Mtu mwenye uwezo kuliko wewe kifedha unaweza kumpa zawadi gani?

Niliwaza kitenge pia ila daah 😁😁 sijui taste za mtu naweza kujita naishia kusengenywa.
 
Zawadi Ni Wewe Mgeni Wao Inatosha,,Si Unoana Hadi Zawadi Ya Kwenda Nayo Unaumiza Kichwa Hadi Kuja Kuuliza Humu,,Mimi Kanuni Yangu Nikiwa Naenda Kwa Aliye Nizidi Sibebi Zawadi Kamwe,,Bali Huwaga Nahakikisha Mimi Ndio Natoka Na Zawadi Kwao...​
Ngoja na mimi nichekeche kichwa naweza kwenda mikono mitupu 🤣🤣 au nikiona sielewi siendi
 
Wazo zuri ila kuku wa kienyeji katikati ya jiji unampataje?
Kama upo Dar unawapata soko la Kisutu hapo wazima kabisa.
Kama unatoka Lumumba unaenda soko la Kisutu kabla hujavuka Bibi Titi Road jirani na City Mall.

Ikiwa maeneo karibu na Mwenge au Shekilango masoko ya maeneo hayo wapo kote.

Kama upo Mwanza, Arusha, Dodoma zipo sehemu wadau watakujuza.
 
Asante. Ingawa sipo kote huko
 
Yule mzungu alipatiwa zawadi ya ngao ya TUZO ya heshima kwa kumfundisha injili,pia alipewa zawadi ya shati la batiki haya ya culture ya kiafrika kama aliyokuwa anavaa mpoto LENYE picha ya bendera ya Africa.

Na keki tukakata keki..kumshukuru kwa kutufundisha injili ya NENO la MUNGU.
 

Bendera***ramani ya Africa not bendera
 
Habari zenu wakuu.
Tufanye una ndugu au jamaa yako aliyekupita mbali kifedha, unaweza kumbebea zawadi gani ili usiende mikono mitupu? Ile imetokea tu unataka kwenda kumtembelea sio kwamba ni mgonjwa au ana changamoto yoyyoyote
Beba kuku hata watatu wa kienyeji, Michele hata kilo 50 na ndizi mzuzu na maparachichi. Kwetu unyakusani hapo umemaliza
 
Habari zenu wakuu.
Tufanye una ndugu au jamaa yako aliyekupita mbali kifedha, unaweza kumbebea zawadi gani ili usiende mikono mitupu? Ile imetokea tu unataka kwenda kumtembelea sio kwamba ni mgonjwa au ana changamoto yoyote.
Mnunulie kitabu cha 48 laws of power.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…