Nape: Wafanyabiashara wa fedha za kigeni walioporwa fedha zao wamefutwa machozi

Hii nchi watu hawaelewi tu, hakuna watu hawapendi kulipa Kodi kama matajiri, ukishaona mtu ana bilion kadhaa bank asimilia 90 ya hao watu ni janja janja nyingi tu na kuibia serikali mapato...
Acha wivu Gold hunter utakufa maskini kwa kijiba cha roho. Sentensi yako ya kusema kuwa mtu tajiri amepata kiujanja ujanja ndiyo inawarudisha nyuma watanzania wengi.

Kwa ni ujanja ujanja ni sawa na ujinga? Naamini hakuna mjanja mjinga, ujanja ni akili.
 
Hii biashara kuwa mikononi mwa watu binafsi kunaathiri kwa namna yoyote thamani ya pesa yetu na akiba yetu ya pesa za kigeni?
Juzi jumamosi kuna sehemu niliitwa kuwafanyia Installation ya program fulan na hapo kuna kama kakiwanda tu! Ila nilipongia mule ofisin nikuta kuna Bureau De change, ni wahindi, wanafanya biashara hiyo mule ndani ila hakuna hata bango nje kuonyesha kuwa pale wanabadilisha pesa za kigen! Nafikiri hii ndiyo Tanzania wanayoitaka watanzania ili wakishapiga mrungura wao waende Dubai kushangaa magorofa na ma high way za Dubai.
 
Nani kakwambia VAR ni kuzuia timu kuwa bingwa. Hivi unaufahamu mfumo wa VAR au unajiropokea tu. Mimi ni shabiki wa mpira lia lia old Trafford na kule santiago VAR haina kazi ya kumzuia mtu/timu kuwa bingwa,haiingii uwanjani kusakata soka. Punguza kulamba asali shostie
Gaidi kuwa mbunge ni dalili kuwa tume ni huru? Kwenye soka kuna mfumo wa VAR, huo mfumo ni wa nini iwapo bingwa alikuwa bado anapatikana? Punguza utoto dogo.
 
Mnafiki wewe,mwanaume lazima uwe na msimamo mmoja
Wewe ni mpuuzi basi, kwan io nikiwa na msimamo wa kumpenda mtu kutokana na kazi zake siku akikosea niendelee kushabikia tu

Au kama sipendi utendaji wa mtu siku akifanya vyema nikaze shingo tu kutokubali jema alilofanya

Mimi sio chawa so Niko flexible, ukikosea nasema ukifanya vyema nasema!
 
Mkapa aliacha dola ikiwa chini sana alipoingia JK na upole wake dola ikafika 2400, sasa Mama kaikuta 2300 utashangaa ikafika 5000 kabla hata ya 2025. Na majibu yake yatakuwa haya haya ya kitoto kusema ukraine, covid, maisha yamebadilika etc

Dola sasa hivi ni Sh ngapi? Ni 2300 hiyo hiyo,
Shilingi ya Tanzania imeimarika zaidi dhidi ya fedha nyingine za nchi jirani Tangia Magufuli afariki

Mfano hii ni Shilingi ya Kenya iliyokua sh 22 dhidi ya Tz na sasa ni Sh 17



Halafu Mkapa unamfananisha vipi na Magufuli? Mkapa alifanya privatization na kufungua nchi kwa wawekezaji na uchumi ukakua, Magufuli alikuwa anafanya kinyume, kuua mashirika binafsi na kufukuza wawekezaji
 
Hakuna watu wakwepa Kodi Kama Hawa matajiri, na ndo maana nikaweka 90 percent naamini Kuna waaminifu pia
 
Na ndio nyie mkisikia mtu ni tajiri akili zako zikakutuma huyo ni mwizi..

Jiwe kwa akili yake alijua kila mwenye hela ni mwizi wakati kuna watu wanafanya biashara halali na wanalipa kodi vizuri tuu...

Mentality ya Jiwe kama angekuwa hai tulikuwa tunakwenda shimoni kama nchi.. Mfumo wa kufreez account za watu ungeuwa uchumi kabisa..

