Mwenge wa Uhuru upo kwa faida ya nani?
Uhuru umeshapatikana mkoloni ameondoka,(kiaina)sasa ni za zamu ya mafisadi wakoloni weusi, makaburu weusi, huu mwenge uwamulike hawa mamluki.
 
Leo naona kiongizi wa mbio za mwenge akichoma moto zana za uvuvi haramu ktk ziwa Victoria.Hivi hili nalo lilisubiria mpaka mwenge ufike kweli?
 
Kizazi cha .com si rahisi kuelewa maana ya Mwenge!
 
ccm hawezi kuufuta mbio za mwenge hio ni ibada ya kanisani katoliki hawawezi kukubali
 
Kama kichwa kinavyo eleza mwenge kwa sasa ndicho chombo katika serikali kinakula pesa za walipa kodi bila ya kuwa na faida yoyote!Nimesema hivyo baada ya kiongozi mkuu wa nchi kufuta posho zote za viongozi wa serikali waliokuwa wanaenda Mkoani Simiyu hii inadhihirisha kuwa Mwenge hauna manufaa yoyote zaidi kufuja.
Nasasa ni wakati wa kupaza sauti na kuupinga mwenge.
 
Imeibuka staili ya watu kushangilia kila kitu ili mradi kafanya wa chama chake! Hasa wana ccm. Juzi rais kafuta posho wamepongeza. Maana yake wasingependa mbio za mwenge ziendelee kuwepo!
Huwezi kupongeza kuokoa sh 10,000 huku unampongeza kutumbua milioni kumi. Huu utakua wendawazimu. Tuwe wawazi watanzania kwa sasa hatuutaki mwenge ukimbizwe.

Ikifika siku mkuu wa nchi akasema mwenge basi mtatiririka kwa pongezi ila kwa sasa mko kimyaaaaa!!

Haya nataka mje hapa wana ccm na msio wana ccm ambao sio wanafiki mseme wazi. Wangap mnasema mbio za mwenge zifutwe mwenge uende makumbusho??

Mnaosema uendelee kukimbizwa wekeni sababu zenu. Tunaopinga tunasababu ya kutumia pesa nyingi bila kuleta tija kwa taifa.haya tiririka hapa.
Kumbuken sipendi unafiki.
 
OMG mbona umekuwa mkali hivi?

Yaan ningekua na mamlaka kuna watu ningewatandika viboko kwa unafiki wao.
Wanampongeza mtu kwa kuokoa hela ya siku moja huku hawamuulizi hizo zilizotumika miezi yote kwann hukuziokoa?? Huku si kudhihirisha ile 1/4 ya ukichaa?? Huenda kwa hili ni 2/4 ni wendawazimu.
Yaan siwapendi wanafiki hatari!!
 
Back
Top Bottom