My Confession: Nilivyohudumia Mimba iliyokuwa na Baba 5 pasipo Kujuana

My Confession: Nilivyohudumia Mimba iliyokuwa na Baba 5 pasipo Kujuana

Kwamba ni siri yaliyomo humu?
Anyways mi nipo kujifurahisha humu sijaja kudanga or anything like that! Awe bwana au babu yako idgaf! popote utakaponikuta usinihesabu kwenye hilo kundi unalowaza!
Punguza kisirani, nitakapokukuta wapi sasa?? 😹😹

Kabla ya kukutoa kwenye hilo kundi kwanza hakikisha lile jambo na babu umelifanikisha.
Umemuahidi ujue..!! 😹😹
 
Kwanini ukubali kupokea matunzo ya mtoto kwa Wanaume watano tofauti

Hata kama tunachepuka, hili halivumiliki
Kwani wewe ulikuwa na malengo nae si umeandika ulikuwa unataka uipige usepe sasa yeye kwa nini akuonee huruma,Tulieni na ndoa zenu jamanii Mwanamke akishajua umemfanya mchepuko nae anakufanya kitega uchumi.
 
Punguza kisirani, nitakapokukuta wapi sasa?? 😹😹

Kabla ya kukutoa kwenye hilo kundi kwanza hakikisha lile jambo na babu umelifanikisha.
Umemuahidi ujue..!! 😹😹
Uweeh nilikuwa namtania babu yangu tunaishiaga hivyohivyo leo kiherehere ndio kimeniisha😂
 
Duhh pole sana aisee
Yaani acha tu sista ingawa ni kitambo ila ilibaki kidogo sana niwe chizi

Niliondoka dar nikaacha ofisi na nilipokaa bila bag mpaka mkoani
Kwa mama mkwe..akasema "baba nisamehe mwanangu ni malaya*
Kumbe yupo dar na jamaa yake aliemtoa bikra

Mtoto alipofariki woote wakaanza mashambulizi kwangu eti nimemloga..
Balaa nikakiwasha nao wakakiwasha..
 
Yaani acha tu sista ingawa ni kitambo ila ilibaki kidogo sana niwe chizi

Niliondoka dar nikaacha ofisi na nilipokaa bila bag mpaka mkoani
Kwa mama mkwe..akasema "baba nisamehe mwanangu ni malaya*
Kumbe yupo dar na jamaa yake aliemtoa bikra

Mtoto alipofariki woote wakaanza mashambulizi kwangu eti nimemloga..
Balaa nikakiwasha nao wakakiwasha..
Pole sana kaka, kuna watu hawana jema ata uwalambe miguu! Dawa ni ku-cut off tu watu kama hao utapona maumivu mbeleleni! Pole sana kwa chamgamoto mkuu!
 
Kwamba ni siri yaliyomo humu?
Anyways mi nipo kujifurahisha humu sijaja kudanga or anything like that! Awe bwana au babu yako idgaf! popote utakaponikuta usinihesabu kwenye hilo kundi unalowaza!
Hem kwanza njoo mjukuu, nipo kwa ajili yako mzee wa pension sitakupa pressure wala...🤣
 
Option ya ku-block no haikuwepo alafu whatsapp ilikuwepo?! Na whatsapp imezinduliwa 2009!! Anyway story yako ni nzuri ila sidhani kama ni ya kweli!!
 
Ngoja nimalizie kisa changu hapa japokuwa kipo on progress

Kuna binti nilikutana naye sehemu, actually nilimchukulia kama heat and run, so kisa kinaanza hivi


Tulifahamiana ndani ya miezi miwili, na ndani ya miezi hiyo miwili nilikutana naye kama mara3 hivi, japo mambo yetu ya ukubwani ilikuwa mara2 na sikuwa na ukaribu kihivyo, kosa langu nilimleta kwangu mara moja akawa amepajua, katika huo mwezi siku moja nililala naye ..tukaja kukutana baada ya week 3 (kutokana na ubusy wa shughuli zangu)

Baada ya week3 ilikuwa siku ya jumapili nipo church akapiga sana simu ili aje kwangu nikawa sipokei maana nikiwa church huwa namute simu ..baada ya ibada nilikuta mised call kama 21 za binti huyo

Ikabidi nimpigie nikamuuliza shida ni ipi..akasema anataka kuja kwangu kuniona...mimi siku hiyo sikuwa na mzuka wa kukutana naye ila kwakuwa aliomba sana kuja kwangu nikasema ok.. aje...

