Mtoto wa kaka yangu wa kwanza (First born) amebamiza 'A' za kutosha za darasa la nne mpaka nimeogopa sana, tutafute pesa Elimu nzuri ni gharama

Mtoto wa kaka yangu wa kwanza (First born) amebamiza 'A' za kutosha za darasa la nne mpaka nimeogopa sana, tutafute pesa Elimu nzuri ni gharama

Wakuu this is the first time nashuhudia kijana wa kaka yangu anafanya maajabu kama haya.

Kiufupi nimefurahi sana huyu angekuwa st kayumba sijui kama angepata hata A moja

Elimu nzuri ni gharama wakuu.

Kila mwaka inatoka mil 5 Ila matunda ni mazuri.

Ukiachana na hilo anaongea kiingereza Kama kiswahili.

Anajiamini
Anachambua mambo makubwa politics ,n.k

Elimu nzuri ni gharama.
Watakutana na Wakwangu wakiwa na Bahasha kutafuta kazi ya mshahara wa laki tano.

Wako kasoma kwa milioni 50 wangu kasoma kwa 1M tu.
 
Huwezi mchukua mtoto wa Feza Primary School uje umpambanishe na mtoto wa Mbagala Kuu Primary School.

Tusiongee saana, embu mtu mmoja aende ktk hizo shule akae ata lisaa tu kisha aje atupe ushuhuda ameona nini.

Zile shule kila muda ni safi, watoto wanapigwa na feni, vitabu na nyezo ni za kutosha. Mwalimu hana stress za mshahara, mwalimu na mwanafunzi wakiwa darasani wote tayari wamekula vizuri na kushiba, kuna hakuna ubuyu wala kachori. Kule mayai, maziwa, samaki n.k vitu ambavyo vinaboost akili ya mtoto.

Wakati mtoto anakula hivyo, huku Kayumba mwalimu tu samaki anakula mara moja au mbili kwa mwezi, akila samaki, kuku ni kama anasi kwake.
Kama kulinganisha tulinganishe wa Feza na wa St Marian. Wa mbagala na wa Mvomero.

To be fair
 
hakuna kitu kama hicho... mdogo wako namjua kalamba 4 ya 30 tuseme ukweli
Hahaaaa wueeeh!
Bahati mbaya siwezi weka evidence never.
Na hunifahamu kamwe,acha drama.
 
Niliwahi kwenda pale Agha Khan Primary School, ipo jirani na shule za Zanaki, Olympio na Diamond.

Umasikini ni mbaya tena ni laana, ee Mungu Baba tutoe huku. Wale watoto ukiwatazama wooote unawaona wamenawiri, wana afya, ngozi nyeusi ina mafuta mafuta yenye kupendeza.

Watoto wadogo wameshiba vizuri, uniform imekaa penyewe, imemtight vizuri. Vifungo vya shati vimebana, kiatu cheusi na soksi nyeupeee.

Hakuna mtoto asiyechana nywele, hakuna mtoto akiongea anarusha mate. Watoto wanacheza kistaarabu, muda wa kutoka pale nje hakuna bajaj au boda hata moja inayosubir kumchukua mtoto, nje kuna prado, harrier, benz, alphard n.k hizi IST, Raum, Rumion ambazo sisi tunatambazo nazo basi pale ndo gari za kwenda kuchukulia watoto.

Ukikaa pale kwa lisaa tu hakika utachukia hizi shule zetu za Kayumba. Walimu wapo smart, hakuna mwalimu kavaa kata K, hakuna mwalimu anayevaa suluari za malinda au zile suluari za karume za elfu tatu tatu sijui elfu nne.

Ee Mungu utusaidie.
Tatizo watanzania tumeshakariri kama umasikini ni sifa lakini uongo mbaya hakuna mtu asiyetaka mwanae asome pazuri
 
Tatizo watanzania tumeshakariri kama umasikini ni sifa lakini uongo mbaya hakuna mtu asiyetaka mwanae asome pazuri
Hapa watu wanaongea tu, ni sawa na mtu mwenye IST aseme gari yake na Cruiser VX zote sawa tu.
 
Huwezi mchukua mtoto wa Feza Primary School uje umpambanishe na mtoto wa Mbagala Kuu Primary School.

Tusiongee saana, embu mtu mmoja aende ktk hizo shule akae ata lisaa tu kisha aje atupe ushuhuda ameona nini.

Zile shule kila muda ni safi, watoto wanapigwa na feni, vitabu na nyezo ni za kutosha. Mwalimu hana stress za mshahara, mwalimu na mwanafunzi wakiwa darasani wote tayari wamekula vizuri na kushiba, hakuna ubuyu wala kachori. Kule mayai, maziwa, samaki n.k vitu ambavyo vinaboost akili ya mtoto.

Wakati mtoto anakula hivyo, huku Kayumba mwalimu tu samaki anakula mara moja au mbili kwa mwezi, akila samaki, kuku ni kama anasi kwake.
Hakuna ubuyu Wala kachori [emoji58]
 
St Kayumba tatizo linaanzia kwa waalimu wengi sana nimbumbumbu kwa sababu ya mifumo mibovu ya elimu tuliyonayo.
Na ujira kidogo wanao pata.
 
Back
Top Bottom