4 7mbatizaji
JF-Expert Member
- Dec 8, 2019
- 8,406
- 9,619
Comment ziwe fupi fupi tafadharini....
Swali langu la kwanza: Hivi ni kweli Lisu alisema asipotangazwa basi watanzania waingie barabarani? au alisema akishinda na asitanganzwe ndipo ataingiza watu barabarani? hizi kauli mbili tofauti na zina maana mbili tofauti.
Swali langu la pili: Mkurugenzi anapata wapi Confidence ya kumpiga mkwara Mgombea mwenye uelekeo wa kushinda urais ndani ya siku chache zijazo? hii ni kutokana na hali halisi ya mikutano ya wagombea mpaka sasa
Kwa maelezo ya mkurugenzi wa tume ,wajiandae kubatizwa kwelikweli na mgombea wa chadema ,
mwisho tume ijue pia kwenye majukwaa Kuna Mambo mengi ya kisiasa so vipo vitu ambavyo hakuna umuhimu kuviingilia maana Kila chama kina mipango yake ya ushindi na pale mgombea mmoja wa chama flani aonapo moja ya mbinu ya chama kingine ni kumfanyia hujuma lazima atoe mapigo na ni kazi ya chama kilichopewa mapigo kujibu mapigo ,hiyo ndo sayansi ya siasa, Sasa tume ikiingilia ugonvi mwingine ambao wawahusu wagombea na vyama vyao wanakua wanajichanganya bila sababu za msingi.
tuhuma zipo na sio kwamba ukituhumiwa Basi una kosa ,ni kujibu tuhuma na kumtoa mpizani wako kwenye reli