Mwenge wa Uhuru upo kwa faida ya nani?
Wanakijiji wa wawili wa Kijiji cha Masqaroda Wilayani Hanang, Mkoa wa Manyara wamekamatwa kwa kuhoji matumizi ya michango ya fedha za mwenge.
Mwenge mwaka huu utawashwa Mkoani Manyara


______________________________________
Democracy is the government of the people, by the people, for the people

Abraham Lincoln

Matatizo ya kutokuwa na au kuzingatia rule of law, usipotoa mchango wa mwenge sio kasa la jinai hata kidogo, wanawaonea wananchi hawajui haki zao. Waachiliwe haraka.
 
Nimepata taarifa hivi punde kwa rafiki aliyekuwa kwenye mkesha wa Mwenge wa UHURU uliolala katika kijiji cha Mambali ( kama nimemsikia vizuri) na kuwa Mgombea wa CCM Ndg. Kigwangala na Kikwete walikuwa wana-kampeniwa uchi uchi.

Habari ndiyo hiyo, mwenge wa UHURU unatumiwa kisiasa .....
 
Huko kwenye Mwenge ni NGONO tu.Suji kama serious person anaweza kujihusisha na uchafu huu.
 
Na ndio maana hata siku moja siwezi kuchangia wala kuhudhuria sherehe za mwenge, ule ni uchawi wa .....na ninafananisha na picha ya Nebukadnezer Mfalme wa Bibiloni.
 
Naona kwa kipindi hiki cha kampeni si ungesimamisha shughuli ilo nalo twaitaji tafsiri ya sheria.
Bse to me mwenge uliasisiwa na the late Mwalimu akiwa chairperson wa CHAMA.
Ingawa kuna watu watasema ni nembo ya taifa as it seeks to unite people and foster projects.
NI BUSRA KWA SASA UNGESIMAMISHA MBIO MPAKA OCTOBER
 
Hivi Jamani Kuna Faida Zozote za Kukimbiza Mwenge wa Uhuru? Kila Mwaka Maelfu ya Pesa yanatumika Kukimbiza Mwenge Nchi Nzima. Eti Wanasema kwamba Mwenge unazindua Miradi hivi Kweli bila kuchoma Mafuta ya kukimbiza Mwenge Miradi Haifunguki?
 
Mimi najua moja ya matokeo ya mikesha ya Mwenge ni kuambukizana ukimwi kwa wingi.
 
Ni kwa sababu tumepoteza dira ya Kitaifa. Zamani mwenge ulikuwa na maana sana ktk kutuunganisha sote kama ule wa Olimpiki lakini siku hizi hauna maana tena.
 
Hivi Jamani Kuna Faida Zozote za Kukimbiza Mwenge wa Uhuru? Kila Mwaka Maelfu ya Pesa yanatumika Kukimbiza Mwenge Nchi Nzima. Eti Wanasema kwamba Mwenge unazindua Miradi hivi Kweli bila kuchoma Mafuta ya kukimbiza Mwenge Miradi Haifunguki?

Hamna mkuu hamna. Ni ushirikina tu huo.
Huwezi kuona mwenge unazimwa wala kuona unawashwa kati kati ya safari. Kwa mfano ikitokea ukiwa unasafirishwa njiani ukazima lazima wakajifiche porini tena watu wawili au watatu ili kuuwasha. Ni ushirikina wa aina yake. I wish tungeu abolish. Nadhani ni ushauri tu alianzisha yule mkuu wa kamati yao ya ufundi anaitwa sheik nani sijui.
 
Hamna mkuu hamna. Ni ushirikina tu huo.
Huwezi kuona mwenge unazimwa wala kuona unawashwa kati kati ya safari. Kwa mfano ikitokea ukiwa unasafirishwa njiani ukazima lazima wakajifiche porini tena watu wawili au watatu ili kuuwasha. Ni ushirikina wa aina yake. I wish tungeu abolish. Nadhani ni ushauri tu alianzisha yule mkuu wa kamati yao ya ufundi anaitwa sheik nani sijui.