Alivyokuja wala hakusema kama ana ujauzito maana ningeomba tupime (hapo tulikuwa na 3 weeks bila kuonana)

Basi bana ..jumapili hiyo akaja kwangu...tukafanya ya kufanya...asubuhi ya juma3 nikataka kwenda kwenye mishe zangu...akasema ana mimba yangu...yaani mimba kaipata usiku huo (mimi nikamkatalia) nikasema tupime akagoma katakata...kuna jirani ni rafiki yangu nikamshirikisha ..tukamwambie apime tukiwa wote akagoma pamoja na vipimo kuwepo akasema na hatoki ndani maana kashaharibu ujana wake

Basi nikaamua kupoa kwa muda ila nikasema kama umegoma kupima atoke ndani ya nyumba yangu akagoma

Kwa shida saana after 1 week 2 days ndio akakubari kutoka ila akadai ana mimba ila kupima hataki

Nikafanikiwa kumtoa kwa nguvu akatoka...akawa anaendelea kusisitizi ana mimba...baada ya mwezi ndio akasema nimpime akakubari..nikampeleka hotel tukapima .
Mimba ikawa imo...

To me, siamini kama huyo ni mtoto wangu japo alishazaliwa..impact yake simu kama zote za kuomba.matumizi...mara anataka ajengewe nyumba

Scenario ya kujitegesha kwangu na ndani ya saa 4 kutangaza ana mimba yangu imenifanya nisiamini mazingira ya mtoto huyo kupatikana (asije kuwa na kadi tano)

Ndio nipo njiani kufanyq DNA ya siri bila yeye kujua

Nimeleta kisa kwenye uzi huu maana vinafana na chako na bado ni tukio ambalo lipo active..wadau mnaweza nipa maoni

Akina dada wa sawa ni hatariqq anakutegeshea na mazingira ya mimba yanakuwa na uncertainity/utata nyingi/mwingi
DNA za bongo ni lazima uambiwe mtoto ni wako! Labda uende na sampe za wababa wawili mjifanye mnamgombania mtoto ndo atleast unaweza kupata majibu sahihi! Tegemea kuambiwa mtoto ni wako!
 
Pole sana kiongozi Mzee endelea na maisha yako imladi bibi yetu hajui kilichotokea
 
Mnatuchanganya mkuu!🤗

Mbona tunaambiwa mwanamke hapendi na hawezi kuwa na mwanaume asiemuhudumia?
Hela ya mwanamke inaliwa sana na wanaume. Hela yake inaliwa na wanaume wa3 tu
1.Ndugu wa familia(baba au kaka yake)
2. Mchungaji au Sheikh au Mganga
3. Mwaume aliyeteka husia zake

Hapo namba 3 kuna ma2
1. Jamaa asiombwe kabisa hela
2. Aletewe ili apunguze kujitafuta.
Na huyu akishajipata ana muacha huyu kuwa single maza na muda wowote atakuwa anaichapa.

Mkuu, natumaini haupo kwenye namba yoyote hapa.
 
Part two
Nawarudisha nyuma kidogo;

Mahusiano mengi ni win-win condition, kuna nyakati yule binti aliwahi kuniomba vitu viwili, moja aliomba mtaji wa biashara na kingine aliniomba nikipata nafasi sio mbaya nimjengee hata vyumba viwili ili ikitokea lolote basi mtoto apate sehemu ya kulala.

Baada ya tafakari, nikaona badala ya kumpa mtaji wa biashara Wacha nimjengee hiyo nyumba aliyokuwa ameniomba.

Nikanunua kiwanja Kibaha kwa Mathias kutoka kampuni moja iliyokuwa inajihusisha na uuzaji na ununuzi wa Viwanja

Baada ya kukamilisha kununua kile kiwanja, huku wale jamaa wanahangaikia kunitengenezea Hati, nikamwaga tofali then nikaanza kuinua vyumba vitatu.

Nikaanza kujenga taratibu huku nahesabu miezi ya huyo mtoto azaliwe.

Nyumba ilipofika usawa wa Lentor, si ndiyo nikakuta hizi kadi nyingine nne za huyu mtoto.
.….............. ................ .................
Alipotoka mazoezini, nikamweleza ukweli kuwa Mimi na yeye basi, nilikuwa natafuta ushahidi bahati nzuri nimeupata. Nikamwonesha zile Kadi zake nne za wale Wanaume wengine zenye majina ya mtoto wake

Kusema kweli nilijizuia sana kumfanya jambo baya siku Ile, nahisi Mungu alinisaidia vinginevyo huenda kwa Umri huu ningekuwa natumikia adhabu ya kuua.

