#COVID19 Mtazamo, Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Serikali na Wananchi kuhusu Ugonjwa wa Corona - COVID-19
Sijasema data sio really, nimesema death zinasababishwa na other underlining issues za mgonjwa.
Kuhusu ventilators usitake kuniambia wakiokufa Tanzania, ni kwa sababu hawakuwekewa ventilator, bali wakiokufa kutokana na hizo underlining issue za mgonjwa, na rate ya wagonjwa kwetu imeongezeka siku tatu au nne zilizopita ambazo zinaweza kuwa caused na small mistakes walizofanya wagonjwa e.g. Prince Charles na kuwekewa kila kitu Mezani , kwenye gari na kuishia nyumba kubwa na hewa safi bado walipata, Pm wa UK, Mke wa Pm wa Canada, Coach wa Arsenal, owner wa Olympiakos the list is long

Mkuu wagonjwa wetu waliokufa wamekufa kwa Corona.

Hatua zisipochukuliwa tutakufa kwa Corona.

Tusiuvae uizraeli kuhalalisha idadi wala sababu za vifo vya Corona.

Ni ukweli uliowazi kuwa idadi ya maambukizi itakapokuwa kubwa (yaani litakapochanganya) vifo pia vitaongezeka.

Mgonjwa mmoja anaambukiza wengine hadi 90 katika kipindi chake cha ugonjwa wake kufikia kufa au kupona.

5% hadi 10% ya wagonjwa wote kutegemea na ubora wa huduma za afya katika sehemu au nchi husika wanakufa na ugonjwa huu.

Ugonjwa unakuwa umeshadhibitiwa kama wanaopona ni wachache kuliko wanaoambukizwa in a given time.

Huu ndiyo ukweli hapo. Hakuna cha ramli wala maombezi.

Corona ni uzembe wetu isingetufikia, na itatumaliza tusipoamka sasa - ukweli mchungu - JamiiForums
 
Mkuu tatizo hamsomi kujiridhisha kama unachoandika ni kigeni au kiliisha ongelewa. Mnakuwa kama mmewasili tokea sayari nyingine.

Inatia uvivu hata kuwajibu.

Hivi huu uzi uliuona? Hata Bakhresa katoa msaada kwenye baadhi ya hizo nchi kuunga mkono juhudi:

Hoja za wanaoona lockdown haifai ni zipi? Tuelimishane - JamiiForums

Kwa hiyo tatizo lako ni misaada ndiyo sasa mnakomoa nani hadi mpatiwe misaada?

Askofu Niwemugizi kaonyesha njia kuna ya kujifunza pale(ujasiri).
Kwa hiyo Awamu ya tano baada ya ku assess vitu ambavyo sio sustainable, wao hawajawa majasiri???
Na kutochukua vitu ulivyopendekeza ambavyo haviwezekani, kwako si sawa.
 
Kwa hiyo Awamu ya tano baada ya ku assess vitu ambavyo sio sustainable, wao hawajawa majasiri???
Na kutochukua vitu ulivyopendekeza ambavyo haviwezekani, kwako si sawa.

Sasa umebakiza sentensi 2. La kheri kwani tunapiga hatua bila shaka.

Unadhani hata pana haja ya mabishano mkuu?

Si muda mrefu umebakia mtakuwa mnaunga mkono juhudi kuliko hata sisi wengine.

Tofauti yenu na wengine si iko wazi?

Nyie mnaunga zote mkono bila kujali ni sahihi au la. Sasa atakapokuwa amefanya zile sahihi mtakuwa mmetuzidi kwenye uungaji mkono kwani wengine tunasubiria zilizo sahihi na za kijasiri peke yake ili tumuunge mkono.

Hii ni kama tunavyomuunga mkono baba Askofu Niwemugizi kwa ajili ya Nobel prize. Jitihada zake ni dhahiri katika kupunguza maambukizi ya Corona jimboni kwake.
 
Leo hii ni mwezi mmoja Sasa tangu tupate mgonjwa wa kwanza mwenye virusi vya Corona, ingawa Hadi Sasa tuna Visa vipatavyo 170. Kuna uwezekano Hali akazidi kuwa mbaya zaidi siku za usoni ingawa hatuombei Hali hiyo.

Kosa lililofanywa tangu awali Ni kusita kuchukua uamzi wa kufunga mipaka na kuzuia watu kutoka au kuingia nchini kwa wageni kutoka nchi zenye maambukizi. Hali hii ilipelekea mwingiliano ambao ndo matokeo ya maambukizi ya ndani kwa ndani tunayoyashuhudia kwa sasa.

Najua lengo kubwa la kushindwa kuchukua hatua za kufunga mipaka ilikuwa Ni kuhami mapato yatokanayo na utalii, lakini hapa tujiulize baada ya kuletewa gonjwa hili hao watalii na mapato yao yako wapi? Hakuna watalii Tena Bali tumebaki tunahangaika na gonjwa tuliloletewa huku shughuli nyingi za kiuchumi zikiathiriwa.

Viongozi wajifunze kupitia janga hili na isijirudie
 
Hivi Jamaica vipi bado tu hawana kisa hata kimoja?
 
