Maadam hayo ndio yalikuwa madhumuni ya kuwasha na kukimbiza mwenge nadhani yamefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kwani hadi leo hii tunaishi KiMungu Mungu tu..yaani pale pasipo na matumaini tunapita, misaada inamwagwa...
Upendo pale penye chuki..heshima penye dharau kwani mnaona Mafisadi wote tunakula nao sahani...hakuna chuki bali heshima na upendo..
Tatizo sio mwenge isipokuwa sisi ndio tumepoteza mwelekeo na UHURU kwetu hauna maana tena..Na nafikiri ukimuuliza mtoto wa shule ya sekondari leo hii nini maana ya UHURU utapata majibu mia kidogo kwani maana halisi imekwisha potea..Hakuna tofauti kati ya kutawaliwa au kuwa huru maadam wananchi bado wako mikononi mwa watawala watunzi wa sheria..
Madhumuni ya mwenge wetu ni sawa na mwenge wa Olyimpic ambao mbali na kuashiria kuanza kwa michezo hiyo hutangaza matumaini, upendo, heshima na zamani ilikuwa mwisho wake kama sijakosea zamani mwenge ulikuwa ukihitimishwa na sikukuu ya Wakulima tukiita Sabasaba..Ilikuwa siku kubwa sana Tanzania nzima toka vijijini, wilayani hadi mikoani, pengine ikisherehekewa kuliko hata siku ya Uhuru wenyewe..
Hapo wakulima huonyesha mavuno yao na mashindano mengi ikiwa ni pamoja ngoma za kienyeji, costumes, ukubwa na uzito wa mazao, maonyesho ya mbegu mpya na kadhalika.. maadam siku hiyo ilikuwa furaha tupu kwa wananchi wote Tanzania utafikiri kweli Olympic ya Watanzania..Ni vigumu sana kumwelezea mtu ambaye hakuwepo miaka hiyo ya 60 na 70 kwani haya yote hayapo tena leo...
Tuliobadilika ni sisi sio mwenge na lawama zetu haziwezi kuwa na msingi wowote kwa sababu ya mwenge unaowashwa kwa mafuta ya taa kuwa sababu ya kupoteza fedha..