Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kabisa, hata mi namshangaa unapelekaje kanisani haya mambo?Yani ujinga wako binafsi ndio unataka kuamini kila mtu ni mjinga sawa na wewe?
Vyeti vya ndoa vinatoka serikalini, sasa nani anakuzuia kuowa bomani?
Na huyo mwanamke kama humtaki kafile divorce mahakamani na siyo kupeleka mambo yako kanisani.
Hamjanielewa tatizo si talaka maana najua inatoka mahakamani tatizo ni ushirika na kutokutambulika ndoa yangu mpya baadaeMkui huyu hajaamua tu kuacha!
Aliyemwabi kanisa linavunja ndoa nani? Hakuna ambae anaitaka hiyo dhambi wote wanakwepa,ndo maana ndoa zinavunjwa mahakamani sio kanisani!
Na maisha yanaendelea, na unafunga nyingine kanisani vzr ,baadhi ya ma kanisa hawana mambo mengi[emoji23]
Nakufahamisha ndoa sikufunga kwa mjomba ako nilifunga kanisani so hata ukianza mahakamani lazima wakurudishe kanisani kwanzaKabisa, hata mi namshangaa unapelekaje kanisani haya mambo?
Kwani umelazimiswa kuabudu huko? Hamia kwa Nabii Shila au kwa mfalme Zumaridi, au kama vipi achana na ukristo. Uislamu upo na sheria zao za ndoa nzuri sana...wake wa 4, akikuzingua unapiga talaka bila kumshirikisha mtu.Kwenye ndoa wakristo tunateseka saana inabidi waumini tuandamane aseeeh
Ukienda mahakamani utashauriwa uanzie kanisani.Hamjanielewa tatizo si talaka maana najua inatoka mahakamani tatizo ni ushirika na kutokutambulika ndoa yangu mpya baadae
Kwa uzoefu huu ushavunja ngapi dada..?😂Mkui huyu hajaamua tu kuacha!
Aliyemwabi kanisa linavunja ndoa nani? Hakuna ambae anaitaka hiyo dhambi wote wanakwepa,ndo maana ndoa zinavunjwa mahakamani sio kanisani!
Na maisha yanaendelea, na unafunga nyingine kanisani vzr ,baadhi ya ma kanisa hawana mambo mengi[emoji23]
Aisee,kumbe bado kuna wanaume?![emoji848][emoji108]nimekupenda! Km ana akili afuate huu ushauri!Let's be real!!!
PART 1: UHALISIA WAKO MTOA MADA.
Mkuu una shida paala!
"nilimfukuza nyumbani baada ya kushawishiwa na ndugu zangu"
Inakuaje mahusiano yako unaruhusu watu wa nje ndiyo wakushawishi kufanya maamuzi??
Wewe kama mwanaume kichwa cha familia na mtu mzima mwenye akili timamu, pamoja na kuelewa hali halisi ya Mkeo, hujui nini Ufanye mpaka ndugu zako ndiyo wakushinikize kufanya maamuzi ??
Anaeishi na mwanamke ni nani? Kanisa, Ndugu zako au wewe?
Anayepitia magumu kutokana na tabia za Mkeo ni nani? Wewe, Kanisa au ndugu zako?
Mwanamke anatoka nje ya ndoa mpaka ushaidi unao, bado huelewi nini ufanye kutatua tatizo??
Kuna kitu hakipo Sawa....
Njoo part 2.
PART 2: IMANI YAKO KATIKA DINI.
Hapa napo una shida boss.
Unapeleka matatizo yako kanisani ili yatatuliwe ili hali mwenyewe unakiri kuchepuka kwasababu ya UPWEKE.
Mkeo awe chanzo cha wewe kuishi maisha hayo halafu matatizo hayo badala ukae uone nini cha kufanya, unayabeba na kupeleka kanisani kisa kufuata taratibu za Kanisa ili hali UNAVUNJA SHERIA ZA MUNGU kwa kufanya uzinzi, huoni kuna sehemu haupo Sawa??
Halafu inakuaje unaruhusu kushikiwa akili na Dini. (Binafsi ni mkristo pia na ninaye amini katika Mungu, hivyo siongei haya kwasababu ni mpagani, HAPANA).
Kila kitu na kiwe na KIASI katika maisha, Mungu ana sehemu yake ya kufanya na wewe pia una sehemu yako ya kufanya. Inapofikia hatua kuruhusu KILA KITU maamuzi yafanywe na Kanisa ili hali wewe ndiye unayeona na kuelewa undani wa tatizo, hii inaonyesha dhahiri unakabidhi nafasi yako kama mwanaume upande wa pili.
JAMANI MAMBO KAMA HAYA NI MFANO HALISI WA KWANINI ASILIMIA KUBWA YA WAKRISTO WANAISHI MAISHA YA SHIDA NA WENGI HUWA HAWAFANIKIWI KATIKA MAISHA.
Dini kuruhusu Itawale maisha yako kila ENEO pasipo kushirikisha upeo binafsi ni UTUMWA.
