Mungu wa miujiza mbona sijawahi kumwona? Au kuona miujiza yake?

SIku ukiweza kuachana na kuwaza maswala ya dini na mambo yake ,bac nikuhakikishie mkuu utaangaika hata nayo tena .maana dini n miradi ya watu kama ww vile uamue kuanzisha tu mradi wako na uangalie soko lako litakuwa ktk nchin gan upige hela za wateja na ndicho katoliki na islami walichowini ktk bara hili la GIZA .
Kwamba ilikuwa ni biashara ya kuteka imani za watu katika yasiyo onekana?
 
Neno Imani linamaana ya kuamini mambo yaliyofichikana kwa yakini kutoka moyoni pasi na chembe ya shaka ndani yake.
Suala la kusema kuwa bora niamini tu kuwa Mungu yupo ili hata nisipomkuta niwe safe huu ni UNAFIKI. Ina maana bado moyo wako unashaka.

Pia mwanadamu mwenye akili hawezi kuhangaika kutafuta miujiza ya Mungu ili hali Mungu kaweka kila aina ya ishara za uwepo wake ndani ya miili yetu na mazingira yanayotuzunguka.

Kinachotakikana ni kukaa na kutulia kisha utafakari jinsi ulimwengu unavyofanya kazi kuanzia asubuhi mpaka usiku. Kisha jiulize Je hays yamefanyika tu bure out of nowhere?
Je unaweza kutrace uwepo wa Mungu katika haya uliyo ya andika kwamba nikikaa tokea asubuhi mpaka jioni nitajua na kuona uwepo wa Mungu?

Na utajua je kuwa kuna creator just by observation?
 
Imani ni Mtihani wa "Ghaibu" (Mambo Yasiyoonekana/unseen )

Lengo la maisha ya dunia ni mtihani. Kama Mwenyezi Mungu angeonekana waziwazi kwa macho ya kila mtu, kusingekuwa na maana ya "Imani" (kuamini kisichoonekana) na kusingekuwa na mtihani tena, kwani kila mtu angelazimika kuamini.
Qur'ani inaanza kwa kusifu wale wanaoamini mambo yasiyoonekana kwa macho lakini yanathibitika kwa akili na mioyo:

"Hichi ni Kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake, ni uwongofu kwa wacha-mungu. Ambao wanaiamini ghaibu (yasiyoonekana)..." — (Surat Al-Baqarah, 2:2-3)

Nihitimishe kwa kusema kuwa :

Huwezi kumwona Mungu kwa macho, lakini unaweza kumwona kupitia kazi Zake. Kama vile usivyoweza kuona upepo au akili, lakini unaona athari zake—vivyo hivyo ulimwengu thabiti, mapigo ya moyo wako, na mifumo ya nyota ni ushahidi na miujiza tosha ya uwepo wa Muumba.
Asante kwa tathmini hii, ndo maana unaambiwa Mungu hayupo nje yako,

Mungu ni awareness ya kujua kitu kina affect maisha yako... Kwamba kuna planes of awareness unakuwa umefikia karibu na God's consciousness.

Je, unaongelea je hii dhana ya watu kuamini kuomba kitu kilicho nje yako na kuponywa? Hii imekaaje? Unadhani kuomba kuwa kuna mtu au kitu kinakusikia nje yako kunasaidia?
 
Dini ni utaratibu wa maisha tu ambapo tumewekewa mtawala ambaye hakuna wa kumuhoji wala kumkosoa. Yeye ni alpha na omega ila hayupo.

Kila jamii ina dini zake na Mungu wake. Tatzo linakuja kwetu sisi badala ya kuabudi babu yako wa kishumundu unaabudu babu wa waisrael Yesu na babu wa waarabu Mohamedi.....
 