Kuna mambo kadhaa yakawa yananijia kichwani, moja nitarudishaje gharama zangu

Pili nilipanga niwapoteze Mama na Mtoto wake, Kuna mpango niliporudi nyumbani niliupanga, ila baadaye huruma ilinijia nikamwacha aendelee na mambo yake

Muhimu nimeshajitoa kwenye ule mtego.

Kwa hasira, nilitafuta dalali, nikauza lile gofu pale Kibaha ili kufidia gharama nilizotumia japo kidogo, uzuri wake Hati ilitoka kwa jina langu

Baada ya tukio lile, simu zilipigwa nyingi kuomba tukae tuzungumze ili kumaliza tofauti.

Kwenye biashara hakuna mtu anatamani apoteze wateja, Mimi nilikuwa mteja wake miongoni mwa wateja wake wengine watano(5) tuliokuwa na Kadi zenye majina ya mtoto wake.

Mtu umemkuta na Kadi tano za mtoto, anataka mkae muyajenge, hivi mnajenga kitu gani hapo

To be honest lile jambo lilinigharimu sana, pamoja na usumbufu wa simu zake kupitia namba tofauti tofauti

Wakati ule simu zilikuwa hazina option ya kumfungia mtu asikupate (kama ilivyo sasa) iwapo umechoka usumbufu wake, hivyo nikawa nikikuta namba ngeni inapiga simu, nikawa sipokei hadi inakata.

Baada ya kutafakari kwa kina, nikatafuta Kozi Fulani nje ya Nchi ya miezi 3 nikaenda kupoteza muda kule ili kuondoa usumbufu wake.

Maana niliona ningeendelea kusalia Nchini wakati ule, ningemtumia watu wamwondoe bure yeye na Mwanae, maana uwezo na nafasi ya kufanya vile nilikuwa nao.

Kufika kule nikasajili namba nyingine niliyokuwa naitumia Whatsapp, na Ile aliyokuwa ananipata kawaida ikawa haipatikani.
.......................................

Huu mchezo kwasasa umekuwa mwingi miongoni mwa Wanawake wengi hapa Nchini

Japo nguvu za giza zimekuwa zinatumika sana kufanikisha hili, Mimi sijaandika kuhusu hili ili kufupisha hadithi

Kuna familia zimeingia kwenye migogoro kwasababu ya jambo hili

Kuna Wanaume wamechanganyikiwa na kuvurugwa kisa kikiwa hiki hiki Cha kulea mtoto mwenye Baba wengi

Kuna Wanaume ndoa zimevunjika kwasababu hii pia.

Kuna Wanaume wameacha kutunza familia zao kwa kutekwa na huu upande wa pili

Nimeandika kwa ufupi ili Ujumbe uweze kueleweka.

Nimemaliza ✍️
Mimi pia nimewahi kuwa muhanga wa tukio kama hili ila baba tukiwa wawili
 
Kama hatukuweza kutafuta hela tukiwa kwenye 28 hadi 45 ndiyo tuanze katika umri huu wa 60+

BTW, heri ya Mwaka mpya Mjukuu, naona umenisusa Babu yako
😂😂😂😂 mie nipo sanaa tyuuh. Sijui weyeee huko.
 
Nilijua tyuu huu uzi lazima Masuria yatapararakana
😂😂😂😂😂😂 haiishagi hadi iishe, Lol
 
Hela ya mwanamke inaliwa sana na wanaume. Hela yake inaliwa na wanaume wa3 tu
1.Ndugu wa familia(baba au kaka yake)
2. Mchungaji au Sheikh au Mganga
3. Mwaume aliyeteka husia zake

Hapo namba 3 kuna ma2
1. Jamaa asiombwe kabisa hela
2. Aletewe ili apunguze kujitafuta.
Na huyu akishajipata ana muacha huyu kuwa single maza na muda wowote atakuwa anaichapa.

Mkuu, natumaini haupo kwenye namba yoyote hapa.
Na ili uziteke hisia zake si tunaaminishwa lazima 'umspoil' vya kutosha!

Ama tumepewa gaka silo? 😀
 
Back
Top Bottom