronic.
 
Back
Top Bottom