Lengo la mtihani ni nini mkuu
Haha jinsi tunavotita mtihani huenda tunakosea? Ila yawezekana ni mtihani maana Avery thing you do needs some sort of figuring things out, hauwezi kujua pasipo experience yenyewe
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Mtoa post nataka nijibu swali lako

1. Kwa nini Hatuwezi Kumwona Mwenyezi Mungu Katika Dunia Hii?

Katika maisha haya ya dunia, binadamu hana uwezo wa kimaumbile (kifiziolojia na kiroho) wa kustahimili kumuona Mwenyezi Mungu kwa macho ya nyama. Macho yetu yana ukomo mkubwa sana.
Kutoka kwenye Qur'ani:

Mwenyezi Mungu anasema wazi kuwa macho ya viumbe hayawezi kumfikia au kumzunguka kwa kumuona hapa duniani:

"Macho hayamfikilii (hayamwoni), bali Yeye anayafikilia macho. Naye ni Mpole, Mwenye khabari." — (Surat Al-An'am, 6:103)

Hata Mtume Musa (Alayhi Salam) alipoomba amwone Mwenyezi Mungu, milima ilisambaratika kwa sababu haikuweza kustahimili utukufu wa Mungu:

"Na Musa alipokuja kwenye miadi Yetu, na Mola wake Mlezi akasema naye, (Musa) alisema: 'Mola wangu Mlezi! nionyeshe nikutazame.' (Mwenyezi Mungu) akasema: 'Hutaniona. Lakini utazame huo mlima; ukikaa pahala pake basi ndiyo utaniona.' Basi Mola wake Mlezi alipojidhihirisha kwenye mlima, aliufanya usawazike na ardhi, na Musa akaanguka chini amepoteza fahamu..." — (Surat Al-A'raf, 7:143)

Kutoka kwenye Hadithi:

Mtume Muhammad (S.A.W) aliulizwa kama amewahi kumwona Mwenyezi Mungu, naye akajibu:

"Ni Nur (Nuru), nitamwonaje?" — (Sahih Muslim)

(Hii ina maana kwamba pazia la Mwenyezi Mungu ni nuru kuu ambayo kiumbe hawezi kuitazama akaendelea kubaki salama).
Okay, sasa je huyo aliye nyuma ya pazia ni Mungu na muumba na muwe a wa yote aliyesema tukimwomba atatuponya?

Kama ni kweli je ni kwanini amejifiicha na itokee hata mara moja kujidhihirishfor the betterment of us believers?

Kwanini tukeshe tukio ba kwa kitu kilicho jificha?.

Huoni kuwa tunajidanganya tu, kwa stori za kale ambazo haazijirudii?
 
Wanabodi...

Poleni na majukumu ya week nzima, as we are welcoming another beautiful weekend.

Naomba tuongelee hili swala kidogo, tumeaminishwa kuhusu uwepo wa Mungu na miujiza yake ya kuponya viwete, kutenganisha bahari na hata kurudisha uhai kwa wafu.

Je Mungu huyo yupo?

Maana nimefika point sasa najiuliza sana, ya kuwa what if dini ni utapeli wa kihisia na imani kwa kitu ambacho hakipo?

What if miujiza tunavyo ambiwa kuwa ukiomba utapata ni kama dhana ya kutuweka tuendelee kuwa watumwa wa shida unazo zipitia?

Maana mimi nilisoma shule za kikatoliki na tukikuwa tunasali sana rosali kila siku, japo ilikuwa na msaada katika masomo na kutupa imani iliyo thabiti, ila bado watoto walikuwa na tabia mbaya sana,

Nakumbuka enzi hizo kulikuwa na Visungura, zile pombe za pakti. Vijana walikuwa wanavusha na kunywa, watu walikuwa wana ruka ukuta, na ikifika rosali wanasali na kutubu...

Ila pia hata kwenye maisha, watu wanahudhuria makanisani, ila bado wanazini na wake za watu,

Watu wanakesha makanisani ila bado wanafanya dhambi na kwenda tena kuomba Mungu awasamehe, je ndugu zangu dhambi ni kitu kibaya?

Mapadri wenyewe tu pia wanalala na kuzaa na wanawake kisiri

Sijawahi kuona mbwa anahukumiwa kwenda kuimba nyama jikoni, atapigwa na atajifunza kumbe kuchukua nyama ni kosa! sijawahi kuona dhambi ikiwa applied kwa kiumbe kingine ila binadamu tu.

