Mungu wa miujiza mbona sijawahi kumwona? Au kuona miujiza yake?

Kiukwel hapo Cha kukushauli ni kwamba wewe amini unacho kiamin usifate watu fanya maamuzi wewe kama wewe unacho ona ni sahihi fanya hicho hicho ili usije kumtupia fran mzigo wa lawama
Kwani unacho kijua humu duniani ulikijua mwenyewe au kupitia watu?
 
Belief that you belief na kama kuna wewe hauami waache wanaoamini.
Hukatazwi kuamini. Na wala hakuna aliye katazwa kuamini.

Kuamini ni uhuru wako na haki yako ya kikatiba.

Lakini, Kuamini unaweza kuamini hata uongo.

Mtu anaweza kuamini kwamba akiruka kutoka ghorofa ya kumi na mbili hadi chini hatoumia na wala hatokufa.

Lakini kiuhalisia sikweli, ni imani yake tu. isiyo na ukweli. Lakini ni haki yake kuamini hivyo, ijapokuwa kiuhalisia ni imani ya uongo.

Vivyo hivyo, kwenye imani za Mungu.

Unathibitishaje kwamba imani yako ya huyo Mungu ni ukweli na si uongo?

Kwa sababu kuamini unaweza kuamini hata uongo.

Sasa unathibitishaje imani yako ya Mungu ni ukweli?
Hii yote inayosababisia discusion ni elimu tuliyoletewa na wazungu
 
Nimekuelewa vyema mkuu.

Kwa hapa tulipofikia kwangu linabaki kua swala la Imani.
Sasa masuala ya imani, ni myths na hayana ukweli.

Kwa sababu kwa imani, unaweza kuamini hata uongo.

Lakini ili tuweze kujua ukweli uko wapi, lazima kuwepo uthibitisho.

Kwa sababu mtu anaweza kuamini hata uongo.

Na msingi wa imani ni kutokuwa na uhakika wala uthibitisho.

Hakuna mtu anaye katazwa kuamini.

Lakini mtu akianza kudai kwamba imani yake ni ukweli lazima athibitishe.
 
Je, kama sisi ni wanyama mbona hatujaweza kuimpose hizi dhana kwao, mfano mnyama kama simba anaweza kuwa simba mwenzie katika kupata jike la kupanda... Is there any morarity in that?

Na je kwanini sisi tunawekeana hukumu? Na kuwa ni dhambi kuchapiwa mke?

Je, hiyo ni dhambi katika muktadha wa nature?

Na hiyo hukumubunayoizungumzia ni kweli utahukumiwa, ni kiumbe gani wa kuku hukumu ukifa na unakuwa huna ufahamu wa aina yoyote?

Huoni kuwa ni man made conception kuwa ukifa kuna sehemu utaenda kuhukumiwa?
 
Na msingi wa imani ni kutokuwa na uhakika wala uthibitisho
Facts, ila imani pia huponya, cell za binadamu huanza kuvibrate according to the frequency of your thoughts

Ndo maana kuna placebo effect
 
Watoto wadogo tu ndo huwa wanajiuliza kuhusu Mungu ila watu wazima wengi tayari wanajua uwepo wake , la muhimu zaid em jifunze kumjua Mungu na Mungu sio babaako anajibu kwa muda anao taka yeye ukitaka ishara hizo za fasta fasta huwez kuziona .

Uumbaji wa viumbe hai na universe hii inatosha kukuthibitishia kua Mungu yupo
 
Facts, ila imani pia huponya, cell za binadamu huanza kuvibrate according to the frequency of your thoughts

Ndo maana kuna placebo effect
Pia imani huaribu.

Lile tukio lililotokea kule Msitu wa Shakahola Kenya, Wale waumini wa mchungaji Paul Mackenzie yule aliyewaambia wafunge hadi kufa bila kula chochote, na waumini wale wakaamini na kufunga kweli hadi wakafa mamia kwa mamia. Ni uthibitisho kwamba imani huaribu pia.

Ukiwa na imani sahihi yenye ukweli inaponya kweli. Mfano mwanafunzi mwenye imani kwamba akisoma kwa bidii atafaulu mtihani. Imani hii ni nzuri na ina ukweli. Na itamsaidia.

Ukiwa na imani ya uongo, isiyo na ukweli, unapotea Mfano, Mtu anaweza kuamini kwamba akitupwa kwenye Simba wakali porini hatoliwa na Simba kama Daniel wa kwenye Biblia. Kwamba Mungu atamuokoa. Kumbe sikweli na ni uongo.

Hapa sasa inategemeana ukweli wa hiyo imani inayoaminiwa na mhusika.

Imani zingine sio, unaingia chaka.
 
Na msingi wa imani ni kutokuwa na uhakika wala uthibitisho.
Lakini mtu akianza kudai kwamba imani yake ni ukweli lazima athibitishe.
Rafiki, bado hujajua maana halisi ya imani.
Ebr 11:1-3
"...imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana."

Humu JF nimethibitisha mara nyingi uwepo wa Mungu kwa kusimulia matendo ya miujiza aliyonifanyia Mungu, lakini kama Smart911 anavyosema kila mara: "watu wa siku hizi ni wabishi."
Hata akitokea malaika wataendelea tu kusema "Mbona Mungu wa miujiza sijamuona"

Lakini sababu kuu ya wao kukosa imani tunaijua:
2 Kor 4:4
"...ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikra zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu."

