Waziri Nape Nnauye akiwa katika kongamano la miaka 2 ya Rais Samia, amesema Rais amewafuta machozi watu wengi walioonewa na utawala uliopita.
Kama vile wale wafanyabishara wa fedha za kigeni ambao maduka yao yalivamiwa ghafla na wanajeshi wenye mitutu na kuchota fedha zote kisha kufunga maduka hayo.
Rais Samia amewafidia na kuruhusu maduka yao kufunguliwa tena.
View attachment 2558822
===
"Rais Samia Suluhu Hassan katika miaka hii 2 ya uongozi amefanya kazi ya kuwafuta watu machozi na amefanya kazi ya kurudisha furaha na tabasamu kwenye maisha ya watu. "Wale wanasiasa wenzangu waliokimbia nchi machozi yao yamefutwa na na furaha imerudishwa kwao wamerudi nyumbani"
"Wale Wenye mahotel ambao hotel zao zilifungwa kwa sababu ya COVID 19 machozi yao yamefutwa kupitia royal tour. Watalii wamejaa. Wale waliokuwa na magari ya kusafirisha watalii waliokuwa wamepaki Arusha na kwingineko wamefutwa machozi na Rais Samia Suluhu Hassan".
"Wale wafanyabiashara waliokuwa wakiuza fedha za kigeni ambao maduka yao yalifungwa na fedha zao zikachukuliwa machozi yao yamefutwa kwa kurudishiwa fedha zao na kuruhusiwa kufungua maduka tena"
"Kubwa ni kwamba tumefurahishwa na umeendelea kutugusa sana Waziri Nape.
Asante kwa kufika na Tarehe 25 tutakuwa hapa kwenye Kilele cha Malkia wa Nguvu kwa ajili ya kuwapa tuzo akina dada na mama zetu waliosababisha na kufanya vyema katika nyanja mbalimbali".