Unakaa unajiuliza ni kwanini binadamu tunawekewa hukumu katika vitu na desire za kimwili ambazo muda mwingine ni haja za kinyama kabisa?

Je dini ni illusion? Na kama ni kweli kwanini binadamu amekuwa mgumu kukubali kuwa hakuna mtu aliye juu mawingu I anayemwangalia kila jambo analolifanya na kuna siku atamuhukumu kwenda kuchomwa moto wa milele?

Ndugu zangu, weekend hii tutaenda makanisani...

Je unakwenda kumwabudu Mungu, aliyeshuhsa mana katika ghalika la waizraeli? Ndiye Mungu aliye sambaratisha bahari ya shamu? Au ni tunakwenda kuabudu Mungu aliye bumbwa kwenye taswira ya binadamu wa kale?

Sijasema Dini ni mbaya, wala sijaikataa Dini ila nataka kujua na kuuliza ni kwanini binadamu hufwata kitu kisicho na maana kwa ajiri ya kupata comfort ya muda mfupi?

Lakini pia wanaoikataa Dini mbona hamna mahala mnaposema kuwa hichi mlicho kikuta kimeanzia, na chimbuko la mwanadamu ni hili? Kwa nini Msiwe delusional tu, ilihali mnapendana na kutakaina mema kwa manufaa ya jamii iliyo bora?

Mimi naamini kila kitu ni energy na hata hawa wanaoamini katika Dini si kwamba hawako sahihi, energy is incomprehensible hasa kwa limits zilizo kwenye mlango ya fahamu, so expression ya hiyo energy lazima iwe abstract, ndo maana kuna vitu kama miujiza, which are manifestaion of energy forms.

Swali ni je, Mungu huyo tunayekwenda kanisani kumwabudu ni yupi? Na mbona unaendelea kwenda ilihali hatumjui? (kwa sisi ambao hatujamwona)
USIPOTAKA KUMUONA, HUTOMUONA!!!
 
Kama huyo Mungu ndio kaumba viumbe wanaomkana, mwenye makosa ni nani hapo?

Yeye muumbaji?

Au viumbe?

Kwa sababu, Kiumbe hawezi kwenda kinyume na vile alivyoumbwa.

Kama Mungu aliumba viumbe wanao mkana, Basi mwenye makosa ni yeye mwenyewe!

Asilaumu viumbe wanaomkana. Kwa sababu muumbaji ni yeye mwenyewe.

Huyo Mungu, kama alijua hapendi kukanwa, angeweza kuumba binadamu wasio weza kumkana.

Angeumba binadamu wema na watiifu tu, wasioweza kumkana hata kidogo.

Kuumba binadamu ambao wanaweza kukukana, wakati unajua kabisa hupendi kunanwa, Halafu bado unalalamikia viumbe haohao wanakukana, Wakati uliwaumba mwenyewe wakukane, Ni ukichaa.

Huyo Mungu kama alijua hapendi kukanwa, Alishindwaje kuumba binadamu wema tu, watakao mtii siku zote na wakati wote bila kumkana?
Mungu alishaziumba nafsi zote za waja na zote akazikushanya sehemu moja na zikakiri kwamba hapana mola mwingine isipokuwa YEYE...kisha akazibainishia njia njema na potovu...kisha akazipa uhuru wa kuchagua njia inazozitaka.

Mungu hapendi uchafu wala kufuru.

Nafsi italipwa kile ilichochagua katika maisha haya ya dunia.
 
Okay, sasa je huyo aliye nyuma ya pazia ni Mungu na muumba na muwe a wa yote aliyesema tukimwomba atatuponya?

Kama ni kweli je ni kwanini amejifiicha na itokee hata mara moja kujidhihirishfor the betterment of us believers?

Kwanini tukeshe tukio ba kwa kitu kilicho jificha?.

Huoni kuwa tunajidanganya tu, kwa stori za kale ambazo haazijirudii?
Maisha ya dunia ni Mtihani wa imani.
Mungu ametuleta hapa duniani kutujaribu imani zetu juu yake na si kwamba alikuwa hajui nafsi zetu toka hapo mwanzo kuwa nini zitakuja kufanya hapa ulimwenguni. La hasha anajua ya nyuma na mbele yetu ila kuna hekima alitaka kuifanya. Nayo ni

*Kudhihirisha Ushahidi Dhidi ya Mwanadamu (Uadilifu wa Kiungu).

