Hizo mbio za mwenge kwa kipindi hiki tulichonacho je vijana wanajua umuhimu wake.

zaidi ya kusambaza UKIMWI kwa kasi ya moto wa petroli kwenye mikesha na kutujazia watoto wasio na wenyewe , hakuna kingine .
 
bajeti ya kulizungusha lile kopo lisilo na macho nchi nzima inatisha na ni ubadhirifu wa kishamba sana .
 

Baada ya kusoma haya yaliyosemwa na Naibu waziri wa habari Juma Nkamia leo May 27 2014 bungeni, unalolote la kuchangia?

Mtazamo wako kwa ujumla uweke hapa.
 
This is very serious , na bado zile za wakuu wa mikoa na wilaya wanazochangisha wafanya biashara , huwa Msimu wa mwenge ndio wakuu wa mikoa na wilaya wanaanza ama kukamilisha ujenzi wa nyumba zao ..."......
 
hii nchi ya ajabu sana gharama zote za kazi gani sasa, unatumia mabilioni kuzindua miradi ya mamilioni halafu tunalalamika nchi haina fedha! hii ni sawa na kuuza ng'ombe kwa kesi ya kuku.
 
sasa hizo pesa siwangeongeza vitanda pale MOI?
 
Kila nchi inautamaduni wake jamani mbona tunapinga kila kitu

Uk wanatumia billions kwa asjili tu ya ufalme ambao upo upo tu

all over the world kila nchi inatunu zake
 
Ningefurahi kama Naibu Waziri angeweka na thamani ya miradi iliyokamilika kabla ya kuanzisha/kuzindua mbio nyingine za Mwenge kwenye mwaka uliofuatia, ili kucheki value for money.
 
Kila nchi inautamaduni wake jamani mbona tunapinga kila kitu

Uk wanatumia billions kwa asjili tu ya ufalme ambao upo upo tu

all over the world kila nchi inatunu zake
kwa hiyo tuendelee na utamaduni usio na tija mbona azimio la arusha walilifuta !!!!! ukifananisha utamaduni huu na wa waingereza kuutukuza ufalme si sahihi wao wameendelea sisi tunamatatizo kila mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake.
 
Huu ni ufisadi wa hali ya juu, mwenge unafungua miradi hewa, wanasema unamulika maovu na kuleta matumaini, ile hali ufisadi unazidi kuongezeka tena saizi wanafanya mchana kweupe, sioni faida ya mwenge, tuache kuishi kwa mazoea, hospitali hazina madawa, miundo mbinu mibovu vijini ndio usiseme, maambukizi ya ukimwi yanazidi kuongezeka kutokana na mikesha ya mwenge, wanajua kinachofanyika ndio maana wanagawa kondom bure kwenye mkesha wa mwenge, sihitaji kusikia habari ya mwene, mabilioni ya fedha hizo huwa zinatumika vipi, tupinge mbio za mwenge kuzuia ufisadi huu mkubwa kwa kisingizio cha mwenge.
 
Licha ya kutafuna pesa zetu kwa mgongo wa huu mwenge hivi serikali haifahamu kuwa hizi mbio za mwenge huchangia kwa asiliamia kubwa maambukizi ya UKIMWI????Vijijini ndio balaa yaani mwenge ukilala hapo kijijini basi inakuwa kama sodoma na gomora!!!Nachukia sana hizi mbio za mwenge na nadhani ni wakati muafaka watanzania tuanze kupiga kelele mbio za mwenge zikome, na hizo pesa zitumike kuboresha huduma za jamii. MIA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…