Zemanda
JF-Expert Member
- Jan 10, 2021
- 8,323
- 18,051
Kuna shida halafu kuna tamaa. Ukweli ni kuwa mabinti wengi miaka hii mnamitazamo mufilisi juu ya maisha.mtu mpaka akuombe ujue amebanwa na anaona mtu wa kwanza kumshirikisha ni mpenz wake,, au unataka amwambie nani jamani na wewe upo[emoji4]
Unatoka kwenu haujui lolote kuhusu maisha ya kujitegemea. Sasa unachojua wewe ni kuomba hela ili utumie vile unavyojisikia. Shida zenyewe sasa unataka ununuliwe bundle ya internet, mwanaume anasema ngoja ajitolee kukununulia.
Bundle ya 30+ ya mwezi ili usipate tabu na kutokuwa hewani. Sasa kwa akili ya mtu asiyejitambua kama most of you, utaingia Instagram, TikTok, YouTube, Facebook, siku nzima yaani unakuta umenunuliwa GB 40+ utaziteketeza ndani ya siku tatu tu au wiki. Then unamwambia tena kifurushi kimesha akununulie tena.
Huko mtandaoni kwenye unavyofuatilia ni upumbavu tu wa akina kajala wamefanya nini kwa harmonize, na mara kwa mange.
Kidogo umepita pita mtandaoni umeona video ya mdangaji kavaa nguo fulani au kaweka kucha fulani au kavaa viatu fulani na wewe unatamani unaanza kusumbua unadanganya unashida ya umuhimu upewe pesa ukanunue huo upuuzi wako roho iridhike.
Miezi 6 ya mahusiano hakuna kitu umechangia kwa mwenzako ambacho ni positive kwenye mahusiano yenu na kuwasaidia.
Wakati kuna mdada mwenzako anapambana kuuza hata juice akipata hata 20,000 nakwenda mnunulia mchumba wake hata boxer kuonyesha yupo na yeye, atakwenda kutafuta hata vicoba akope wanunue vitu vya ndani.
Mimi mwanamke akakope anunue vitu vya ndani aiseee nitamlipia hilo deni na nitajitafuta nimpatie hata pesa ya ziada.
Sio unakuja kunifuja mapato yangu hafifu unanirudisha nyuma nguruwe wewe .
Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app