Mwenyezi Mungu anajua tangu mwanzo nani atafanya wema na nani atafanya uovu kwa sababu Yeye ana ujuzi wa mambo yaliyopita, yaliyopo, na yajayo (Ilm al-Ghaib). Hata hivyo, humpa mwanadamu uhuru wa kuchagua na kufanya vitendo hivyo ili:

• Ushahidi uwepo: Siku ya Kiyama, mtu asihukumiwe kwa kile ambacho Mungu alikuwa anajua angekifanya, bali ahukumiwe kwa kile alichokifanya yeye mwenyewe kwa mikono yake.

. Kama Mungu angewapeleka watu motoni au peponi kabla hawajaja duniani kwa kisingizio cha "Najua mgefanya hivi," wanadamu wangepinga wakisema: "Mbona hukutupa nafasi ya kujaribu? Tungefanya wema!" Dunia ni uwanja wa kudhihirisha vitendo hivyo ili mtu asione ameonewa.

Na jambo la kusema kuwa Mungu katuleta duniani ili atujaribu aone nani mwenye vitendo vyema haimaanishi kuwa Mungu alikuwa hajui nini tutakuja kukifanya hapa duniani.

Msingi hapa si kwamba Mungu anajifunza kitu kipya ambacho alikuwa hakijui. Badala yake, maana yake ni: "Ili kukuwekeni katika hali ambayo sifa zenu halisi (za wema au ubaya) zidhihirike wazi machoni penu na machoni pa viumbe wengine."

• Ni sawa na mwalimu anayejua darasani kwake nani ni mwanafunzi hodari na nani ni mvivu. Lakini mwalimu hawezi kutoa maksi au kufelisha mtu bila kutoa mtihani wa karatasi. Mtihani huo unalenga kudhihirisha ukweli wa uwezo wa mwanafunzi kwa vitendo.
 
Okay, sasa je huyo aliye nyuma ya pazia ni Mungu na muumba na muwe a wa yote aliyesema tukimwomba atatuponya?

Kama ni kweli je ni kwanini amejifiicha na itokee hata mara moja kujidhihirishfor the betterment of us believers?

Kwanini tukeshe tukio ba kwa kitu kilicho jificha?.

Huoni kuwa tunajidanganya tu, kwa stori za kale ambazo haazijirudii?
Pia uelewe kuwa Mungu ni mfalme.hivyo apokei amri,ushauri wala mapendekezo kutoka kwa yeyote...YEYE anafanya alitakalo.

Alishaamua kuwa wanadamu wala majini tusiweze kumuona katika maisha haya ya dunia. Imagine tungekuwa tunamuona Mungu ni nani angekufuru, nani angempinga Mungu...? nadhani dunia nzima ingekuwa na wachamungu...Ila kaamua tusimuone ili aone tutamuamini pasi na kumuona.? Ndio tunarudi ile kauli ya kwenye Quran kuwa...tumeumbwa ili tuje kufanyiwa majaribio.

Kitendo cha Mungu kuonekana kusingekuwa na maana ya kuumbwa Pepo na Moto, Kusingekuwa na maana ya kifo, kusingekuwa na maana ya uwepo wa siku ya Qiyama n.k
 
Anayezaliwa leo hii viungani hapo vatican, na anayezaliwa leo hii viungani hapo mecca. , huwezi sema wana chance sawa, wewe unaona wanachamce sawa hawa?

Yani mtu azaliwe sudan, gaza au hata viunga vya kongo hapo useme wanachance sawa na wengine
Kwenye Quran, Mungu amesema kuwa hamdhulumu mja bali mja hujidhulumu mwenyewe.

Swali lako linalenga kugusa dhana za uadilifu wa Mwenyezi Mungu (Al-Adl), uhuru wa kuchagua (Free Will), na jinsi binadamu anavyohukumiwa katika Uislamu.

