Leo Asubuhi nimesikia Kiongozi wa Mbio za Mwenge Mwaka 2006 na ambae pia alipata kukimbiza Mwenge huo Nchini Msumbiji Mr Antony Mtaka akilalamika kuhusu watu wanaopiga vita mbio za Mwenge na kuwashutumu vijana ambao wanaonekana kutojua faida zake na kuwaona wanasiasa hasa upinzani japo hakuwataja, kama watu ambao wako mstari wa mbele kupinga mbio hizo za Mwenge.
Hakika mimi ni mmoja wa watu ambao kidogo nilipata kuona kidogo uzuri wa mbio za Mwenge miaka ya mwanzoni ya tisini nikiwa shule ya sekondari,na pia nimesikia simulizi zake, kuwa enzi ya Mwalimu Mwenge ulikuwa ukipita kwenye shirika la umma au ofisi yoyote ya Umma basi ukiondoka baada ya muda utaona mlipuko wa kusambalatisha watendaji wote ovyo waliokuwa wanashiriki kuyumbisha shirika au ofisi ya umma.
Hii inaonyesha ubunifu mzuri ambao Mwalimu kupitia wataalamu wake wa kutafuta taariifa za Serikali walimpomfikishia taarifa za matatizo ya watendaji wa Serikali na Mashirika basi yeye alitumia nafasi hiyo kurekebisha na kuwaadhibu viongozi hao huku wananchi wakiwa na ufahamu huo kupitia Mwenge kwa hiyo Wananchi walikuwa na kiu kila pale mwenge ulipopita ulizaaa matarajio ya wananchi hao.
Lakini leo wananchi wanaona Mwenge kama Ngeo na chombo cha mafisadi wa umma kujichotea fedh kupitia mfuko wa kuendeshea mbio hizo, na si alama ya
Uzalendo na Umoja [Patriotism & Unity].Na pale ambapo Serikali imekosa Ubunifu wa kuwalithisha Watanzania vijana na watoto kuwa
Mwenge ni Alama ya Umoja wa Umma na matokeo yake umekaa sana kisiasa badala ya kuwa ni KITAIFA na kuondoa ubinafsi wa chama tawala kuhodhi mbio hizo.
Umefika wakati mbio hizo kuludi kule kwenye mfumo wa utekelezaji wa Mwalimu wa kufumua na kuwafunga Mafisadi kuanzia ngazi ya kata, tarafa, wilaya ,Mkoa na atimae Taifa.Pia mbio hizo kuwa ni kitivo cha kuongoza na kuelimisha umma hasa vijana kupitia vipeperushi,elimu ya vitabu au majarida na sio kukusanya viongozi wa Serikali na kuanza kufukuzana nao huku na huku wakinyemelea posho kwa mgongo wa Mwenge.
Na Mwenge huo ukimbizwe na vijana kutoka kada zote na vyama vyote na sio vijana wa CCM tu,Wachaguliwe vijana wakakamavu kutoka CCM,CDM,CUF,NCCR na hata vyama vya Kitaaruma Vyuo na Shule za Sekondari na Msingi kuonyesha kuwa ni Kikundi cha kitaifa na mbio za kitaifa na sio kuwa ni Mali ya CCM.
Maoni yangu mimi kama Kijana tunauitaji Mwenge huo kama alama ya umoja ambako kila unakopita unatukumbusha na kutuhamasisha kama Taifa moja nje ya vyama vyetu vinavyotwambia kuwa wewe ni MwanaCCM na yule ni Mwana CDM na Kaka yake nani yeye Ni CUF.
Ila naungana na wadau wote wanaopigania mabadiliko na mageuzi ya uendeshaji mbovu wa sura ya MBIO HIZO ambao ndipo umekaa KIFISADI kiasi kuwa unaunda chuki dhidi ya wananchi na Mwenge huo.Tunaitaji kubadilisha mfumo wa kukimbiza mwenge wa kizamani na kuweka katika mfumo unaokubalina na kizazi kipya cha vijana wa kuaniza miaka ya sabini na kushuka chini yaani uwe
Moden Torch of Freedom.
Nawasilisha

Hati ya Uhuru wa Tanzania na Mwalimu Julius K Nyerere [By Then Tanganyika]

Marehemu Baba wa Taifa Julius Kambarage Nyerere

Marehemu Meja Alexander Gwebe Nyirenda akipokea Mwenge.

Marehemu Meja Alexander Gwebe Nyirenda akipandisha Mwenge Juu Ya Mlima Kilimanjaro

Mwenge wa Uhuru Nadni ya Shilingi Moja
View attachment 39494
Ngao ya Tanzania [coat of arms] yenye Mwenge wa uhuru