Kuna jamaa mmoja amestaafu pilot alikuwa UAE miaka 30 na alikuwa akirudi Tz mara mbili kwa mwaka...
Wamemuwekea hela ya kustaafu kwa dollar... zaidi ya Million 700 ..
Wakaanza sijui kodi zikatwe... Akakubali kama 58 ikaondoka baada ya mwezi hawa hapa sijui una nyumba 4, viwanja 5 hukujumuisha sijui nini wakalamba 75 kwenye account..
Mzee wa watu akashauriwa afungue Equity Bank Kenya ahamishie salio huko bila hivyo angemalizwa..

Na ndio maana mitaji ya watu ilikimbizwa Zambia / UG / Kenya..
Malori mengi ya Tz yalibadili plate no za Zambia/ Rwanda / Kenya kwakuwa hata ukiwaambia jinsi ulivyopata kihalali wao wanakupiga cha juu.
 
Yale maridhiano ya serikali na vyama vya siasa yameendelea kuleta neema kwa watanzania, heko CHADEMA na Samia.
 
Inaonyesha huna uwezo wa kuelewa mambo kwa mantiki, ndio maana unaishia kuongea upuuzi. Lengo la VAR ni kupunguza malalamiko yaliyokuwepo na kuhakikisha ushindi unapatikana kihalali inavyowezekana. Huo mfano nimetoa ili kuendana na hoja yangu ya tume huru ya uchaguzi. Sasa sijui ni utoto gani unaniambia, mara sijui asali na upuuzi kama huo. Subiri watoto wenzio wa VETA mjadili.
 
Nyie mlidanganywa sana na yule jamaa.

Mfano Makusanyo ya TRA kipindi cha Magufuli yalikuwa trilioni 1.2, kipindi cha Samia ni trilioni 2.

Kukusanya kodi huhitaji kufanya uporaji wa kishamba kama ule
We kweli zumbukuku. Sasa kama uliona Magu anadanganya buyu wa sasa unamuaminije wakati huyu anakupa data za jumla jumla.?

Then hayo makusanyo amekusanya kwenye nini wakati saa hizi hata ukienda kariakoo mfanyabiashara anakuambia nakupa risiti ya kusafirishia. Unamuambia nitadakwa anakuambia ah siku sio kama zamani usihofu.

Nakumbuka enzi ya Magu mfanyabiashara anakupa risiti hata kama unaondoka.

Vituo vya mafuta vyenyewe mashine zilishajifia.

Pump ya mafuta bandarini ilishajifia.

Nchi ipo ipo tu.
 
Kenya kuna anguko kubwa sana la kiuchumi ndugu, wanapitia transition period so muache ujinga kulinganisha pesa yetu na nchi maskini mwenzetu


Unaacha kulinganisha pesa yetu na global dominance currency kama dollar, Yuen, euro unaleta comparison na wakenya ambao kwa mwaka tunafanya biashara ambayo haifiki hata bilioni 600 za kitanzania
 
Raia huwa tunashangilia sana lakini madhara yanapotokea nisisi pia tunapiga kelele na kulialia..

"Mmeshiba ~ ndiooo."
"Mnanjaaa ~ ndiooo".

Umasikini wa Watanzania na Tanzania kwa kiasi kikubwa unachangiwa sana na wafanyabiashara wezi wasio waaminifu wanaoshirikiana na wanasiasa walio kwenye mifumo kuifirili nchi.
 
VAR imepunguza nini mbona bado malalamiko yapo. Punguza ujuaji kwenye mambo usiyoyaelewa. Hio tume huru ni ipi hasa,maana ruzuku mlizikataa kisa hamkuukubali ushindi uliotokea wala wabunge walipatikana ila ghafla mmebadili gia na kuichukua kinyemela. Mnachotqkq nyie ni tume itakayowapendelea,katiba itakayowapa madaraka mkononi. Mlamba asali umepanic
 
We zumbukukuku Magufuli nimesema alikuwa anadanganya kwenye nini?
Nime assume ni kweli makusanyo yake yalikuwa trilioni 1.2 kwa mwezi (Japo alipiga marufuku mtu kuhoji takwimu za Serikali) Sasa Samia ni Trilioni 2
Au unataka tuamini ya Magufuli na ya Samia tusiamini?
Wakati jamaa alikuwa muongo hadi ugonjwa na kifo chake nacho akifanyia uongo..!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…