Kijuujuu, inaweza kuonekana kama mtoto wa Kiislamu amependelewa. Hata hivyo, vyanzo vya Kiislamu (Qur'ani na Hadithi) vinaonyesha kuwa nafasi na fursa za kupata radhi za Mungu ziko sawa na kwa usawa kabisa, kwani kila mtu anahukumiwa kulingana na mazingira na kiwango cha maarifa alichopewa.

Kuna misingi minne inayofafanua usawa huo ila sitaki andiko liwe refu, nitakupa misingi miwili ya uadilifu wa Mungu katika jambo hili

1. Kila Mtoto Anazaliwa Katika "Fitrah" (Maumbile Safi ya Kiislamu)

Katika Uislamu, hakuna mtoto anayezaliwa akiwa Mkristo, Myahudi, au Mpagani. Kila mtoto anazaliwa akiwa na mwelekeo wa asili wa kumtambua Mungu mmoja (Fitrah). Mazingira na wazazi ndio wanaombadilisha baada ya kuzaliwa.

Kutoka kwenye Hadithi:

Mtume Muhammad (S.A.W) alisema:
"Kila mtoto anazaliwa katika maumbile safi (Fitrah), kisha wazazi wake humfanya kuwa Myahudi, au Mkristo, au Majusi (Mwabudu moto)..." — (Sahih al-Bukhari)

Hii ina maana kwamba machoni pa Mungu, watoto wote huanza mstari mmoja wa mwanzo wakiwa wasafi na sawa kabisa.

2. Kanuni ya "Hukumu Kulingana na Viwango vya Mtihani"

Mwenyezi Mungu habadilishi kanuni ya mtihani; anatoa mitihani tofauti lakini kwa uadilifu ule ule. Mtu aliyezaliwa kwenye mazingira ya Kiislamu ana mtihani tofauti na yule aliyezaliwa kwenye mazingira ya Kikristo:

• Mtihani wa Mtoto wa Kikristo: Mtihani wake ni "Kutafuta Ukweli" (The Test of Seeking Truth). Ikiwa atatumia akili yake vizuri, akahoji, na kutafuta ukweli kwa nia safi, Mungu humwongoza. Katika Uislamu, mtu anayetoka kwenye dini nyingine akasilimu hupata thawabu mara mbili (kwa mujibu wa Hadithi katika Sahih al-Bukhari), kwa sababu ya juhudi kubwa aliyofanya kupenya vikwazo vya kifamilia na kijamii.

• Mtihani wa Mtoto wa Kiislamu: Mtihani wake ni "Kulinda na Kutenda" (The Test of Preservation and Action).

Kuzaliwa Mwislamu hakukuhakikishii kwenda Peponi. Mara nyingi, watu wanaozaliwa kwenye Uislamu huchukulia dini kama mazoea (cultural Muslims). Mtihani wao ni mkubwa zaidi kwa sababu tayari wanajua sheria lakini wasipozifuata, au wakifanya madambi kama unafiki, adhabu yao inaweza kuwa kali zaidi kwa sababu walikuwa na elimu lakini hawakuifanyia kazi.
 
Hukatazwi kuamini. Na wala hakuna aliye katazwa kuamini.

Kuamini ni uhuru wako na haki yako ya kikatiba.

Lakini, Kuamini unaweza kuamini hata uongo.

Mtu anaweza kuamini kwamba akiruka kutoka ghorofa ya kumi na mbili hadi chini hatoumia na wala hatokufa.

Lakini kiuhalisia sikweli, ni imani yake tu. isiyo na ukweli. Lakini ni haki yake kuamini hivyo, ijapokuwa kiuhalisia ni imani ya uongo.

Vivyo hivyo, kwenye imani za Mungu.

Unathibitishaje kwamba imani yako ya huyo Mungu ni ukweli na si uongo?

Kwa sababu kuamini unaweza kuamini hata uongo.

Sasa unathibitishaje imani yako ya Mungu ni ukweli?
yote kwa yote suala la mungu tumezaliwa tumekuta hadithi za uwepo wake the same na mababu zetu ambao wamefaliki hatujawakuta mfano leo hii ukiambiwa uthibitishe kama walikuwepo ilihali hujawaona
 
Wanabodi...

