Mwenge wa Uhuru upo kwa faida ya nani?
Historia ya Mwenge ni nzuri, mimi ni mmoja wa wanoamini hili. Kwamba uendelee kukimbizwa- hapana.. kwa nini

Sisi tumekwisha kuwasha Mwenge
Na kuuweka Juu ya Mlima Kilimanjaro
umulike hata nje ya mipaka yetu,
ulete tumaini pale ambapo hakuna matumaini,
upendo mahali palipo na chuki na
heshima palipojaa dharau!..?



Kwa hali tuliyo nayo kama nchi hakuna matumaini ya Mwenge kutusaidia
kuleta tumaini pale ambapo hakuna matumaini,
upendo mahali palipo na chuki na
heshima palipojaa dharau!


Ukitaka kujua hili Muulize Shigongo, atakuambia ilivymuwia ngumu alipojaribu kufanya kongamano ya kujenga utaifa kule Manzese…

Ni vema tukubali kuwa hapa tulipo panahitaji kama ni ndumba basi ni ya tofauti mazingira yamebadilika sana kiasi kuukimbiza Mwenge na kuamini utaleta matumaini kwa jamii ya leo tunajidanganya…labda tuseme tunaigiza kama tunavyofanya katika maeneo mengi.

Mwezi wa May mwaka huu nilikuwa katika mkutano mmoja wa wazito fulani ambao huwa wanashiriki sana katika kuhakikisha Mbio za Mwenge zimefainikiwa kila mwaka.. walipotangaziwa kuwa mwaka huu Mwenge utapunguziwa mzunguko wake …walipiga makofi sana mimi nikajiuliza nini maana yake? Na, je siku watakapotangaziwa kuwa hautakimbizwa kabisa si watashangilia zaidi?

Ukweli ni kuwa Watanzania wachache ukiacha wale wanafaidika na fedha zinazochangwa ambao watajali ukisimamishwa…. Ila kama kawaida yetu tunaogopa kusema “Jamani eeh hili hatuafiki…”

Mimi ukiniuliza nitasema tuupumzishe makubusho(Uandikiwe historia nzuri unayostahili) kwanza twende na mikakati practical zaidi ya kurudisha utaifa, upendo na mshikamano huenda baadaye tukapata njia nzuri ziadi za kuutumia kama ni lazima tuache maigizo – let’s be practical.

Mbona mengi tumeyapumzisha ikiwepo Maandamano ya MSHIKAMANO – July 1[SUP]st[/SUP]..

TANZANIA TANZANIA NAKUPENDA KWA MOYO…

:lock1:
 
Leo kwa mara nyingine mbio za mwenge zimeanza tena Tanzania, na safari hii mwenge umewashwa huko Dole Zanzibar kuendeleza ile adhma ya taifa letu changa kuwa "sisi tumekwisha kuwasha mwenge na kuuweka Kilimanjaro". Mwenge huu ulipowashwa mara ya kwanza na kuwekwa kwenye kilele cha Kilimanjaro na Nyirenda, ulikuwa uwe ishara ya matumaini, upendo, na umoja wa Taifa letu.

Matukio ya hivi karibuni hasa baada ya muasisi wa mwenge huo kufa, kuna kila dalili kuwa tunachokimbiza sasa hivi ni kivuli tu cha mwenge ule kwani miale ile ya mwanzo ya mwenge wetu wa uhuru imeanza kuzimika na inaonekana ikififia kila mwaka mpya ujapo. Mwenge huu sasa umekuwa ni alama ya watu wachache kujiangazia wao na familia zao huku sisi wengine tukiendelea kubakia gizani. Hakuna kitu kinachoonesha kufifia kwa mwenge huo kama suala la mikataba ya nishati, madini, ununuzi wa rada, ndege ya rais, n.k Zaidi ya yote kwa wanafunzi waliokwama Ukraine, mwenge huu kwao tayari umezimika ( a little strech there, but why not try..??)

Je kuna matumaini ya kurejesha nuru yake tena? Je kuna haja ya kuuwasha tena ili uendelee "kuwamulika" wabadhirifu, wazembe maofisini, wala rushwa magendo n.k ? Au tuamue kuuzima tu, ili kila mtu ajiwashie mshumaa wake yeye mwenye na wale wenye uwezo wawashe vibatari, chemli, na taa za umeme! ?

huu mwenge kweli tunasababu ya kuendelea kuukimbiza?

