Asalaam alaykum,
Wito Sina Nia ya kuchafua serekali. Hivi kwa kipindi hichi cha janga la wimbi la tatu la Covid, Kuna umuhimu gani wa kukimbiza mwenge? Maana naona unaleta mikusanyiko isiyo na ulazima na kuchochea ongezeko la ugonjwa huu. Mfano mzuri niliona Jana mwanza,bmwenge ulilala wilaya ya nyamagana (buhongwa shuleni) kikweli nilisikitika Sana watu walikuwa wengi hakunaa social distance ya mtu na mtu, mask zilikuwa zinatolewa Ila asilimia kubwa walikuwa hawana cause Ni wananchi wa chini, pili kulikuwa na show za wasanii watu walikuwa wanajazana wakiwa wamezunguka kuwashangaa.
Tatu usiku walikesha na disco vumbi usiku kuchaa. Mbaya zaidi kulikuwa na kundi kubwa la wanafunzi na watoto wengine hambao hawajui tahadhari au Kinga kifasaha kuhusu covid. Ni aibu kwa serekali kuu ambayo inajifanya inajali kuhusu wimbi la tatu la covid huku wakiruhusu mwenge uzunguke nchi mzimaa. Shame on you!
Kuna ulazima gani wa kukimbiza mwenge? Na ksma Kuna ulazima kwani wasiuzungushe na magari tu na ukifika wilaya au mkoa unapotakiwa ukalale, ulalee ofisi ya mkuu wa mkoa au wilaya na kuwe na limit ya watu.
Alafu najiuliza, huo mwenge kwa Karne hi unamanufaaa gani kwa taifa?maana naona unahamashisha ulevi, uzizii, ugovi wa familia na watoto kupotea kila utapo lala mahali.mtanisamehe sio muandishi mzuri Ila naomba kuwakilisha.
Sent from my TECNO B1p using
JamiiForums mobile app