Mwigulu Nchemba awaambia Watanzania wahamie Burundi wasipoweza kulipa tozo za miamala

Mwigulu Nchemba awaambia Watanzania wahamie Burundi wasipoweza kulipa tozo za miamala

Moja ya makosa makubwa sana ya mama SSH kufanya ktk baraza la mawaziri ni kumpa huyu mtu uwaziri. Lazima atamuangusha tu mama SSH, amejaa kiburi, dharau na kujisikia kupindukia na watu wa namna hii ni wanafiki mno

Hayati Magufuli amewaachia nchi ambayo aliyowajengea misingi mizuri ya ulipaji kodi na kupigana na ufisadi na wizi wa mali za wote. Wao wangeiboresha tu.Mama Samia kaingia madarakani kayavuruga yote ya Hayati Magufuli na kurudisha fedha kwa mafisadi.

Dr Mpango ndiye aliyekuwa Waziri wa fedha. Kuna watu walikuwa wakipiga tenda hewa na serikali na kulipwa mabilioni bila ya kufanya chochote. Serikali ikafanya kazi yake na kuokowa mabilioni kutoka kwa wezi. Mama Samia kasema hataki dhuluma. Wezi warudishiwe fedha zao! Kweli ni fedha zao? Na kuwafanya wote waliokuwa wakifanya kazi na Hayati Magufuli , waliopigana na wakwepa kodi na mafisadi mpaka Tanzania ikafika uchumi wa kati Sasa wanaitwa wadhulumaji.

Sasa Wanasema kodi zikusanywe kutoka kwa walala hoi. Kila senti moja wakipokea misaada kutoka kwa ndugu zao ambao wameisha katwa kodi, zinakatwa kodi tena. Sasa Wawekezaji fake na mafisadi wanasema wamefurahi na kupumuwa tangu Hayati Magufuli kutuacha. Hawa ni wachache tu waliokuwa wakiwalalia ndiyo wengi. Serikali lazima itafute kodi kutoka kwa wanyonge. Hiyo Rais Magufuli asingeruhusu, na wala isingetokea.

Serikali sasa inataka kodi kwa nguvu kutoka kwa walala hoi. ambao ni wengi. Kwa Hayati Magufuli haya yasingetokea. Mafisadi na wadanganyifu wasingerudiishiwa fedha walizowaibia Watanzania. Kungekuwa hakuna haja ya kuweka kodi kwenye huduma inayotumiwa na wanyonge wengi.
 
Elimu ya Mwigulu Nchemba inatia mashaka sana.
Hakuna kitu hapo ni ujanja na uhuni yupo alipo
Mteuzi ameweka pamba kwenye masikio
Ugumu wa kutumbua ni vile teuzi ni za kulipana fadhila
Mteuzi akitaka kubadili upepo kwa faida ya wananchi na kutunza heshima yake kwa Taifa hili afanye haya....
Ajiepushe na wastaafu
Vunja Baraza la mawaziri na Bunge
Ajiepushe na wa kusifu na kuabudu
So far anasikiliza ya kuambiwa na makundi makundi
Asipofanya haya basi kizazi chake kitalipa machungu ya wananchi mbeleni

Mchumi uchwara alipashwa awe nyumbani anabeba watoto lakini ukimya wa mteuzi ni dalili za kubariki kejeli na dharau hizi.

Hii nchi ipo six feet kwa udongo
Mteuzi wake up n smell the coffee
 
Jeuri ya namna hii huwa wanakuwa nayo Wanasiasa wa Tanzania tu. Sababu wanajua Wananchi wa Tanzania wanaowalipa mishahara na posho. hawana la kuwafanya.

Ni kauli iliyojaa dharau, kebehi, kiburi, ujivuni, ubazazi, ubaradhuli na ulaanatullah. Huyu amejikinai. Hawajali wananchi maskini wa Tanzania. Na watanzania sababu ni wapole sana nadhani hatuna la kufanya.

Tumpongeze anaupiga mwingi sana.

ALIYOYANENA Mwigulu Lameck Nchemba ndiyo aliyoagizwa na mkuu wake Yaani Rais Samia. Na ili kuthibitisha hilo hamtaona akichukuliwa hatua zozote
 
Jeuri ya namna hii huwa wanakuwa nayo Wanasiasa wa Tanzania tu. Sababu wanajua Wananchi wa Tanzania wanaowalipa mishahara na posho. hawana la kuwafanya.

