Mzigo wa wazazi kulea mabinti na watoto wa binti zao

 
Wazazi nao wachangamkie tenda. Licha ya kuhakikisha wanawasomesha binti zao, waanzishe utaratibu wa tangu watoto wakiwa wadogo, wa kukubaliana na familia tofauti tofauti zenye watoto wa kiume, kwamba watoto waje kuoana panapo majaaliwa hapo baadae. Wanapokuwa wa umri wa kubalehe, nao wataarifiwe kuwa fulani ndie atakuwa mwenza wa maisha yako na hatimaye waolewe kama ilivyopangwa kama wataridhiana. Inaweza kupunguza mapepe na kurukaruka kwa msichana na mvulana pia.
 
Haha
 



Haiwezekani sababu nature is already ordered [emoji28]
 
Asipo patikana wakuoa itakuaje mkuu ? Au haujui tunapoenda nafasi za mabinti kuolewa zina zid kuwa ndogo.
 
Wazazi ndio wanafanya haya mambo yaendelee. Kila mzazi angeweka ngumu hamna mtoto wa kike angeshika mimba hovyo. Tatizo ni wazazi kuwa maboya. Yaani kweli mzazi na akili yako mtoto wako wa kike anakuja kuzalia nyumbani na wee u akenua meno tuu...eti nalea mjukuu. Pumbaf kabisa. Watu wazima hovyoooo
 
Noma Sana mkuu
 

Kampeni ya Uzazi wa Mpango ina miaka 20 hapa nchini Mkuu.
Labda useme serikali iwekee mkazo.

Pia iongeze Hali ngumu ya Maisha ili kudhibiti kuzaa Sana
 
Yasikukute mkuu.binti yako akizaa hapo nyumbani mpokee tu.ukimfukuza ndio balaa linapoanzia.
 
Bora wee umesema, hakika Una busara.
 
Haya mambo haya! Watoto jitahidini basi, ni ubinafsi Mzazi kukulea kwa miaka zaidi ya 20 na kukulelea mtoto/watoto wako ikiwa uko hai.

Ikitokea muombe mzazi wako akuangalizie mtoto hata kwa two years ukajipange.
Si mpaka awe na hiyo akili...Kuna binti kazaa watoto nane nyumbani..na wote 80% analea Mama ake mzazi.
 
Haya mambo haya! Watoto jitahidini basi, ni ubinafsi Mzazi kukulea kwa miaka zaidi ya 20 na kukulelea mtoto/watoto wako ikiwa uko hai.

Ikitokea muombe mzazi wako akuangalizie mtoto hata kwa two years ukajipange.
Kuna jamaa yangu flani hua namshangaa sana, yani yeye amewapeleka watoto wake kwa baba na mama yake (babu na bibi) eti ndio wanamsaidia kulea.
Basi mimi hua namuuliza kwamba hizo pesa tunazo iba huku kazini anazifanyia nini?? Yaani haoni kama hizo pesa hazimsaidii na watoto wake wanakosa malezi ya baba??
 
Si mpaka awe na hiyo akili...Kuna binti kazaa watoto nane nyumbani..na wote 80% analea Mama ake mzazi.
Kabla sijaoa nilikua singo baba with 5 kids.
Sasa hii kiti ilikua inamtesa sana mama yangu akitaka niwapeleke watoto wangu kwake akawalee na niwe namtumia mahitaji tu.... aiseee nilimkatalia na nikamwambia hawa ni watoto wangu na niwajibu wangu kuwalea mimi mwenyewe.
Basi mama yangu alikua anaumia sana, ila nashkuru Mungu wote walikua vyema na aliekua mdogo wakati huo leo yupo class 7 wakati wakubwa zake wapo chuo huko.
Ila badae nilioa na nikaongeza wengine 3...🙈
 
Jirani, kuna watu hawataki kukaa na watoto wao, nafuu kwao ni watoto kulelewa na watu wengine na wao kutuma pesa tu. Kuna kundi hili la wakwepa majukumu na kundi lile lingine la walioleta watoto duniani wakati hawana uwezo wa kuwalea wala kuwahuduma sababu na wao hawajiwezi kabisa.
 
Aisee
Kuna wakaka wawili ..hao wakizaa na wake zao watoto wanapeleka kwa mama yao..mkubwa ana watoto 7..mdogo watano..na hua wanapelekwa kwa Bibi yao wengine kwa kuachishwa nyonyo..ila Mama yao anawaendekeza vijana wake..Baba yao kaongea na kupandisha mikono juu.
 
Tatizo ni kwamba wanawake hao ndo wanaume wenye hisia nao, ukiwa mstaarabu ni ngumu sana kupata mwanamke sababu watakuambia hawana hisia na wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…