MwanaHalisi: Deni la Taifa lakadiriwa kuongezeka na kufikia Trilioni 104

MwanaHalisi: Deni la Taifa lakadiriwa kuongezeka na kufikia Trilioni 104

Lakadiriwa kufikia takribani Trilioni 104

Ni ongezeko la zaidi ya bilioni 600 kwa mwezi

Kila Mtanzania anadaiwa karibu milioni 1.7


View attachment 2779419
Wala hakuna shida,deni linaliowa hata lingefika Trilioni 900 kinaendelea kulipwa.

Cha muhimu hakuna mtu atakukopesha kama huna uwezo wa kulipa.

Mwisho Deni lenyewe ukilinganisha na GDP ratio hata 50% Bado ilhali Ukomo ni 75% na Kuna Nchi deni lao ni zaidi ya 100% ya GDP na maisha yanasonga.Deni la Nchi sio sawa na deni la mtu au taasisi
 
Sisi ni matajiri, Jiwe 2020 [emoji16]
Mbona kaenda kimasikini sana, serikali zingine mwaliko wa Kiataifa inakwenda cabinet yote.

Ndege 10 mpaka 20 na zaidi. Mpaka magari ya Raisa huwa yanaenda kwa ndege. Tanzania kwenda mawaziri 9 mnalalamika, badilikeni, hii nchi haitafunguka mkiwa na mawazo ya kimasikini.

Think big to be big.
 
Vipo vyanzo vya kutosha kuiingizia hii nchi pesa za kutosha, kabla hata ya kuzungumzia uvujifu wa mapato kwa kuondoa matumizi yasiyo ya lazima. Kinachohitajika ni akili tu kama za Wa-Israeli wanaoishi jangwani.
Huwezi kupunguza mikopo wakati bado hauna vyanzo vya kutosha vya kuiingizia nchi pesa.

Hii nchi iliwekewa misingi mibovu sana ya kiuchumi toka awamu ya kwanza. Mwinyi Mkapa na Kikwete walijitahidi sana, kila mmoja kivyake kuweka mambo sawa, yakaanza kuelekea kuwa vizuri sana, akaja mwendazake, kafumua fumuwa na kuharibu kila kitu, ndani ya muda mfupi sana.

Sasa japo tunaona mama Samia anajitahidi kuiweka sawa mifumo iliyofumuliwa. Tutegemee mema, lakini kuhusu madeni ni lazima tukitaka tusitake, hatuwezi kuyaepuka kwa sasa.
 
Wala hakuna shida,deni linaliowa hata lingefika Trilioni 900 kinaendelea kulipwa.

Cha muhimu hakuna mtu atakukopesha kama huna uwezo wa kulipa.

Mwisho Deni lenyewe ukilinganisha na GDP ratio hata 50% Bado ilhali Ukomo ni 75% na Kuna Nchi deni lao ni zaidi ya 100% ya GDP na maisha yanasonga.Deni la Nchi sio sawa na deni la mtu au taasisi
Ukumo wa madeni ya kimataifa huwa unaamuliwa na wanasiasa, pia wapo watu wanaweza kukukopesha kwa makusudi kabisa wakijua hutaweza kulipa huo mkopo.
 
Mi sijui mwesho wa haya mambo utakuwaje! Tuna lundo la madeni lkn ukiuliza nini tumefanyie hizo hela huwezi pewa jawabu.
20230917_112351.jpg
 
Mkuu ili tuwe na uelewa wa pamoja ungeweka takwimu ya kila mwaka kutoka 2011 hadi 2023 ukiambatanisha matumizi yake.

Kwa namna ulivyo weka taarifa yako ni rahisi wengi wetu kudhani kuwa deni lote hilo limeongezeka katika awamu ya 6 tu. Jambo ambalo sio sahihi.

Ukianisha mkopo na matumizi yake kwa kila mwaka tutaweza kuonana ni wapi kasi ilianza kujitokeza kwa kulinganisha matumizi yake.

Kwa kufanya hivyo tutaweza kutoa fair judgment!

Imeongezeka kwa shilingi Trilioni 30.
 
Back
Top Bottom