Ni kauli iliyojaa dharau, kebehi, kiburi, ujivuni, ubazazi, ubaradhuli na ulaanatullah. Huyu amejikinai. Hawajali wananchi maskini wa Tanzania. Na watanzania sababu ni wapole sana nadhani hatuna la kufanya.

Tumpongeze anaupiga mwingi sana.

Kumbe maagizo raisi aliyotoa wizarani baada ya kusikia kilio cha wananchi ni kwamba wasio taka kutoa kodi wahamie Burundi?
Kama kauli hii waziri ameitoa baada ya maelekezo ya raisi basi huu ndio msimamo wa rais.
Ila kama sii msimamo wa rais na ni baada ya maelekezo yake basi Waziri hamtilii maanani rais na anatamani kupindua maamuzi yake ili yale ya waziri yawekwe kunye kumbukumbu kua ndiyo sahihi
 
Kwa hiyo maelekezo ya Mhe, Rais kuhusu hizi tozo ni usanii mtupu kama majibu na misimamo wanayotayari. Kama Mama alimuwajibisha aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza (huenda kwa ile kauli yake inayokinzana na maelekezo ya Mama) huyu ni nani aendelee kuwa ofisini????
 
Kwani mama alikuwa ameenda kule ili kukwepa tozo mpya
Mama alienda kule kusalimia kama ilivyo ada ya ujirani mwema.

IMG-20210718-WA0012.jpg
 
Viongozi wapu.uzi kama hawa kina Mwigulu ndiyo wanaopandisha joto la uhitaji wa KATIBA MPYA
 
Wait...WHAT?!!

Kwa hiyo uchumi wa MTANZANIA siyo uchumi wa TANZANIA?! Kwa hiyo tunakaribisha wawekezaji wa kigeni ila watanzania wasioridhishwa na hali ya uchumi wanaambiwa wahamie Burundi? SHERIA ni MSAHAFU au BIBLIA kwamba haziwezi kubadilishwa?! Bunge ndio linatunga KANUNI?

Labda ni mimi wa darasa la saba B sielewi Daktari wa Uchumi anasema nini. Basi sawa.
Ujinga wa viongozi na baadhi ya wananchi ni kufikiri kuwa uchumi hujengwa kwa kodi, na pia uchumi wa nchi ni tofauti na uchumi wa raia.
Kodi haikuzi uchumi kwa ujumla wake bali huhamisha umiliki wa pesa kutoka kwa raia kwenda serikalini katika nchi hiyo hiyo (ni kama kuhamisha pesa yako mfuko mmoja kupeleka mwingine).
Uchumi wa nchi ni jumla ya uchumi wa raia wote pamoja na wa serikali.
Maendeleo ya uchumi hupatikana zaidi kwa kukusanya nje na kuingiza ndani na ndiyo maana wajanja walianzisha utumwa, ukoloni na sasa ukoloni mamboleo.
Ubinafsi na ujinga wa viongozi wengi wa Afrika huwaza kuwaongezea kodi wananchi wao kwa lugha laini za kukuza uchumi (sawa na mzazi mjinga na masikini ambaye huwaza kuwapeleka watoto wake kufanya vibarua badala ya shule).
 
Jeuri ya namna hii huwa wanakuwa nayo Wanasiasa wa Tanzania tu. Sababu wanajua Wananchi wa Tanzania wanaowalipa mishahara na posho. hawana la kuwafanya.

Ni kauli iliyojaa dharau, kebehi, kiburi, ujivuni, ubazazi, ubaradhuli na ulaanatullah. Huyu amejikinai. Hawajali wananchi maskini wa Tanzania. Na watanzania sababu ni wapole sana nadhani hatuna la kufanya.

Tumpongeze anaupiga mwingi sana.

Kama hutaki kulipa nauli piga mbizi
Kama hutaki baki na mavi yako nyumbani
Kama hutaki kulipa basi hamia Burundi
 
Kwani huyu dokta korona ni mrundi kama meko
Sina uhakika ila niliona alivyoapishwa raia wakipande hicho walimpongeza sana na wakasema tumeonyesha mfano wa mshkamano kwa kumpa cheo hicho ndugu yao hatujawa wabaguzi
Siku hio mimi sikulala wala sikula nilitetemeka sana kwa hofu
 
Back
Top Bottom