Poleni na majukumu ya week nzima, as we are welcoming another beautiful weekend.

Naomba tuongelee hili swala kidogo, tumeaminishwa kuhusu uwepo wa Mungu na miujiza yake ya kuponya viwete, kutenganisha bahari na hata kurudisha uhai kwa wafu.

Je Mungu huyo yupo?

Maana nimefika point sasa najiuliza sana, ya kuwa what if dini ni utapeli wa kihisia na imani kwa kitu ambacho hakipo?

What if miujiza tunavyo ambiwa kuwa ukiomba utapata ni kama dhana ya kutuweka tuendelee kuwa watumwa wa shida unazo zipitia?

Maana mimi nilisoma shule za kikatoliki na tukikuwa tunasali sana rosali kila siku, japo ilikuwa na msaada katika masomo na kutupa imani iliyo thabiti, ila bado watoto walikuwa na tabia mbaya sana,

Nakumbuka enzi hizo kulikuwa na Visungura, zile pombe za pakti. Vijana walikuwa wanavusha na kunywa, watu walikuwa wana ruka ukuta, na ikifika rosali wanasali na kutubu...

Ila pia hata kwenye maisha, watu wanahudhuria makanisani, ila bado wanazini na wake za watu,

Watu wanakesha makanisani ila bado wanafanya dhambi na kwenda tena kuomba Mungu awasamehe, je ndugu zangu dhambi ni kitu kibaya?

Mapadri wenyewe tu pia wanalala na kuzaa na wanawake kisiri

Sijawahi kuona mbwa anahukumiwa kwenda kuimba nyama jikoni, atapigwa na atajifunza kumbe kuchukua nyama ni kosa! sijawahi kuona dhambi ikiwa applied kwa kiumbe kingine ila binadamu tu.

Unakaa unajiuliza ni kwanini binadamu tunawekewa hukumu katika vitu na desire za kimwili ambazo muda mwingine ni haja za kinyama kabisa?

Je dini ni illusion? Na kama ni kweli kwanini binadamu amekuwa mgumu kukubali kuwa hakuna mtu aliye juu mawingu I anayemwangalia kila jambo analolifanya na kuna siku atamuhukumu kwenda kuchomwa moto wa milele?

Ndugu zangu, weekend hii tutaenda makanisani...

Je unakwenda kumwabudu Mungu, aliyeshuhsa mana katika ghalika la waizraeli? Ndiye Mungu aliye sambaratisha bahari ya shamu? Au ni tunakwenda kuabudu Mungu aliye bumbwa kwenye taswira ya binadamu wa kale?

Sijasema Dini ni mbaya, wala sijaikataa Dini ila nataka kujua na kuuliza ni kwanini binadamu hufwata kitu kisicho na maana kwa ajiri ya kupata comfort ya muda mfupi?

Lakini pia wanaoikataa Dini mbona hamna mahala mnaposema kuwa hichi mlicho kikuta kimeanzia, na chimbuko la mwanadamu ni hili? Kwa nini Msiwe delusional tu, ilihali mnapendana na kutakaina mema kwa manufaa ya jamii iliyo bora?

Mimi naamini kila kitu ni energy na hata hawa wanaoamini katika Dini si kwamba hawako sahihi, energy is incomprehensible hasa kwa limits zilizo kwenye mlango ya fahamu, so expression ya hiyo energy lazima iwe abstract, ndo maana kuna vitu kama miujiza, which are manifestaion of energy forms.

Swali ni je, Mungu huyo tunayekwenda kanisani kumwabudu ni yupi? Na mbona unaendelea kwenda ilihali hatumjui? (kwa sisi ambao hatujamwona)
Mungu yupo ila sio kama wanadamu wanavyomfikiria.
 
Kwenye Quran, Mungu amesema kuwa hamdhulumu mja bali mja hujidhulumu mwenyewe.

Swali lako linalenga kugusa dhana za uadilifu wa Mwenyezi Mungu (Al-Adl), uhuru wa kuchagua (Free Will), na jinsi binadamu anavyohukumiwa katika Uislamu.

