MwanaFalsafa1
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 5,565
- 843
HIVI KUNA nchi nyingine yenye ritual/practice kama hii?
Maadam hayo ndio yalikuwa madhumuni ya kuwasha na kukimbiza mwenge nadhani yamefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kwani hadi leo hii tunaishi KiMungu Mungu tu..yaani pale pasipo na matumaini tunapita, misaada inamwagwa...SISI TUNATAKA KUWASHA MWENGE ..Mlima Kilimanjaro
Umulike nje ya mipaka yetu...ulete tumaini
pale ambapo hakuna matumani, upendo mahali ambapo pana chuki na heshima ambapo pamejaa dharau
Huo wimbo ulikuwa unaelezea madhumini ya kuwasha na kukimbiza mwenge!
Je kwa miaka yote zaidi ya 40, mwenge umekamilisha nini kati ya hivyo?
Maadam hayo ndio yalikuwa madhumuni ya kuwasha na kukimbiza mwenge nadhani yamefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kwani hadi leo hii tunaishi KiMungu Mungu tu..yaani pale pasipo na matumaini tunapita, misaada inamwagwa...
Upendo pale penye chuki..heshima penye dharau kwani mnaona Mafisadi wote tunakula nao sahani...hakuna chuki bali heshima na upendo..
Tatizo sio mwenge isipokuwa sisi ndio tumepoteza mwelekeo na UHURU kwetu hauna maana tena..Na nafikiri ukimuuliza mtoto wa shule ya sekondari leo hii nini maana ya UHURU utapata majibu mia kidogo kwani maana halisi imekwisha potea..Hakuna tofauti kati ya kutawaliwa au kuwa huru maadam wananchi bado wako mikononi mwa watawala watunzi wa sheria..
Madhumuni ya mwenge wetu ni sawa na mwenge wa Olyimpic ambao mbali na kuashiria kuanza kwa michezo hiyo hutangaza matumaini, upendo, heshima na zamani ilikuwa mwisho wake kama sijakosea zamani mwenge ulikuwa ukihitimishwa na sikukuu ya Wakulima tukiita Sabasaba..Ilikuwa siku kubwa sana Tanzania nzima toka vijijini, wilayani hadi mikoani, pengine ikisherehekewa kuliko hata siku ya Uhuru wenyewe..
Hapo wakulima huonyesha mavuno yao na mashindano mengi ikiwa ni pamoja ngoma za kienyeji, costumes, ukubwa na uzito wa mazao, maonyesho ya mbegu mpya na kadhalika.. maadam siku hiyo ilikuwa furaha tupu kwa wananchi wote Tanzania utafikiri kweli Olympic ya Watanzania..Ni vigumu sana kumwelezea mtu ambaye hakuwepo miaka hiyo ya 60 na 70 kwani haya yote hayapo tena leo...
Tuliobadilika ni sisi sio mwenge na lawama zetu haziwezi kuwa na msingi wowote kwa sababu ya mwenge unaowashwa kwa mafuta ya taa kuwa sababu ya kupoteza fedha..
Jamani me napenda kutoa dukuduku langu kuwa hivi kutembeza mwenge nchi nzima kuna umuhimu kweli kwa sasa? Hatuna zahanati za kutosha, Madarasa ya shule hayana viti wala vifaa vya kishule. Lengo la mwenge ilikuwa kujikumbusha UHURU WETU na kujenga umoja na mshikamano, Lakini ukiangalia tuna tarehe ya UHURU inatosha pia kama nikufikisha ujumbe kwa wananchi tunaweza kutumia TV, Magazeti na ziara za viongozi!!
Hili mnalionaje wana ThinkTanker!!
Jamani me napenda kutoa dukuduku langu kuwa hivi kutembeza mwenge nchi nzima kuna umuhimu kweli kwa sasa? Hatuna zahanati za kutosha, Madarasa ya shule hayana viti wala vifaa vya kishule. Lengo la mwenge ilikuwa kujikumbusha UHURU WETU na kujenga umoja na mshikamano, Lakini ukiangalia tuna tarehe ya UHURU inatosha pia kama nikufikisha ujumbe kwa wananchi tunaweza kutumia TV, Magazeti na ziara za viongozi!!
Hili mnalionaje wana ThinkTanker!!
Mzee Es, nitakujibu kwa kina baadaye kwani mimi ni mmoja wa watu walio"bahatika" kuwa wakimbiza "moto"...
Mwenge hauna maana yoyote, basi kwa sababu watu wanatafuta kazi ya kufanya na night allowance inabidi wa uweke.Nina imani hata viongozi hawaoni maana yake kwa sasa hivi ila nani atamfunga paka kengere?
Kiongozi gani atasema kuwa mwenge sasa basi.Mimi nitawasaidia watafute nafasi pale mnazi mmoja wautundike pale mtu akitaka kuoona aende pale kwa mda wake, au wauweke jumba la makumbuusho haina haja yoyote kwa sasa kukimbiza mwenge.Nikupoteza muda.
Nilipokuwa shule ya msingi,tulikuwa tunaacha masomo na kwenda kuupokea mwenge wa uhuru.
I feel hii ilikuwa brainwashing ya kutupwa.
Kama wewe ulishiriki kukimbiza huu mwenge ,tuambie faida zake!
Nilipokuwa shule ya msingi,tulikuwa tunaacha masomo na kwenda kuupokea mwenge wa uhuru.
I feel hii ilikuwa brainwashing ya kutupwa.
Kama wewe ulishiriki kukimbiza huu mwenge ,tuambie faida zake!
Kuna mwaka fulani katika mkoa mmoja wa Pwani,baada ya mkesha wa mwenge asubuhi ziliokotwa ndoo mbili zimejaa kondomu zilizotumika, wanaume walikesha haswa!
Posho kwa wakubwa, maambukizo ya ukimwi, kulazimishana michango na mambo mengine wenzagu wataengeza.
hebu angalia asili a mwenge wa uhuru, utaona mambo mengi tu positive.