Ulishawahi kushirikisha kanisa kuhusu KUCHEPUKA KWASABABU YA UPWEKE??
Nina Imani hilo bado hujalifanya.
Nina mengi ya kuandika, ila Kiufupi ZINDUKA!! Maisha yako yasimamie WEWE na uwe na utashi wa kufanya maamuzi wewe mwenyewe na lile linaloshindikana kabisa Shirikisha watu ukiwa tayari una maamuzi yako binafsi bila kujali washauri watasema nini.
Sasa angalia kwasasa unataka kulazimishwa kusamehe ilihali mwenyewe unakiri nafsi yako inagoma, ila kwa vile ni DINI inataka hivyo unajilazimisha iwe hivyo.
Haya, baada ya kufuata ushauri wa kidini wa KUSAMEHE ili hali wewe bado una kinyongo moyoni, humo ndani mtaishi kwa AMANI au ni mwendo wa KUWA MNAFKI KWA MWENZIO, kuonyesha yameisha ilihali bado una machungu moyoni??
Na kwa hali hiyo unadhani UTAACHA kuchepuka zaidi kuitafuta furaha uko nje??
Maisha wengi huwa wana fake kwasababu ya kuogopa JAMII ITANIONAJE, ili hali magumu unapitia wewe, shida ni zako, na jamii inakutazama ukiteseka, halafu bado unaionea HAYA katika kufanya maamuzi!! Hii kitu naiona kwa wengi sana, hasa kwa hawa watu wanaojifanya kuamini Katika Dini.
Aisee maisha ni mafupi sana kuruhusu kila ushauri wa mtu kuendesha maisha yako.
FANYA VILE MOYO WAKO UNAPENDA, ACHANA NA MENGINE.
Be a man Bro!
Usipoteze muda,nenda mahakamani malizana na hii habariAhsante nitajitahidi kuwaelewesha kwa hili pia
Jmn kumsamehe mtu ni lazima(kabisa Mungu kaagiza na ni nzuri kwa afya yako pia),ila haimaanishi kuwa ukimsamehe lazima urudiane nae,hapana!Kuna mahali umeni quote vibaya... Kuhusu Mimi kumfukuza sababu ya ndugu... Ni yeye alipohojiwa akasingizia huyo sababu wakati in ya uongo.
Kuhusu kushirikisha dini Mimi ni muumini wa mda mrefu pia nilishawahi kua kiongozi wakati Fulani, zaidi ndoa tulifunga kanisani ivo kufuata taratibu za kanisa sioni tatizo kwakua ndivo nnavyo amino.
Kuhusu maamuzi yangu najua kabisa simtaki na ndio msimamo wangu na vielelezo nnavyo tatizo linakuja sikutegemea kama ntalazimishwa kiasi cha kutishiwa ili nirudiane nae kwa kigezo cha msamaha.
Kuhusu kuzini ni dhambi kama zilivyozingine ila kipindi hichi inanigharimu zaidi kwa sababu ya upweke na stress na ndo mana nataka nimalizane nae ilinipate fursa ya kuoa muda ujao
Uhalali kikanisa sio rahisi!Ndugu najua mahakama ndio inayotoa talaka ila nilichokua nataka ni kupata uhalali kikanisa ili niweze kufunga ndoa tena kanisani hapo baadae.... Ila last option utakua hiyo
[emoji848][emoji848]heeee makubwa !Ni kweli kabisa coz huyu mwanamke anafanya Yale mama yake amemfanyia baba yake na wametengana mpaka sasa pamoja uzee wake bado anatafuta mabwana
[emoji23][emoji23][emoji23]sawa baba jSister nna namba D Nazi saana sema nn mambo ya talaka ndo yananirudisha kumzungumzia mama jay.... Ukicheki tuu apo church namba D zinaningoja kinoma zishaweka hadi booking kabisa
Hama kanisa oa,maisha yanaendeleaNdo utaratibu wa kanisa naweza ndoa kuivunja ila kanisa halitoshiriki swala langu lolote baadae kama nitaoa nje na kanisa
Unaposema imani unamaanisha nn?Tatizo ni imani uliyoizoea ila nimeamua ntasali hapo hapo kibishi hata wakinitenga
Aah ndo maana unateseka!Adventist
Kazi anayoHapo nakuelewa...
Shida ni km huyo binti anataka kuolewa hapohapo kanisani kwenu,ila km yupo tayari kufunga ndoa kanisa lingine mbona haina shidaMkuu bado talaka ndo inazingua na mi nataka kumuoa binti mwenye imani ya kiroho kweli kweli sa nawaza bomani hatokubali mpaka ni clear ili swala ambalo church inaniwekea usiku
Dear huyu ni msabato sio Rc!Church hawakuwekei usiku ni wewe hujaamua. Ondoka hapo church nenda ngazi ya juu yake...ukifika huko utarudishwa kanisani kwako na itakuwa rahisi. Ila jiandae inaweza chukua hata 4 yrs kumaliza hiyo process.