Nikipitia kwenye mitandao mbalimbali, napata picha kuwa inawezekana maambukizi ya COVID-19 hapa nchini yamesambaa zaidi kuliko fahamu zetu za kawaida zinavyotupa taarifa.

Ili kudhibiti kuenea zaidi kwa maambukizi haya, inabidi kasi ya upimaji iongezeke maradufu (mass testing) ili walioambukizwa watambuliwe na kuwa isolated accordingly.

Kuna changamoto kadhaa dhidi ya utekelezaji wa mpango huu, lakini kwa leo tuzipitie hizi kubwa 3:

1) Uwezo mdogo wa serekali kufanya mass testing.
Solution: kama walivyopendekeza wadau kupitia platforms mbalimbali, mipango yote ya maendeleo inayotumia pesa nyingi sana kwa mabilioni na matrilioni (inajulikana) isimame kwa muda kwanza ili resources zote zielekezwe kwenye mapambano dhidi ya COVID-19 ikiwamo kununua/kutengeneza mobile testing kits za kutosha zitakazokuwa zinatembea mtaa kwa mtaa, na ikiwezekana nyumba kwa nyumba.

2) Uwezo mdogo wa serekali kuwa na vituo vya kutosha kuwatunza walioambukizwa wengi kwa mkupuo.
Solution ya changamoto hii ni pamoja na iliyotajwa kwenye # 1 hapo juu lakini pia iliyotajwa kwenye # 3 hapa chini.

3) Wananchi wanaogopa kupima kwa vile wengi wao hawataki kwenda kwenye confinement (isolation) ambako mazingira yake inasemekana siyo rafiki sana kwa sababu zilizo wazi lakini pia uwezekano wa kunyanyapaliwa.
Solution: baada ya kukamilisha upimaji kwenye kila kaya na kukagundulika maambukizi, serekali ijadiliane na kaya husika kama ina uwezo wa kufanya isolation within the premises. Cha msingi serekali ijiridhishe kuwa isolation kwa waathirika pale kwenye kaya ni jambo linalowezekana (kimiundombinu na kiuchumi). Ni wale waathirika ambao kaya wanazotoka haziwezi kuwahudumia hali wakiwa majumbani mwao ndiyo wawe wanapelekwa kwenye government sponsored isolation centres.
Solution hii pia ina address changamoto # 2 hapo juu.

Nihitimishe kwa kusema hivi... bila kujali tofauti ya itikadi au imani miongoni mwetu, Watanzania tulibebe hili tatizo tukiwa pamoja kama familia moja. Tuondoe siasa kabisa kwani hazitatufikisha kokote.

Tukifanya mass testing, itakuwa rahisi sana kama nchi kuwa na mkakati mzuri wa kuhakikisha kuwa maisha ya Watanzania wengi hayapotei kwa upande mmoja lakini pia kwa upande mwingine itakuwa rahisi kujijenga upya kiuchumi kama nchi (post COVID-19) kwani tutakuwa tunajua status ya afya ya nguvu kazi yetu.
 
Tuishinde COVID-19 kama tulivyomshinda dictator Iddi Amin Dada wa Uganda miaka ile.
tulikuwa kitu kimoja, viongozi wetu waliweza kutufanya tuongee lugha moja.
 
Corona ni janga la dunia, mabeberu imewatoa kamasi sembuse Jiwe..!!
 
Kumekuwa na kauli tofauti tofauti kuhusu viongozi wa kisiasa zinazohusu namna ya kupambana na maambukizi ya ugonjwa huu wa Corona ili usiendelee kuenea zaidi, japo zinakuwa na malengo mazuri lakini pindi zinapotofautiana zinaleta sintofahamu katika jamii.

Jana nimemsikia makonda akisema akifika kesho (Jumatatu) kila mkazi wa Dar avae barakoa ni lazima, RC Makonda akasema watu wakate hadi vipande vya kanga washonee barakoa wavae.

Leo nimeona clip ya video kutoka bungeni nadhani ya Naibu waziri wa afya akisema barakoa za vitambaa hazizuii na hazisaidii kabisa kuzuia kusambaa kwa virus vya Corona na kwamba zipo barakoa (Mask) maalum za kuzuia maambukizi hayo na hizo ndio zinatakiwa zivaliwe.

Hapa mbona mnawachanganya raia, wafauate lipi?
 
Kwa vile tuna tatizo ambalo linatukabiri na pia wataalamu walio na ujuzi wa kuwaelimisha Wananchi kuhusu nini cha kufanya wakati huu, ni vyema wasiohusika na taaluma hiyo wawaachie wahusika waelimishe Wananchi nini cha kufanya. Wanasiasa wao kila kitu wanajua. Matokeo yake tunayaona kwenye kila nyanja, si elimu, afya, uchumi, mawasiliano, you name it.
 
Kwa vile tuna tatizo ambalo linatukabiri na pia wataalamu walio na ujuzi wa kuwaelimisha Wananchi kuhusu nini cha kufanya wakati huu, ni vyema wasiohusika na taaluma hiyo wawaachie wahusika waelimishe Wananchi nini cha kufanya. Wanasiasa wao kila kitu wanajua. Matokeo yake tunayaona kwenye kila nyanja, si elimu, afya, uchumi, mawasiliano, you name it.
Wanawachanganya watu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom