Mwenge wa Uhuru upo kwa faida ya nani?
Ebanaaeee..nilikuwa nasikia mwenge mwenge..juzi nikasema ngoja nikauone!!!

Nilitegemea nitakuta ni limoto likubwaaaaaaa linawaka eneo lote linakuwa na mwanga.

Picha linaanza tumefika eneo la tukio saa 4 usiku sion hata mwanga wa moto naona tu balbu za umeme. Nikauliza "Oya mwenge umeshasepa? Akinionesha ule pale!!

Wakuu Nilishangaa mnooooo!!! Kamoto kadogo af jamaa wamekazunguka!! Af nilicheka kwa chini chini hadi machozi!!!
 
Na hauna replacement, mwenge huu unaojulikana wa UHURU umeisha nguvu na umeshindwa kuwamulika CCM wezi wa kura walioliteka jeshi la polisi na kulitumikisha kama punda, hapa tulipo Jeshi la polisi limekuwa mtumwa wa CCM. Polisi wanashindwa kuwakemea CCM,inaonekana wazi CCM wanafanya mikutano kila pembe lakini wengine ni hapana na inakuwa ni kosa kubwa sana ,la jinai .

Mwenge umeshindwa kuiona hali hii na hauna tena zile nguvu zake eti umulike kila kona,hamna kitu tena na nina wasiwasi karibu CCM watafanikiwa kuuzima hata hako kajimuangaza kalichobakia,ili wainyonyoe Tanzania na kuacha mashimo matupu.

Mwenge umeshindwa kuimulika CCM na matendo yake.
 
Magufuli alisitisha mbio za huo Mwenge mkamtukana weeee!
Kwamba kasitisha kidikteta na kibabe bila kushirikisha wengine, na pia kasitisha sababu kaharibu uchumi na hivyo hana hela za kufadhili mbio za huo Mwenge!

Sasa ni hivi, mimi binafsi siasa za tangu Jk, Magu na sasa Samia zimenifundisha mambo mengi sana juu ya watz.

Kwahiyo Samia wewe ongoza nchi uonavyo tena ikiwezekana apore hata hela akafiche ughaibuni huko!

Na mtumishi yeyote mwenye nafasi asipofisadi kwa kigezo eti anafanya uzalendo atakuwa mpumbavu sana!
 
Mataga na UVCCM hawana akili, hawajui tofauti ya kukosoa na kutukana.

Katiba mpya yazidi kurindima, Dr. Hosea anena

Serikali iache matumizi ya anasa, Serikali ina matumizi ya hovyo, luxury na anasa

Viongozi wanafanya ubadhirifu, na Ufisadi, .. Wananchi wanashindwa kuwawajibisha. KATIBA MPYA inatakiwa

Mwenge ni mojawapo ya matumizi ya hovyo
 
Na hauna replacement ,mwenge huu unaojulikana wa UHURU umeisha nguvu na umeshindwa kuwamulika CCM wezi wa kura walioliteka jeshi la polisi na kulitumikisha kama punda,hapa tulipo jeshi la polisi limekuwa mtumwa wa CCM. Polisi wanashindwa kuwakemea CCM,inaonekana wazi CCM wanafanya mikutano kila pembe lakini wengine ni hapana na inakuwa ni kosa kubwa sana ,la jinai .

Mwenge umeshindwa kuiona hali hii na hauna tena zile nguvu zake eti umulike kila kona,hamna kitu tena na nina wasiwasi karibu CCM watafanikiwa kuuzima hata hako kajimuangaza kalichobakia,ili wainyonyoe Tanzania na kuacha mashimo matupu.

Mwenge umeshindwa kuimulika CCM na matendo yake.
UMEBAKIA KUENEZA UKIMWI....TU😃😃🤣👆😁😁
 
Mimi binafsi hadi leo sielewi kwa kina nini maana ya mbio za mwenge,unasaidia nini ktk taifa letu ukikimbizwa na usipokimbizwa.Kuna mambo nikiulizwa mf nini faida ya majeshi yetu najuwa na kazi zao naona.Tafadhali wanajf
 
Hakuna faida ya mwenge lakini unadumaza akili za watanzania yaani hakuna kuhoji,lakini pia kama unawatoto waambie kabisa wasikaribie huo Moto ni hatari Kwa maisha yake
 
Kuuliza si ujinga na aulizaye ataka kujua. Mantiki ya kuwa na mwenge unaozungushwa mikoa na wilaya zote Tanzania kwa mazingira ya sasa ni nini? bajeti yake ni kiasi gani na nani anayegharimia? Kiongozi wake huchaguliwa na nani na vigezo vya kumchagua kiongozi huyu wa Mwenge ni vipi? Kuna siku nilimwona kwenye luninga akifanya ukaguzi wa madarasa ya shule moja mkoani akilalamika kwamba fedha hazikutumika ipasavyo. Kwani yeye anahusikaje na matumizi ya fedha za halmashauri? Tafadhali mwenye uelewa atujuze.
 
