Ni huku kwenye maNCHI ya MAJITU MYEUSI tu mbona kwenye Nchi za watu wenye akili Rais akizingua anatupwa Lupango
 
Kumbe sheria ya Sasa haimpi Rais mamlaka tawi maalumu!!! Sasa inakuwaje baadhi ya viongozi waliopita wanaotuhumiwa kutumia tawi hili maalumu kwa mambo yanayoonekana siyo?
Kuna inavyotakiwa kuwa na ilivyo!
 
Labda kwa kuwa ni Muswada itategemeana na akili za wabunge zikoje! Huenda wasiupitishe au wakataka ufanyiwe marekebisho zaidi kabla ya kuupitisha.

Ingawa kwa bunge letu ambalo asilimia kubwa ya wabunge hawakuchaguliwa kwenye sanduku la kura,tegemea mswada utapita bila kupingwa.
 
mm sitakuwa msemaji katika hili , kheri nikae kando. Ila hizi ni dalili mbaya Sana . msoga anahusika asilimia %.huyu jamaa sijui ana nia gani . muamuzi wa ugomvi ataingilia Kati Sasa hivi .
 
Ww ni muumini wa sheria za kulinda viongozi wanaokaa madarakani kwa shuruti. Hivyo hakuna la kushangaza hapo. Ila machafuko pekee ndio yataondoa hizi sheria za kulinda watawala ili wafanye watakavyo.
kwa sheria hii hata humu jf tunaenda kufungwa midomo yetu na huenda baadhi yetu wanaenda kupotezwa kusikojulikana.tuungane pamoja 2025 kuwafuta wabunge wote wa kijanai kabla ya hayo kutokea.
 
kwa sheria hii hata humu jf tunaenda kufungwa midomo yetu na huenda baadhi yetu wanaenda kupotezwa kusikojulikana.tuungane pamoja 2025 kuwafuta wabunge wote wa kijanai kabla ya hayo kutokea.

Mkuu utawafutaje wabunge wa CCM, wakati hao hao usalama ndio wanasimamia wao kuingia bungeni?
 
Kama kuna watu wanapewa Uhuru wa kujieleza halafu wanautumia vibaya kutukana viongozi hata wakuu wa Nchi kwa kigezo ni wapinzani hii sheria itaenda kuwadhibiti ipite tu kwa nguvu zote ili tuheshimiane
Wa mpito anapojizungushia ulinzi.

Bado wawili.

Tusubiri.
 
Sheria nzuri ni KATIBA mpya.

Raisimu ya Warioba irudi mezani tufanye marekebisho kidogo, tuchague wajumbe wa Bunge la Katiba,

Hatimaye tupate KATIBA mpya.

Hayo yanayoendelea ni maigizo na HOFU ya Watawala.

Kama mnadhani mnaweza watishia maiti mortuary kifo endeleeni.

Mungu ibariki TANZANIA.

Amen.
 
kwa sheria hii hata humu jf tunaenda kufungwa midomo yetu na huenda baadhi yetu wanaenda kupotezwa kusikojulikana.tuungane pamoja 2025 kuwafuta wabunge wote wa kijanai kabla ya hayo kutokea.
Usiogope.

Uhai ni hazina iliyo mikononi mwa Mungu.

Hata hao wanaojaribu kututisha, hawana HAKIKA juu ya kesho Yao walalapo usiku.
 
Hii nchi inakuwa ya kipumbavu kabisa. Eeh Mungu tusaidie. Tuondolee wale wote ambao ni kikwazo cha ustawi wa Taifa letu Tanzania
 
Mdude Shida yako iko wapi ? Si mpo kwenye maridhiano na Serikali??? Au hii serikali sikivu imeanza kuwateka tena kama ile serikali ya ki dikteta?? Mh. Freeman Aikael Mbowe alisema msimseme vibaya mama. Tulieni tu mambo mazuri yanakuja
Punguza upumbavu watu wanapojadili mambo ya kitaifa kwa faida ya vizazi...au wewe Mbowe akisema ndiyo kasemekia kila mtu?
 
Mama anawalinda wenzake wa zamani.

Kina bashite wameanza kulindwa kifaulo faulo kabla ya hiyo sheria.

Sasa ndiyo tutegemee vimungu watu.

Sheria mbaya kabisa hii.
Ana vimelea vya UDIKTETA uchwara.


Sisi Bado tunamshuri asigombee, akalee wajukuu muda wake wa mpito ukiisha 2025.
 
Bashite, Sabayau,kingaiii, ziro nk nk wanajulikana.
Kujulikana kwao na kwenyewe kwa mbinde, au hii ni kufuatia kifo cha jasusi mbobezi ikaonekana hakuwa na kinga....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…