Mama Obama
JF-Expert Member
- Mar 5, 2016
- 1,621
- 1,087
Moja ya makosa makubwa sana ya mama SSH kufanya ktk baraza la mawaziri ni kumpa huyu mtu uwaziri. Lazima atamuangusha tu mama SSH, amejaa kiburi, dharau na kujisikia kupindukia na watu wa namna hii ni wanafiki mno
Hayati Magufuli amewaachia nchi ambayo aliyowajengea misingi mizuri ya ulipaji kodi na kupigana na ufisadi na wizi wa mali za wote. Wao wangeiboresha tu.Mama Samia kaingia madarakani kayavuruga yote ya Hayati Magufuli na kurudisha fedha kwa mafisadi.
Dr Mpango ndiye aliyekuwa Waziri wa fedha. Kuna watu walikuwa wakipiga tenda hewa na serikali na kulipwa mabilioni bila ya kufanya chochote. Serikali ikafanya kazi yake na kuokowa mabilioni kutoka kwa wezi. Mama Samia kasema hataki dhuluma. Wezi warudishiwe fedha zao! Kweli ni fedha zao? Na kuwafanya wote waliokuwa wakifanya kazi na Hayati Magufuli , waliopigana na wakwepa kodi na mafisadi mpaka Tanzania ikafika uchumi wa kati Sasa wanaitwa wadhulumaji.
Sasa Wanasema kodi zikusanywe kutoka kwa walala hoi. Kila senti moja wakipokea misaada kutoka kwa ndugu zao ambao wameisha katwa kodi, zinakatwa kodi tena. Sasa Wawekezaji fake na mafisadi wanasema wamefurahi na kupumuwa tangu Hayati Magufuli kutuacha. Hawa ni wachache tu waliokuwa wakiwalalia ndiyo wengi. Serikali lazima itafute kodi kutoka kwa wanyonge. Hiyo Rais Magufuli asingeruhusu, na wala isingetokea.
Serikali sasa inataka kodi kwa nguvu kutoka kwa walala hoi. ambao ni wengi. Kwa Hayati Magufuli haya yasingetokea. Mafisadi na wadanganyifu wasingerudiishiwa fedha walizowaibia Watanzania. Kungekuwa hakuna haja ya kuweka kodi kwenye huduma inayotumiwa na wanyonge wengi.