Kiufupi shughuli za mwenge zina poteza pesa na mda ambao wanaitajika kugua miradi ni viongozi na watendaji waliopewa madaraka.
Swala la kutembeza mwenge na kuweka mikesha tunajionesha bado ni nchi changa iliyozaliwa jana.

Pesa ya mwenge na kazi zake zingekuwa kwa CAG maana yeye ndio mkaguzi wa mapungufu yote na mwenendo wa utendaji wa serikali.
 
Achana na hiyo kama unaweza kusafiri mwanza mpaka dar kuzindua vizimba vya samaki/ wavuvi ziwa victoria ila ukashindwa kwenda arusha mei mosi kwenye sherehe za waliowajiri, unahisi kuna nn hapa poti
 
Hilo ni jambo muhimu sana, baada ya kopo lonalowaka na kutembezwa kila mahali, linaloitwa Mwenge wa Uhuru kuwasili Mkoani Dar es Salaam, Wakazi wa Mkoa huo wamejitenga wazi wazi na Ibada hiyo ya Shetani, Mapokezi ya mwenge huo yamebaki kuwa ya wanaccm wachache na viongozi wao tu, Jambo hilo ni sawa na ushindi kwa Wanaopinga jambo hilo.

Ikumbukwe kwamba Mbio za mwenge za DSM ndio zilizopigiwa promo kuliko popote.

Hata hivyo uchunguzi wetu umebaini kwamba, tangu enzi na enzi hakujawahi kuwepo na mradi wowote uliozinduliwa na Mwenge wa Uhuru uliowahi kudumu hata kwa miezi 6, Wanazuoni wanadai hilo linatokana na ghadhabu za Mungu kwa ibada hiyo ya Shetani

Kwa kulijua hili Wakazi wengi wa D'salaam kwa kauli moja wameamua kupuuza kabisa jambo hili ili kuondoa Nuksi
 
Huku kigamboni kesho ndio mwenge sasa hv tupo tunakula beer za bure na kesho tunaenda chukua posho..
Pamoja na kuzisarambua posho(kwa wajanja tu)
N.B wakizeleta we tafuna ila sualala KATIBA MPYA lipo palepale TUNAITAKA
 
Pigeni hela Wanangu
 
Hilo ni jambo muhimu sana, baada ya kopo lonalowaka na kutembezwa kila mahali, linaloitwa Mwenge wa Uhuru kuwasili Mkoani Dar es Salaam, Wakazi wa Mkoa huo wamejitenga wazi wazi na Ibada hiyo ya Shetani, Mapokezi ya mwenge huo yamebaki kuwa ya wanaccm wachache na viongozi wao tu, Jambo hilo ni sawa na ushindi kwa Wanaopinga jambo hilo.

Ikumbukwe kwamba Mbio za mwenge za DSM ndio zilizopigiwa promo kuliko popote.

Hata hivyo uchunguzi wetu umebaini kwamba, tangu enzi na enzi hakujawahi kuwepo na mradi wowote uliozinduliwa na Mwenge wa Uhuru uliowahi kudumu hata kwa miezi 6, Wanazuoni wanadai hilo linatokana na ghadhabu za Mungu kwa ibada hiyo ya Shetani

Kwa kulijua hili Wakazi wengi wa D'salaam kwa kauli moja wameamua kupuuza kabisa jambo hili ili kuondoa Nuksi
Hujawahi kulitakia mema Taifa la WaTanzania. Yaani unaona mwenge, ambao ni ishara ya Uhuru Africa ni Ushetani?

Ulaaniwe.

Ukweli ni kwamba weye ndie unayefanya kazi za kishetani, na uwakala wa mabeberu
Kila ukiuona, unapagawa kwa jinsi mionzi yake inavyofukuza mabeberu.
 
Ibada ya kishirikina haijawahi kuwa baraka.
 
Habari WanaJF,

Hivi mwenge wa uhuru una umuhimu gani na unasaidia nini?

Ama ni matambiko?

Tukikimbiza kile kitorchi uhuru unaonyesheshwaje?

Naomba kulelezwa ni alama ya uhuru ama utumwa?

Mzalendo daima
 
Back
Top Bottom