Mume adaiwa kumuua mkewe kwa risasi huko Bunju, Dar es Salaam

Mume adaiwa kumuua mkewe kwa risasi huko Bunju, Dar es Salaam

Moja ya vitu vinavyoleta mauaji ni kutokuwepo uaminifu miongoni mwa wanandoa,hii inapekekea mmoja anachanganya familia,yaani unakuta watoto wote wanne siyo wako na mume anaamini ni wake siku zote na jamii inaamini hivyo.
Siku ikija kujulikana,na mbaya zaidi mume akaunganisha matukio mbalimbali kama mke kuomba talaka ambapo itaambatana na kugawana mali ili akaushi vizuri na aliyemzalisha,ndo mwisho wa siku mtu anapigwa risasi.
 
Mwanaume aliyetambulika kwa jina la Laurent Kweka anatuhumiwa kumuua Mkewe, aliyefahamika kwa jina la Jenipher, kwa kumpiga risasi nyumbani kwao Bunju A, Mtaa wa Mkoani, Zone ya Senzele, Dar es salaam.

Akizungumza kuhusu tukio hilo, Mwenyekiti wa Shina la Mtaa wa Mkoani, Lucia Shirima, amesema tukio hilo lilitokea alfajiri ya Oktoba 1, 2026, ambapo alipigiwa simu na Mfanyakazi wa ndani wa familia hiyo aliyemweleza kuwa, “Baba amemuua Mama.”

Shirima amesema baada ya kupokea taarifa hiyo alifika eneo la tukio na kuwasiliana na Viongozi pamoja na Polisi, ambao baadaye walifika katika nyumba hiyo.

Kwa mujibu wa Shirima, walipoingia ndani waliukuta mwili wa Jenipher ukiwa upande wa kushoto, pembeni ya kitanda, huku Mumewe akiwa hayupo eneo la tukio ambapo baadaye alipata taarifa kuwa Kweka alikuwa amekwenda kujisalimisha Polisi.

Jitihada za kupata taarifa rasmi kutoka Jeshi la Polisi kuhusu tukio hilo zinaendelea, na tulipowasiliana kwa simu, tulielezwa kuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Jumanne Muliro, hakuwepo, huku simu ya Kaimu Kamanda ikiita bila kupokelewa.

Unahisi nini kinasababisha matukio ya ukatili na mauaji kuongezeka ndani ya ndoa na familia zetu siku hizi, na nini kifanyike kuzuia majanga haya?

Video:
View: https://www.facebook.com/share/v/189ju9sdmC/

Huyu wangemuweka gereza moja na yule Khamis wa kigamboni halafu yule Khamis nilisikia atatoa kitabu wangeshirikiana na huyu nazani wangetoa kitabu bora tungepata mafunzo kutoka kwao
 
Duh poleni sana
Ila jamaa kafanya maamuzi
Ya hasira inawezekana kauli zilitoka zikamtia gazabu
Duh alafu kajipeleka polisi mwenyewe

Ova
Usuper woman.. Hata mimi najiweza.!

Wakati anaongea hivyo kawezeshwa na alikuja yeye ns Maku yake wakati anaolewa

Wanawake wapunguze ujuaji wataokoa si katerero tu na maisha pia

NB: TZ kwa Sasa Kuna damu za watoto waliouwawa zinadai haki kwa baba zao na wajomba zao.. Usipokuwa makini unaweza kufanya vitu hatari Kwa mwenza.. Wingu la damu limetanda be awere na milipuko ya gadhabu
 
Bwana Kweka ameshindwa kudhibiti hasira zake hadi kufikia hatua ya kumuua mkewe, that's too bad.

Tusifike huko wanandoa, mambo yakiwa magumu tupeane nafasi, tutengane na yakishindikana tuachane kaa amani.

Lengo ni kulea hawa watoto pamoja, ila mambo yakiwa magumu hata remotely watalelewa tu.
Mkuu

Kinacho tutenganisha ni kifo tuu
 
Ndoa hazijawahi kukosa changamoto tangu zamani enzi hizo za akina chifu Mangungo ila kizazi chetu ndio tuna mioyo miepesi.
Wazee wa zamani wamelea sana watoto ambao sio wao kwenye ndoa. Unakuta mtoto wa mwisho au wa tatu ni wa mzee mwingine na mzee analea au mtoto anapelekwa kwa bibi yake na ndoa inaendelea. Au mzee anazaa nje ya ndoa akiwa ndani ya ndoa na mama haondoki wala nini.

Sihalalishi kuwa tufanye hivyo kuzaa nje ya ndoa au kufanya usaliti bali tuwe hata na nusu ya mioyo ya watu wa zamani ambapo ni kutengana kwa amani. Mioyo miepesi sio tu kuwa kwenye usaliti bali pia kwenye mali.
 
Ndoa hazijawahi kukosa changamoto tangu zamani enzi hizo za akina chifu Mangungo ila kizazi chetu ndio tuna mioyo miepesi.
Wazee wa zamani wamelea sana watoto ambao sio wao kwenye ndoa. Unakuta mtoto wa mwisho au wa tatu ni wa mzee mwingine na mzee analea au mtoto anapelekwa kwa bibi yake na ndoa inaendelea. Au mzee anazaa nje ya ndoa akiwa ndani ya ndoa na mama haondoki wala nini.

Sihalalishi kuwa tufanye hivyo kuzaa nje ya ndoa au kufanya usaliti bali tuwe hata na nusu ya mioyo ya watu wa zamani ambapo ni kutengana kwa amani. Mioyo miepesi sio tu kuwa kwenye usaliti bali pia kwenye mali.
Zamani watoto ilikuwa ni utajiri sasahivi watoto ni majukumu,jua kutofautisha hicho.
 
Baadhi ya mali zitauzwa; Watafunguliwa trust fund ambayo itatumika kuwasomesha mpaka university. Atateuliwa ndugu wa kuishi na watoto mpaka hapo watakapojiweza wenyewe. Kwa kipindi chote hicho baba atakuwa jela kutumikia kifungo.
Nani atayasimamia hayo? Hao watoto wanaenda kuteseka Amini nakuambia! Tuliopitia uyatima tunajua hayo.
 
Back
Top Bottom