Habari wakuu,
Leo nimeona kituko ambacho sio cha nchi hii, hadi mimi niliyekuwa naangalia nimeona aibu.
How comes mtu unashindwa kuaapa tena kwa Kiswahili, mbaya zaidi mtu kasoma ana Masters ya Science.
Hadi mheshimiwa Rais kasema hio degree yake ichunguzwe, huenda hata hivyo vyeti ni fake.
TAMISEMI angalien mfano wa Mh Rais, mnamuaibisha sana, yale majina hewa ya walimu mliyoyatoa nasema hivi, ipo siku tu mtakula matapishi yenu.
Nina imani kabisa TAMISEMI mkiambiwa mkalete wale watu mlioajiri na vyeti vyao orginal kuanzia secondary mpaka chuo kikuu, hawana wale watu.
Mh Rais pita TAMISEMI, narudia tena pita TAMISEMI kuna wahuni ambao hawajitambui wanaendesha hio taasisi, mpaka Watanzania wanaichukia nchi yao.