Pre GE2025 Nchi imerudi mfumo wa Chama kimoja, Magufuli kaacha utamaduni mbaya kwenye siasa, itachukua miaka 20 kumpata kiongozi kama Kikwete

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ebu kuwa na heshima na kinywa chako hii mitandao ya kijamii isikufanye ujitoe ufahamu wako wewe ukiitwa shetani utafurahi?
 
Mbadala wa CCM ndio kama upinzani tulionao sasa hivi shida inaanzia hapa ndio maana wengine wameamua wasiwe wanapiga kura
 
Mbadala wa CCM ndio kama upinzani tulionao sasa hivi shida inaanzia hapa ndio maana wengine wameamua wasiwe wanapiga kura
Unaweza kuwafanya hao hao CCM wakawajibika kwa kuhakikisha wanapatikana viongozi wazuri wenye upeo badala ya kusubiri ''mbadala''. Timiza wajibu wako kwa kudai katiba nzuri na viongozi wa CCM wanapofanya makosa au ufisadi jitokeze kuwakemea na kudai waondolewe. Wewe unadhani ukikaa na kukata tamaa mabadiliko yataletwa na malaika?
 
🚮
Wapinzani kamwe hawataishika dola kwa aina hii ya siasa wanayoifanya. Haitatokea.
🚮 🚮 🚮
Uvccm imesheheni wajinga wengi mno. Endelea kujidanganya
 
Mkwere ndio raisi wa ovyo kuwahi kutokea kwenye hii nchi
Kupata jibu hilo, umefanya very poor analysis kwa kitumia false premises na kupata wrong conclusion.

1.Wakati wake mawaziri ,Msabaha, Katibu Maswi Eliakimu, Lowasa, walianguka Toka madarakani kwa scandal mbalimbali.

JK angekuwa wa hovyo angewalinda, lakini aliridhia kujiuzuru Kwao.

2.Report za CAG kuhusu matumizi na wizi serikalini zilijadiliwa kwa uwazi bungeni,
Magufuli hakutaka,na alimfukuza kazi Prof Assad CAG kwa kuweka wazi madudu ya Serikali.

Leo pia Mama Abdul anaogopa , speaker anaogopa, hawataki report za CAG zisomwe na kujadiliwa kwa uwazi bungeni.

3.Wabunge wa CCM walitenguliwa na Mahakama baada ya wapinzani kukata rufaa Mahakamani, hakuwahi kuingilia uhuru wa Mahakama hata siku moja.

4.Uwanja wa siasa kulikuwa na mazingira rafiki ya kufanya Siasa, alikaa na wapinzani IKULU wakaongea , kwa maslahi ya taifa, wakanywa na na Sharubati. wakacheka, wapeana 5, Waka shake hand na nchi ilikua inapumua.

Sio sasa Mama Abdul na UONGO wa 4 R magumashi zake.hamna kitu.

5.Mtandao wa barabara za Rami kuunganisha mikoa nchi nzima, ni yeye,SGR ,Interchange zilikuwa on paper wakati wake.bMagufuli akaja kujenga.

6.Ajira kila mwaka aliajiri wahitimu wengi wa vyuo vikuu, madaktari ,walimu kwa uchache kuwataja waliajiriwa.
Aliongeza mishahara kila mwaka Leo ni taabu tupu.

7.Vyombo vya habari vilifanya kazi kiasi kikubwa wakiwa huru, likiwemo gazeti la mwanahalisi ambalo lilimwita VASCO DA GAMA kwa ajili ya kusafiri.

Kwangu mimi na kwa wanaoelewa ,Kikwete was the best President ever, and will remain best President of our time.

Alikuwa na weakness ndogondogo za kibinadamu, ambazo Mamako, Babako, watoto wako na mke wako na wewe mwenyewe kama binadamu unazo.

Issue ya kutekwa ulimboka kwangu ni sawa kwa maslahi ya Taifa,mgomo ulikuwa mbaya uliua ndugu zetu hospitalini hasa Muhimbili.

Karibu UORODHESHE MABAYA YA JK angalau manne hivi.

Na kama ni kwa sababu ya chuki utueleze chuki yako inatokana na nini hasa.


🙏🙏
 
Kuleta ufisadi wa kiwango cha juu kwako ni kuleta mwanga? Hakuna Rais anayeweza kuvunja rekodi ya ufisadi wa mkwere
Na hata hiyo demokrasia tunayoisifia ilikuwa ni katika kuwafanya wapinzani wapunguze kumfuatilia ila kwa kweli hakuna kipindi ambacho taifa hili limepotia ufisadi wa kutisha na nchi ilikuwa inanuka madawa ya kulevya kama wakati wa mkwere, kama huna pesa kipindi cha mkwere sijui ni haki gani ungeweza kuipata. Kama huna mtu anayekujua sijui ungepitia wapi kupata nafasi kwenye sekta nyeti kama huna pesa au huna baba au mjomba serikalini.

Yaani wakati wa JK ukiyaona majina ya watu waliokuwa kwenye sekta nyeti ungedhani hii nchi inawatoto wa wakubwa tu ndiyo viongozi. Anagalia BOT na vitengo vingine nyeti kama huna jina sijui ungepitia wapi.

Kwakweli JK utawala wake ulikuwa dhaifu sana na tusiombe akaja kutokea kiongozi wa karba ya mkwere.
 
Naam, ni hoja lyoshiba
 
Na hata hiyo demokrasia tunayoisifia ilikuwa ni katika kuwafanya wapinzani wapunguze kumfuatilia
Hao walioitwa wapinzani enzi za mkwere walikuwa ni mapandikizi yake wenye njaa yao mjini...

Hapakuwa na wapinzani halisi na ndio maana alipikuja JPM aliwafunua utupu hao 'wapinzani' kwa kuwanunua na kuwapa ubunge kwa tiketi ya CCM.

JPM ni rais aliyetuthibitushia kuwa hakuna wapinzani TZ.
 
hakuna haja ya akupiga kura kwa maana chaguzi zimegubikwa na wizi.
na huu ndio msingi wa umaskini wetu mpaka tutakapojitambua.

Na amini kizazi kitakachofata kitasattarabika kama nchi za Marekani na Kenya
 
Miaka 20 karibuni hapa nadhani itachukua nusu karne huko..
 
Nashauri tufute vyama na chaguzi zoooote
Watanzania hatupo tayari na chaguzi.
Viongozi wotee wawe wanateuliwa na chama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…