Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wanabanjuana sana kwenye mikesha ya mwenge asubuhi ndocom kibao zinakutwa uwanjani!..kwanini mlipa kodi wa Tanzania abebe gharama za mambo yasiyo na maana kama yanayoonekana kwenye clip hapo juu?
Ni kweli mbio za mwenge ni upuuzi mtupu lakini zikifutwa yawezekana tutakuwa tunaua kiwanda kimojawapo wakati kipaumbele chetu ni kujenga taifa la viwanda.Mbio za Mwenge zifutwe. Zinatupotezea mali, fedha, na muda wa kufanya kazi.
Mwenge wa uhuru upo kwa faida moja tu, ya ccm kundelea kutawala na kupumbaza.Leo kwa mara nyingine mbio za mwenge zimeanza tena Tanzania, na safari hii mwenge umewashwa huko Dole Zanzibar kuendeleza ile adhma ya taifa letu changa kuwa "sisi tumekwisha kuwasha mwenge na kuuweka Kilimanjaro". Mwenge huu ulipowashwa mara ya kwanza na kuwekwa kwenye kilele cha Kilimanjaro na Nyirenda, ulikuwa uwe ishara ya matumaini, upendo, na umoja wa Taifa letu.
Matukio ya hivi karibuni hasa baada ya muasisi wa mwenge huo kufa, kuna kila dalili kuwa tunachokimbiza sasa hivi ni kivuli tu cha mwenge ule kwani miale ile ya mwanzo ya mwenge wetu wa uhuru imeanza kuzimika na inaonekana ikififia kila mwaka mpya ujapo. Mwenge huu sasa umekuwa ni alama ya watu wachache kujiangazia wao na familia zao huku sisi wengine tukiendelea kubakia gizani. Hakuna kitu kinachoonesha kufifia kwa mwenge huo kama suala la mikataba ya nishati, madini, ununuzi wa rada, ndege ya rais, n.k Zaidi ya yote kwa wanafunzi waliokwama Ukraine, mwenge huu kwao tayari umezimika ( a little strech there, but why not try..??)
Je kuna matumaini ya kurejesha nuru yake tena? Je kuna haja ya kuuwasha tena ili uendelee "kuwamulika" wabadhirifu, wazembe maofisini, wala rushwa magendo n.k ? Au tuamue kuuzima tu, ili kila mtu ajiwashie mshumaa wake yeye mwenye na wale wenye uwezo wawashe vibatari, chemli, na taa za umeme! ?
huu mwenge kweli tunasababu ya kuendelea kuukimbiza?
sijakusikia tangu mkuu wa nchi amsamehe makonda/bashite kwa kuingiza makontena yote yale bila kulipa ushuru tena kwa jina lake. na bado yupo ofisini anapiga kazi na majigambo yalopitiliza. sijakusikia ukizungumza llote juu ya mkuu wa nchi kuwapa kifuta machozi wakae kimya wahanga wa mv .Nyerere huku wale wa arusha na bukoba wakiambulia hakuna. sijakusikia ukiuliza kwann mkuu wa nchi hajaenda kuwafariji wahanga na kuzika badala yake alikunywa chai na mapolisi ikulu. kwako wewe mwenge ndio jambo muhimu kwakuwa unataka kuffisha mjadala ?Leo kwa mara nyingine mbio za mwenge zimeanza tena Tanzania, na safari hii mwenge umewashwa huko Dole Zanzibar kuendeleza ile adhma ya taifa letu changa kuwa "sisi tumekwisha kuwasha mwenge na kuuweka Kilimanjaro". Mwenge huu ulipowashwa mara ya kwanza na kuwekwa kwenye kilele cha Kilimanjaro na Nyirenda, ulikuwa uwe ishara ya matumaini, upendo, na umoja wa Taifa letu.
Matukio ya hivi karibuni hasa baada ya muasisi wa mwenge huo kufa, kuna kila dalili kuwa tunachokimbiza sasa hivi ni kivuli tu cha mwenge ule kwani miale ile ya mwanzo ya mwenge wetu wa uhuru imeanza kuzimika na inaonekana ikififia kila mwaka mpya ujapo. Mwenge huu sasa umekuwa ni alama ya watu wachache kujiangazia wao na familia zao huku sisi wengine tukiendelea kubakia gizani. Hakuna kitu kinachoonesha kufifia kwa mwenge huo kama suala la mikataba ya nishati, madini, ununuzi wa rada, ndege ya rais, n.k Zaidi ya yote kwa wanafunzi waliokwama Ukraine, mwenge huu kwao tayari umezimika ( a little strech there, but why not try..??)
