Dogo bado mchanga sana. Chukua hii shule;
Alipaswa aseme hivi:
"Nisamehe mume wangu, sikukusudia kukukosea."
Ukiangalia in 6 dimensions hayo maneno yake ya mwanzo ni kama kejeli, sio msamaha.. anasema "kama", so haamini kama kakukosea.
"Ukiwa na Mb nakuomba jifunze" ... Kwa hiyo dogo kuna muda unakuwa huna Mb, si ndio? Sawa.
Maneno "nakuomba jifunze" ni maneno ya mtu mjivuni sana, kimsingi hajakuomba, that's a command brother. Alipaswa aseme "Nitafurahi tukijifunza zaidi kuhusu...." Kwenye kujifunza yeye keshagraduate ndo mana kajitoa, na wewe hamna unachojua, badala ya kuongeza ujuzi anakwambia ujifunze, sivyo? Freshi.
Then neno nakupenda halina hisia kama hajakuita jina zuri. Nakupenda whichi ipo plain ivoo? Haina mayai wala kachumbari 😆.. She had to say "nakupenda mume wangu/mpenzi wangu/kipenzi changu"
Naungana na wadau wanaosema hako katoto ni kajuaji; unyenyekevu zero(0%).
That's your headache, endelea kumeza panado taratiibu, hakunaga aliyekamilika.