Mwenge wa Uhuru upo kwa faida ya nani?
Ungefutwa tu jamani. Nimeshangaa kuwa sasa eti kuwasha mpaka watu waende uwanjani jamani gharama za bure hata in terms of time!
 
Siku hizi wanaokwenda kwenye mwenge ni makada wa ccm na watoto wa shule tu.
 
mwenge umulikia mafisadi ili wazidi kututawala...

ungewekwa stoo\makumbusho kwa kumbukumbu
 
hauna tofauti na ile story\mantiki ya kigoda cha dhahabu ambacho watu walikisujudia kabla mfalme hajakalia.
 
Wakuu samahani kwa hili jaman naomba kuuliza hvi Mwenge unafaida gani au unasaidia nn katika nchi yetu wakuu maana ukitua sehem na kukesha basi ujue hapo kila vitu vibaya hufanyika. Mfano ulevi, umalaya, wizi na matukio mengine kibao so naomba kuelimishwa zaidi kuhusu hili.



MIMI NI MTANZANIA HALISI NINAE PENDA NCHI YANGU.

!
!
kwa kuwa mwenge hauvuki kijiji basi fegi isimruke mtu kama mpo wengi.
 
mwenge uongezwe thamani uwe wa dhahabu maana huu wa sasa ni chakavu ndio maana authaminiki.
 
Ngoja ukawa tuchukue nchi huo mwenge tutauweka kando
 
Enzi zetu mwenge ulikuwa unamulika mpaka mipakani,hiyo ni miaka ya kuanzia 65 mpaka miaka ya 70.siku hizi haumuliki kabisa.
 
Zamani mwenge ulikuwa unamurika mipaka, mafisadi, miradi ya maendeleo n.k
Lakini kwa hv sasa unaficha mafisadi na wahujumu uchumi wa nchi.
 
Mwenge hauna hatuna haja yakueendeleza kwasababu kwasasa unatuongezea zambi ukilala sehemu kinacho endelea hapo niumalaya wizi ukabaji nk...kwahiyo hatuhitaji natukichukuwa .nchi ukawa tunaupigamalufuku.. maana siku ukijahuku ofs za wilaya hazifanyi kazi kisa Mwenge
 
Mwenge = torch

1. Unasaidia kumulika wakoloni wasitutawale kabisa Tanganyika

2. Unasaidia kuregulate thamani ya $ ikipanda dhidi ya shillingi.

3. Mwenge unasaidia kupiga kura ya ndio pale kunapokuwa na upinzani saana bungeni
 
Kwa miaka hii ya karibuni mwenge umepoteza uhalisia imekuwa ni sehemu ya watu kupiga pesa( viongozi) na washerekeaji( wananchi) imekuwa ndio sehemu ya kucheza ngoma, kunywa pombe na kufanya ufuska kwa kiwango cha kutisha
 
Back
Top Bottom