Maisha ya dunia ni Mtihani wa imani.
Mungu ametuleta hapa duniani kutujaribu imani zetu juu yake na si kwamba alikuwa hajui nafsi zetu toka hapo mwanzo kuwa nini zitakuja kufanya hapa ulimwenguni. La hasha anajua ya nyuma na mbele yetu ila kuna hekima alitaka kuifanya. Nayo ni
*Kudhihirisha Ushahidi Dhidi ya Mwanadamu (Uadilifu wa Kiungu).
Mwenyezi Mungu anajua tangu mwanzo nani atafanya wema na nani atafanya uovu kwa sababu Yeye ana ujuzi wa mambo yaliyopita, yaliyopo, na yajayo (Ilm al-Ghaib). Hata hivyo, humpa mwanadamu uhuru wa kuchagua na kufanya vitendo hivyo ili:
• Ushahidi uwepo: Siku ya Kiyama, mtu asihukumiwe kwa kile ambacho Mungu alikuwa anajua angekifanya, bali ahukumiwe kwa kile alichokifanya yeye mwenyewe kwa mikono yake.
. Kama Mungu angewapeleka watu motoni au peponi kabla hawajaja duniani kwa kisingizio cha "Najua mgefanya hivi," wanadamu wangepinga wakisema: "Mbona hukutupa nafasi ya kujaribu? Tungefanya wema!" Dunia ni uwanja wa kudhihirisha vitendo hivyo ili mtu asione ameonewa.
Na jambo la kusema kuwa Mungu katuleta duniani ili atujaribu aone nani mwenye vitendo vyema haimaanishi kuwa Mungu alikuwa hajui nini tutakuja kukifanya hapa duniani.
Msingi hapa si kwamba Mungu anajifunza kitu kipya ambacho alikuwa hakijui. Badala yake, maana yake ni: "Ili kukuwekeni katika hali ambayo sifa zenu halisi (za wema au ubaya) zidhihirike wazi machoni penu na machoni pa viumbe wengine."
• Ni sawa na mwalimu anayejua darasani kwake nani ni mwanafunzi hodari na nani ni mvivu. Lakini mwalimu hawezi kutoa maksi au kufelisha mtu bila kutoa mtihani wa karatasi. Mtihani huo unalenga kudhihirisha ukweli wa uwezo wa mwanafunzi kwa vitendo.