Ni maandamano tu kama yale ya CDM, Nyani Haoni.:crazy:
 
Wakuu,

Kati ya TUNU za taifa hili ilikuwa ni mwenge wa uhuru, Mwenge wa Uhuru ulimawakati wa kukimbiza mwenge huu kila mtanzania alijitahidi kwa kadri ya uwezo wake kuuona na hata kuushika ingawa ilikuwa na ulinzi mkubwa sana.

Nitawakumbusha maneno katika wimbo huu - utajua kweli waasisi wa taifa hili walijitoa wenyewe kwa faida ya wananachi wa wakati huo na vizazi vijavyo. Kwa sasa kilichobaki ni wizi wa waziwazi, hakuna huruma, hakuna uzalendo kila mtu kivyake vyake as if hatuna viongozi wa juu wa taifa hili linaloteketea.

KUWASHA MWENGE WA UHURU:
Kuwasha mwenge na kuuweka juu ya mlima Kilimanjaro;
Umulike hata nje ya mipaka yetu ulete TUMAINI;
Pale ambapo hapana matumaini, upendo mahala ambapo pana chuki na HESHIMA ambapo pamejaa dharau.

-----------------------------------------------------------

Tazama Ramani utaona nchi nzuri,
Nenye mito mingi na mabonde ya rutuba
Nasema kwa kinywa harafu kwa kufikiri
Nchi hii mashuhuri inaitwa Tanzania

Majira yetu haya yangekuwaje sasa
Utumwa wa nchi Nyerere ameukomesha.

--------------------------------------------

Hizi ndizo baadhi ya nyimbo ambazo ni tunu ya taifa hili, watu waiimba nyimbo za ushindi, nyimbo za uhamasishana upendo na mshikamano, watu walikuwa tayari hata kufa kutetea nchi yao, mali asili na utaifa wao. Sasa hivi mtu anaiba mali za umma then anarudi mitaani anatamba na hakuna mtu yeyote wa kuthubutu kumgusa.

Kuelekea miaka 50 ya Uhuru binafsi naona kama tumepoteza dira as na Nation, lazima turudisha tunu hizi - SOLIDALITY FOREVER.
 
Leo nimeskia kwenye taarifa ya habari R.f.a kuwa Dr. Gharib Bilal atakuwa mgen rasmi wakati wa uwashwaji wa mwenge huko Butiama tarehe 14 october..nikajiuliza kuna umuhimu wowote kwa wakati huu kuwasha mwenge kila mwaka na kutumia pesa nyingi za wavuja jasho wa Tz?..au ni mimi ambaye nipo kwenye hii era ya dot com. Nawasilisha
 
Hilo likibatari ni mradi wa wakubwa.vilevile unachangia kueneza ngoma na mizindiko ya CCM.
 
tatizo wakilipitisha na sisi tunalifuta, wataachaje kamatunalifurahia?
 
Naomba nijue faida za kukimbiza huo mwenge nchi nzima
 
ni kufuja resource za serikali tu hakuna jipya,haya pia karibu jamvini
 
Siku nyingine kupata jibu stahili toa kwanza mawazo yako kuhusiana na hilo unalowakilisha...
 
tar 14.10.2011 ni siku ya kukumbuka kifo cha shujaa wa africa na rais mwadilifu zaidi africa. Kumbukumbu za mwaka huu zinaenda na sherehe za miaka hamsini ya uhuru wa tanzania, watanzania swali je mwenge unamchango kwenye maendeleo ya nchi au? Je speed yetu ya maendeleo tangu uhuru ikoje ni rais gani anaweza akawa dira kati ya walitangulia, je nchi za wezetu wamefanyanini wakafikia pale walipo?









 
Leo nilipokuwa katika eneo langu la kazi niliweza kushuhudia msafara wa mwenge ukiwa na magari mengi ya kifahari na ulinzi wa hali ya juu ,wakati nilipotoka kazini nikakuta mahali ambapo mwenge umefikia na inasemekana utalala hapo na eneo hilo limepambwa na burudani za kutosha, nikabaki najiuliza kuna umuhmu gani wa kutumia gharama kubwa kutembeza mwenge na je watanzania tunafaidika vipi na huu mwenge? Tafadhali naombeni mnisaidie kujua..naomba kuwasilisha
 
Back
Top Bottom