Je kuna matumaini ya kurejesha nuru yake tena? Je kuna haja ya kuuwasha tena ili uendelee "kuwamulika" wabadhirifu, wazembe maofisini, wala rushwa magendo n.k ? Au tuamue kuuzima tu, ili kila mtu ajiwashie mshumaa wake yeye mwenye na wale wenye uwezo wawashe vibatari, chemli, na taa za umeme! ?
huu mwenge kweli tunasababu ya kuendelea kuukimbiza?
Umekurupuka sana... angalia hiyo post ni ya mwaka 2008 na sasa ni mwaka 2018, kuna mtu kaufufua huu uzi.... bytheway, kwani kila kitu lazima yeye ahoji?? kama na wewe ni mkereketwa kwanini usihoji??... usiwe mwepesi wa kupangia maisha ya watu, ishi uwezavyo.sijakusikia tangu mkuu wa nchi amsamehe makonda/bashite kwa kuingiza makontena yote yale bila kulipa ushuru tena kwa jina lake. na bado yupo ofisini anapiga kazi na majigambo yalopitiliza. sijakusikia ukizungumza llote juu ya mkuu wa nchi kuwapa kifuta machozi wakae kimya wahanga wa mv .Nyerere huku wale wa arusha na bukoba wakiambulia hakuna. sijakusikia ukiuliza kwann mkuu wa nchi hajaenda kuwafariji wahanga na kuzika badala yake alikunywa chai na mapolisi ikulu. kwako wewe mwenge ndio jambo muhimu kwakuwa unataka kuffisha mjadala ?
Wahenga walisema nzi akiacha ujinga anaweza kutengeneza asali.
Huwa nawaza km ulivyonena, mwenge hauna maanaWasalaam.
Kuna haja Sasa serikali iruhusu mjadala mpana iwapo Tunahitaji mbio za Mwenge kwenye hii karne ya Sayansi na teknolojia.
Mwenge umekuwa jero na hauna tija tena. Zama za kudanganyana kuwa Mwenge unaleta amani hazipo.
Amani inaletwa na kuvumiliana, kuheshimiana na kupendana.
Mwenge tunaona unazindua miradi ya bei chee, lakini miradi yote ya mabilioni inazinduliwa na Rais.
Mwenge umekuwa ni chanzo cha umasikini kwa wananchi. Wanachangishwa kwa lazima na wakati mwingine kuuziwa hata mifugo yao kwa nguvu.
Mwenge unasababisha ulevi na ngono zembe sehemu unapolala hivyo kuongeza idadi ya mimba zisizo tarajiwa pamoja na magonjwa yatokanayo na kujamiiana.
Wafanyabiashara wa ufuta Lindi wamechangishwa kila mmoja shilingi milioni mbili kwa ajili ya shughuli ya kuzima Mwenge, kwanini huo Mwenge uzimwe kwa mamilioni ya shilingi?
Pia Mwenge ni chukizo mbele ya mwenyezi Mungu. Nchi yetu inakabiliwa na magumu mengi kwasababu ya maneno magumu ambayo Mungu ameusemea Mwenge na waukimbizao huo Mwenge.
Isaya 50:11 Tazama, ninyi nyote mwashao moto, mjifungiao hiyo mienge; endeni ninyi katika mwali wa moto wenu, na katikati ya mienge mliyoiwasha. Mtayapata haya kwa mkono wangu; mtalala kwa huzuni.
Kila Siku huzuni imeifunika Nchi yetu. Nchi yetu ni ya NNE katika Nchi zenye huzuni zaidi.
Hatuna mafanikio kwenye kila tufanyacho.
Makinikia na fidia yake yameishia wapi?
Mradi wa gesi Mtwara iliyowakusanya watu wa mataifa mbalimbali uko wapi Leo?
Korosho zimegeuka kongosho, haziuziki, hata wakitokea wanunuzi wanakuwa magumashi.
Kwenye michezo tuna huzuni.
Kwenye viwanda Kuna huzuni, Hatuna viwanda, hata vile vya Kaijage havipo.
Kwenye biashara tuna huzuni.
Huzuni kila sehemu.
Nakaribisha kukosolewa na wale wanao Ona Mwenge una faida. Wasiporomoshe matusi ila watuambie Mwenge unafaida gani zaidi ya kututia umasikini?
Nchi nyingine zinapata hasara gani kwa ktokimbiza Mwenge?
Asanteni
Mwenge si lolote ila ni uchawi upumbazaoHuwa nawaza km ulivyonena, mwenge hauna maana