Kijuujuu, inaweza kuonekana kama mtoto wa Kiislamu amependelewa. Hata hivyo, vyanzo vya Kiislamu (Qur'ani na Hadithi) vinaonyesha kuwa nafasi na fursa za kupata radhi za Mungu ziko sawa na kwa usawa kabisa, kwani kila mtu anahukumiwa kulingana na mazingira na kiwango cha maarifa alichopewa.

Kuna misingi minne inayofafanua usawa huo ila sitaki andiko liwe refu, nitakupa misingi miwili ya uadilifu wa Mungu katika jambo hili

1. Kila Mtoto Anazaliwa Katika "Fitrah" (Maumbile Safi ya Kiislamu)

Katika Uislamu, hakuna mtoto anayezaliwa akiwa Mkristo, Myahudi, au Mpagani. Kila mtoto anazaliwa akiwa na mwelekeo wa asili wa kumtambua Mungu mmoja (Fitrah). Mazingira na wazazi ndio wanaombadilisha baada ya kuzaliwa.

Kutoka kwenye Hadithi:

Mtume Muhammad (S.A.W) alisema:
"Kila mtoto anazaliwa katika maumbile safi (Fitrah), kisha wazazi wake humfanya kuwa Myahudi, au Mkristo, au Majusi (Mwabudu moto)..." — (Sahih al-Bukhari)

Hii ina maana kwamba machoni pa Mungu, watoto wote huanza mstari mmoja wa mwanzo wakiwa wasafi na sawa kabisa.

2. Kanuni ya "Hukumu Kulingana na Viwango vya Mtihani"

Mwenyezi Mungu habadilishi kanuni ya mtihani; anatoa mitihani tofauti lakini kwa uadilifu ule ule. Mtu aliyezaliwa kwenye mazingira ya Kiislamu ana mtihani tofauti na yule aliyezaliwa kwenye mazingira ya Kikristo:

• Mtihani wa Mtoto wa Kikristo: Mtihani wake ni "Kutafuta Ukweli" (The Test of Seeking Truth). Ikiwa atatumia akili yake vizuri, akahoji, na kutafuta ukweli kwa nia safi, Mungu humwongoza. Katika Uislamu, mtu anayetoka kwenye dini nyingine akasilimu hupata thawabu mara mbili (kwa mujibu wa Hadithi katika Sahih al-Bukhari), kwa sababu ya juhudi kubwa aliyofanya kupenya vikwazo vya kifamilia na kijamii.

• Mtihani wa Mtoto wa Kiislamu: Mtihani wake ni "Kulinda na Kutenda" (The Test of Preservation and Action).

Kuzaliwa Mwislamu hakukuhakikishii kwenda Peponi. Mara nyingi, watu wanaozaliwa kwenye Uislamu huchukulia dini kama mazoea (cultural Muslims). Mtihani wao ni mkubwa zaidi kwa sababu tayari wanajua sheria lakini wasipozifuata, au wakifanya madambi kama unafiki, adhabu yao inaweza kuwa kali zaidi kwa sababu walikuwa na elimu lakini hawakuifanyia kazi.
HAyo unayoyasema wewe unaona yanatekelezeka mpaka mwaka huu wa 2026, yametekelezeka kwa kiwango gani
 
Katika moja ya miujiza ya Mungu na huwa inanistaajabisha na kunifanya nicheke kila siku ni pale ninapoona Mungu ameumba viumbe ambao wanamkana!!

Hakika huu ni muujiza mkubwa sana.

Quran 10:45

" Na Siku (ya kiyama), (MUNGU) atakapo wakusanya, itakuwa kama kwamba hawakukaa ila saa moja tu ya mchana! Watatambuana. Hakika wamepata hasara walio kanusha kukutana na Mwenyezi Mungu, wala hawakuwa wenye kuongoka.
Mashairi mazuri
 
There is no first event, no start, and no uncaused beginning
Doesn't that prove kuwa Mungu ni alpha na omega...