HATUKATI TAMAA, TUNAENDELEA KUWAOMBEA, NURU YA INJILI IWAZUKIE
 
Uhakika ni nini?
 
Mawazo finyu hasa dunia ya tatu ndio wanaotegemea miugiza!!
 
Hapana...Kila Mwanadamu amepewa chances sawa. Kila mwanadamu anazaliwa akiwa katika maumbile ya dini ya kiislam ila wazazi wake wawili ndio humbadili mtoto na kumpeleka katika dini nyingine.
Anayezaliwa leo hii viungani hapo vatican, na anayezaliwa leo hii viungani hapo mecca. , huwezi sema wana chance sawa, wewe unaona wanachamce sawa hawa?

Yani mtu azaliwe sudan, gaza au hata viunga vya kongo hapo useme wanachance sawa na wengine
 
Kwa hiyo sukari ya kwenye matunda ndiye Mungu?

Kwa nini binadamu tunakuwa wepesi kuamini vitu tu sivyo na ujuzi wowote navyo?
Rudi usome vizuri kaka/dada alafu uje tuendelee na mdahalo!
 
Wewe umemuelezea "Mungu" ilihali mimi niliandika "mungu"
 
Mungu yuko nje ya mfumo wa Muda

Big Bang ndiyo iliyotengeneza Muda na space

Yule aliyesababisha Big Bang llazima alikuwepo kabla ya muda kuanza.

Na huyo ndo Mungu- alikuepo na ataendelea kuepo
Je una uhakika kuwa aliyekuwepo before ni Mungu? Je ufahamu huu ambao ili uwe na maana lazima kuwepo na muda Umejuaje kuwa kuna kitu beyond muda?
 
Uhakika ni nini?
Sidhani kama definition itakusaidia.
Ngoja nikuelezee kwa kukupa mifano: Mungu ameahidi katika kitabu cha Mathayo 7:7 kwamba tukiomba tutapewa. Mtu mwenye imani haombi kwa kubahatisha. Anaomba huku akiwa na uhakika kuwa atapewa kile anachoomba. Ndivyo tunavyofanya sisi tunaoamini. Tuna confidence/certainty kwamba ahadi hiyo ni ya kweli na ataitimiza, kwa kuwa tunajua Mungu yupo na ni muweza wa yote.

Wewe ukiambiwa na Trump uende akupe US Dollars 10,000 utaenda with confidence kuwa atakupa kwakuwa unajua yupo na ana uwezo wa kukupa pesa hiyo.

Sasa sisi tunaoamini tunajuaje Mungu yupo? Ushahidi kuwa Mungu yupo ni ujio wa Yesu Kristo duniani. Mungu aliupenda ulimwengu akamtoa Yesu aje duniani ili kila amwaminiye asipotee. Yesu alikuja duniani akakaa na wanadamu, ndio sababu anaitwa Emanueli, yaani Mungu pamoja nasi. Yesu alifanya miujiza mingi. Aliponya wagonjwa, aliwalisha maelfu mikate, alifufua wafu... Hiyo inadhihirisha uwezo wa Mungu wa kufanya jambo lolote. Ndio sababu tunapoomba tuna confidence kwamba tutapewa mahitaji yetu au kutendewa miujiza. Hiyo ndiyo imani. Sio bahati nasibu.

Sijui kama nimeeleweka, my learned friend.
 
Karibu katika dini ya Uislam. Dini ambayo umeumbiwa nayo kabla ya wazazi wako kukubatiza na kukufanya uwe mkristo
Sawa Elezea kwa namna itakayo nifanya Niamini kuwa Dini ya kiislamu inaelezea Mungu wa kweli na tmuthibitishe kuwa yeye ndiye Mungu wa kweli
 
Mungu yupo ila alivotafsiliwa kwenye dini ni mafumbo tu.

Yahitaji hakiri ya utulivu sana hata kuielewa biblia au neno la Mungu.

Mim naweza kusema Mungu ni NATURE yenyew iliyo umba au kufanya kila kitu kiwepo au kifanyike na ikaweka sheria zake ziakisi kwa chochote kitendekacho kiwe kizuri ama kibaya.

Na biblia ndo ina code zote jinsi binadam aishi.
ila ukiisoma kichwa kichwa unasema ni story tu na usielewe chochote.

Ni somo lefu mpaka uje uelewe
 
Unaona ambavyo muwa unakua na maji matamu (sukari) ndani yak, Ni tofauti na Bamboo ambayo haina sukari na yote ni ya jamii moja.... Ndio huyo "mungu" ambaye hujawahi kumuona kafanya....

kumbuka udongo hauna sukari
Daah! Ng'ombe akipewa sumu anakufa!
 
Kabla ya Big Bang, dhana ya sekunde, dakika au jana na kesho hikuwapo kwa sababu hakukuwa na nafasi (space) wala maada (matter) zinazosogea ili kuwezesha muda kuhesabika
Unaweza kuelezea concept ya Time? au kwako time ni order of events?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…