Mwenge wa Uhuru upo kwa faida ya nani?
Sijawahi kujua faida ,uhitaji wa mwenge, tuboreshe na kumpa nguvu zaidi Ofisi ya CAG, kwani kubwa mwenge walau ukaguzi wa miradi kwa macho kwa sekunde chache.Garama za mwenge mbali ya pesa, watendaji selikali mkoa ndani ya mwezi wapo busy na vikao mwenge! Hauna tija.
Kwanini Mwenge hauko audited?
 
watu ni waoga sana wa mabadiliko, they are comfortable with what they are used to. kiukweli hata rais moyoni mwake anajua kuwa mbio za mwenge ni ujinga na ndio maana hawatengi fedha za kutosha, mwisho wa siku watumishi kwenye halmashauri wanalazimika kuchangia jambo la kipuuzi lisilo na logic yoyote. muda umefika sasa wa tawi losilozaa matunda (mbio za mwenge) kukatwa na kutupwa motoni. Ule mwenge tunaweza kuujengea sehemu maalum ukae hapo.
 
Wapuuzi sana hawa maccm December hatukusherekea miaka 57 ya uhuru wa Tanganyika. Nduli alidai 900 millions sijui za sherehe hiyo sijui kazihamishia wapi. Muungano pia wa miaka 55 akadai hivyo hivyo sikumbuki vizuri bajeti ya sherehe za Muungano ilikuwa ni kiasi gani lakini haikufika bilioni 1.

Gharama za kukimbiza hiyo tochi yao ni bilioni 200 kwenda juu. Siku hizi wakiulizwa gharama hawasemi tena wanaficha lakini cha ajabu huyo nduli na dikteta wa Ikulu haoni kama gharama hizo hazina maslahi yoyote kwa Watanzania.

Ina maana kwa miaka mitano zaidi ya trillion 1 hadi 2 inatumika kwa shughuli hiyo ya kipuuzi. Fikiria hiyo pesa ingetumika kwenye mambo yenye maslahi kwa Watanzania ingefanya mazuri mangapi ukilinganisha na kukimbiza hiyo tochi yao.


Mwenge huu hata CCM wenyewe hawautaki. Wapo naona kwasababu wanachomoa chomoa hela za mafuta, na pia Mwenge unawasaidia kuwapumbaza wananchi.
Pascal Mayalla, GuDume, BAK, maggid, Sky Eclat , Mzee Mwanakijiji na wachambuzi wengine wakaribie ili tufaidi hasara na faida za kitu hiki.
Kipekee said mohamed mzee mbobezi wa historia ya Tanganyika, kabla na baada ya Uhuru, atatupa kiunaga ubaga historia ya huo Mwenge, kuanzia harakati za kina Forojo Ganze na wenzake Sheikh Yahya Hussein, hadi walipoufikisha magogoni.
Asante
 
Mbaya zaidi wanawasumbua watumishi wa umma kwenye almashauri zao kuchangia mwenge. Mishahara yenyewe haipandi tangu 2016 lakin kila mwaka watumishi wanatakiwa kuchangia mwene
 
Ukitaka ulaji omba uchaguliwe kuwa kiongozi wa mwenge kitaifa. Ukishazunguka Tanzania nzima per diem yake utaupa umasikini a short break.
Ndio ndio,hili lipo Wazi My sister.

Mwenge unawaotesha vitambi,Wanavuna mijihela.

Hivi wale Maskauti niwaonao,Huwa ni Maskauti Wa Roman Catholic...? Au ni jezi tu zimefanana..?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ndio ndio,hili lipo Wazi My sister.

Mwenge unawaotesha vitambi,Wanavuna mijihela.

Hivi wale Maskauti niwaonao,Huwa ni Maskauti Wa Roman Catholic...? Au ni jezi tu zimefanana..?
Wale ni chipukizi wa UVCCM
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hoja ni ya msingi sana kwa sasa.
Bajeti yake ingeweza kufanya mambo mengi ya muhimu.Ifutiliwe mbali
Mungu pekee huweza kuleta Amani na Utulivu,si mwenge.
 
Naunga mkono hoja...hii kitu binafsi naichukia.. Kudumisha amani hakufanywi na kitu bali watu. Naungana na mtoa hoja.
 