Hivi kweli?!!!!
 
Malengo ya mwenge yameshachakachuliwa!! mwenge ulikuwa wa kitaifa na siyo wakichama lakini siku hizi uko kichama zaidi.
 
.....kama kudumisha (si kuleta) mshikamano baina ya watanzania, yapo mambo mengi yenye akili ya kufanikisha hilo na si hili dubwana linalotafuna pesa zetu!! pia ukihudhuria mikesha ya mwenge wa uhuru...ni ngono zembe kwenda mbele!!! pia unapotembelea sehemu, ofisi za umma zinalazimishwa kuchangia 'mafuta' ya mwenge. pia umeshapoteza sura ya kitaifa na siku zinavyozidi kwenda mbele unachukua sura ya kichama (CCM-aaaaaaaagggggggggghhhhhhhhh!!!!!!!!!)
 
Nami ni mmoja wa watu ambao tunaona utata kwenye zoezi zima la mwenge. Kama ni lazima uwepo, just because ulianzishwa na fulani, basi ungetafutwa utaratibu mbadala wa uendeshaji wake. Mfano, theme ya mwaka 2010 ni kujenga barabara za eneo fulani, basi hiyo michango ielekezwe huko na lengo la mwaka huo lihitimishwe kwa kufungua barabara hizo. Na mwaka unaofuata labda kujenga wodi mpya muhimbili (kamilifu na vitanda) and the list goes on and on.....Nina uhakika toka ulipowashwa naintinikweusi mpaka leo tungekuwa mbali. Na sio kukimbiza nchi nzima, no....uende kwenye tukio la mwaka huo tu.

Sasa hii bora kukimbizana tu mwanzo mwisho mie naona wala haina tija, sore kwa makamanda mnaotumia nguvu nyingi kuufanya uwe, but...neeeyyy
 
Mwenge kwa sasa ni suluhisho kwa serikali isiyoweza kusimamia utekelezaji wa shughuli zake. Fedha zinatoka serikalini kwa ajili ya miradi na wasimamizi wake wamewekwa na serikali...sasa kwa kuwa wanafahamu kuwa fedha nyingi zinaishia mifukono mwa wasimamizi hao inabidi waweke mwenge ili BAADHI ya miradi hiyo iwe imekamilishwa. Hawatambui jinsi mwenge unavyoconsume fedha na muda mwingi wa watendaji na wananchi....Naamini ukiwa na serikali madhubuti yenye vyombo madhubuti vya kusimamia matumizi ya fedha za umma hutahitaji mwenge.
 
huku ni kuibiana tu...wanatumia mamilioni ya fedha za wananchi pasipo sababu ya msingi...bora huo mwenge uwekwe jumba la makumbusho tu!!
 
Mwenge ni mzuri saana tatizo usanii mwingi
 
Mwenge ni mzuri saana tatizo usanii mwingi
Mwalimu Nyerere alianzisha wazo la Mwenge kwa nia njema. Lakini sasa kimekuwa chombo cha kifisadi. Huko vijijini wakisikia mbio za mwenge hawalali. Maana ni msimu wa Watendaji kuwakamua pesa. Huna pesa hata mbuzi, kuku, mazao yako vinachukuliwa. Hizo pesa wanazoita za mafuta ya mwenge sijui huwa yanaingia kwenye hesabu ipi? Kama ni mbio za Serikali kwa nini isigharamie? Miradi inayozinduliwa na mwenge mara nyingi ni miradi iliyo kwenye budget ya Serikali au nu miradi ya ubabaishaji inayokoma mara mwenge ukiishapita. Hakuna anayefanya tathmini ya ufanisi wake baada ya hapo. Ni wizi mtupu.
 
Mimi nikiusikia huwa naenda mbali nao kabisa. Ndugu yangu moja miaka ya nyuma alipigwa sana kwa kiherehere cha kugombania kuubeba.
 
Waulize TACAIDS wanazielewa vizuri sana faida za mwenge...semina,mikutano na warsha vinaongezeka sambamba na virusi vya UKIMWI..
 
Back
Top Bottom