Kama ilivyo energy isiyo weza kutengeneza wala kuvunja bali hubadilisha form moja kwenda nyingine?
 
Wanabodi...

Poleni na majukumu ya week nzima, as we are welcoming another beautiful weekend.

Naomba tuongelee hili swala kidogo, tumeaminishwa kuhusu uwepo wa Mungu na miujiza yake ya kuponya viwete, kutenganisha bahari na hata kurudisha uhai kwa wafu.

Je Mungu huyo yupo?

Maana nimefika point sasa najiuliza sana, ya kuwa what if dini ni utapeli wa kihisia na imani kwa kitu ambacho hakipo?

What if miujiza tunavyo ambiwa kuwa ukiomba utapata ni kama dhana ya kutuweka tuendelee kuwa watumwa wa shida unazo zipitia?

Maana mimi nilisoma shule za kikatoliki na tukikuwa tunasali sana rosali kila siku, japo ilikuwa na msaada katika masomo na kutupa imani iliyo thabiti, ila bado watoto walikuwa na tabia mbaya sana,

Nakumbuka enzi hizo kulikuwa na Visungura, zile pombe za pakti. Vijana walikuwa wanavusha na kunywa, watu walikuwa wana ruka ukuta, na ikifika rosali wanasali na kutubu...

Ila pia hata kwenye maisha, watu wanahudhuria makanisani, ila bado wanazini na wake za watu,

Watu wanakesha makanisani ila bado wanafanya dhambi na kwenda tena kuomba Mungu awasamehe, je ndugu zangu dhambi ni kitu kibaya?

Mapadri wenyewe tu pia wanalala na kuzaa na wanawake kisiri

Sijawahi kuona mbwa anahukumiwa kwenda kuimba nyama jikoni, atapigwa na atajifunza kumbe kuchukua nyama ni kosa! sijawahi kuona dhambi ikiwa applied kwa kiumbe kingine ila binadamu tu.

Unakaa unajiuliza ni kwanini binadamu tunawekewa hukumu katika vitu na desire za kimwili ambazo muda mwingine ni haja za kinyama kabisa?

Je dini ni illusion? Na kama ni kweli kwanini binadamu amekuwa mgumu kukubali kuwa hakuna mtu aliye juu mawingu I anayemwangalia kila jambo analolifanya na kuna siku atamuhukumu kwenda kuchomwa moto wa milele?

Ndugu zangu, weekend hii tutaenda makanisani...

Je unakwenda kumwabudu Mungu, aliyeshuhsa mana katika ghalika la waizraeli? Ndiye Mungu aliye sambaratisha bahari ya shamu? Au ni tunakwenda kuabudu Mungu aliye bumbwa kwenye taswira ya binadamu wa kale?

Sijasema Dini ni mbaya, wala sijaikataa Dini ila nataka kujua na kuuliza ni kwanini binadamu hufwata kitu kisicho na maana kwa ajiri ya kupata comfort ya muda mfupi?

Lakini pia wanaoikataa Dini mbona hamna mahala mnaposema kuwa hichi mlicho kikuta kimeanzia, na chimbuko la mwanadamu ni hili? Kwa nini Msiwe delusional tu, ilihali mnapendana na kutakaina mema kwa manufaa ya jamii iliyo bora?

Mimi naamini kila kitu ni energy na hata hawa wanaoamini katika Dini si kwamba hawako sahihi, energy is incomprehensible hasa kwa limits zilizo kwenye mlango ya fahamu, so expression ya hiyo energy lazima iwe abstract, ndo maana kuna vitu kama miujiza, which are manifestaion of energy forms.

Swali ni je, Mungu huyo tunayekwenda kanisani kumwabudu ni yupi? Na mbona unaendelea kwenda ilihali hatumjui? (kwa sisi ambao hatujamwona)
Maisha yako tangu kuzaliwa hadi sasa ni muujiza mkubwa kuliko hiyo unayoitafuta.

Mshukuru na Kumtukuza Mungu kwa kkila hatua ya maisha yako. Wengine wameishia njiani na wengine ghafla mno wakiwa wanatembea.

Be Thankful to Thee
 
Back
Top Bottom