NB:-
Moderator, Uzi huu usiunganishwe na Uzi mwingine wowote, wala usifutwe. Una tija na maslahi mapana ya ukuaji na ustawi wa taifa letu
Mwengee wooooo mwenge... mbiyo mbiyo.... mwenge tunaukimbiza... mbiyo mbiyo hadi makawo makuwu... mbiyo mbiyoo...
Inasikitisha sana gharama zinazotumika na nguvu kazi zinavyotumika pasipo maslahi yenye tija kutokana na huo mwenge. Binafsi naona huu mwenge ni dumazisho la fikra kwa wananchi... ukitaka shuhudia ubaya wa mwenge na athari zake ni pale unapolala mwenge... matendo ovu yote hutendeka pasi kizuizi wala kemeo...
Kwa wanaouabudu mwenge hili bandiko ni sumu mbaya kabisa kwao..
 
1. Mwaka 2014 zilitumika zaidi ya Billion 120 kwa tabia zetu za wizi,ufisadi na ubadhirifu nathubutu kuweka round figure kuwa billion 170 na sitoshangaa ikawa mara 2 zaidi



2. Mwaka 2015 zilitumika Billion 180



3. Mwaka huu zimetumika Bilioni 220



Hapo ongeza muda ambao watu wametumia kutofanya kazi, foleni,Ongezeko la Ukimwi, na mengineyo hivyo nathubutu kusema kwa mwaka huu mwenge una cost taifa si chini ya TRILLION 1 na nusu



Pesa zipo nyingi tuu maana wakati huo huo serikali kupitia TANESCO inawalipa IPTL shilling million 400 kwa siku na kila siku inashindwa mahakamani.



Naamini maneno ya Magufuli kuwa pesa iko nyingi sana nchi hii na hatuhitaji misaada toka kwa wazungu.









Tarehe 27 mwezi May, mwaka 2014 siku ya Jamanne majira ya saa 4 asubuhi, kwenye kipindi cha maswali na majibu, Naibu waziri wa habari vijana, utamaduni na michezo Juma Nkamia alieleza makadirio ya gharama za kukimbiza Mwenge wa Uhuru nchini.



Nkamia alisema "serikali kuu hutenga kiasi cha fedha kulingana na mahitaji na gharama halisi ya wakati husika.. Mwaka 2012 jumla ya shilingi Bilioni 43 zilitumika ambapo kati ya hizo Bilioni kumi na moja (11) zilitengwa na serikali na Bilioni 32 zilichangwa na mashirika, taasisi, makampuni na wadau mbalimbali walioombwa kuchagia kwa ajili ya kuadhimisha uzinduzi na kilele cha mbio za mwenge wa uhuru." Taarifa zinaonesha kuwa mwaka 2014 inakadiriwa jumla ya Shilingi Bilioni 120 zilitumika kama gharama ya kukimbiza Mwenge nchi nzima.

CALCULATION.



Bilioni 120 zinazotumika kukimbiza mwenge nchini (mwaka huu huenda zikaongezeka), zinatosha kufanya yafuatayo;



1. Kununua mashine 60 za MRI na CT Scan kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa wenye kuhitaji vipimo hivyo. Ikumbukwe hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuna mashine moja tu ya MRI na moja ya CT Scan ambazo zote ni mbovu. Fedha za Mwenge zinaweza kununua mashine 60 za aina hiyo.



Rais Magufuli alijaribu kuhimiza ukarabati wa mashine hizo lakini zilifanya kazi kidogo tu kisha zikafa tena. Kwa sasa hakuna huduma za Vipimo vya MRI Hospitali ya Muhimbili, hadi imefikia hatua wagonjwa wametunga kirefu cha MRI kuwa ni;

-Magufuli -Rudi -Imeharibika tena.



2. Shilingi Bilioni 120 zinazotumika kukimbiza Mwenge zinatosha kulipia mikopo ya wanafunzi 61,624 wa vyuo vya Elimu ya Juu nchini. Hadi sasa takribani wanafunzi 40,000 walioko vyuoni hawajapata mikopo. Kumbe fedha za Mwenge zingeweza kuwalipia mikopo wanafunzi wote walio
 
Ambacho Watu wasiojulikana hawakiwezi ni kuteka nchi nzima, kutesa nchi nzima na kuwapoteza raia wa nchi nzima.
Kutumia Watu wasiojulikana kuzuia kuhoji ni upumbavu na unyafuzi wa fikra
Wasichokijua zaidi ni kwamba hata kwenye jalala wasilolipenda wanaweza pata msumari wa kuungia tanga la jahazi lao...
Nilipata kuandika mfalme aliyependa sifa alitembea utupu mji mzima akisifiwa uzuri wa vazi lake mpaka alipozinduliwa na kitoto kidogo... "...babu usiii chapa!" Ndipo akatanabahi na waliomsifu wakatahayari huku akiamuru wakamatwe...
 
Back
Top Bottom