Ni halali Wazanzibari kufanya kazi za Watanganyika?

Huwa nakuheshimu sana mkuu ila kwa hili hapana. Hiyo elimu usiilete maana utaharibu atmosphere kabisa bora tubaki hv hv km hatujui, ukiuchimba muungano na mambo yake unatamani uwe rais wa jamhuri na jambo la kwanza uitishe uchaguzi wa rais wa tanganyika.
 
Ndio wenye amri kwenye jeshi hilo sasa hivi; na huko nyuma viongozi wa CCM toka Tanganyika walisikiliza hao hao wezao wa CCM kutoka Zanzibar wanataka nini kifanyike.
Alikuambia Nani kwamba huko nyuma walikuwa wakiwasikiliza , Sasa mbona waliwafukuza?
 
Alikuambia Nani kwamba huko nyuma walikuwa wakiwasikiliza , Sasa mbona waliwafukuza?
Naona huelewi ninachokiandika.

Hao watu wa CCM wa pande zote mbili walilinda maslahi yao bila kujali wanakotokea.
Hao unaowazungumzia wewe waliofurumshwa ni wale ambao hawakulinda maslahi ya chama.

Kwa hiyo nielewe ninachozungumzia hapa.
Hao viongozi wa CCM toka visiwani walikuwa na madaraka yote bila kuingiliwa na wenzao wa Tanganyika, mradi tu maslahi yanalindwa.
 
Liliongezwa ili kuwadidimiza Wazanzibari. Walijua Wazanzibari wakiendelea kuwa na elimu watakuwa ni tatizo.
Kwamba wasomeshwe bure halafu wadidimizwe?
Mkuu sio Wazanzibari wamesoma Bara. Weka kumbukumbu sawa. Kuhusu HESLB kudhamini Wazanzibari tafadhali toa takwimu. Hata ikitokea hivyo unavyosema, ni wajibu wa HESLB kudhamini Watanzania.
Ni Mzanzibar gani aliyepo madarakani au kazini hakunufaika na elimu ya bara?
Nitajie kiongozi yoyote wa CUF au ACT aliyewahi kulaani elimu ya juu kuwa suala la muungano
Bandari haijawahi kuwa ya muumgano. Bandari ya Bagamoyo inaweza kuwa ni tatizo kwa Zanzibar nayo ilifanywa hivyo ili Zanzibar iwe tegemezi. Mara nyingi ndivyo inavyotakiwa Bara.
?
Tunazungumzia JMT kwa hivyo haijalishi Katiba ya Zanzibar kutambua waziri mkuu. Waziri Mkuu ni wa JMT.
?
Mkuu hivi ndivyo ilivyo hivi sasa kwa 21%. Nayo hakuna siku imetekelezwa kwenye ajira.
?

Nadhani ni wale wa ''... Zanzibar na TV za rangi Afrika '.
Masalamu.
 

Kwa hisani ya Aljazeera

Tazama clip hiyo hapo juu. Dakika ya 2.38 Jusa anasema kama maoni ya katiba hayatazingatia Baraza la Wawakilishi LINAWEZA kupitisha maamuzi ya kuvunja muungano.

Mwenyezi mungu ni mkubwa na mwema sana, sasa hivi wana Baraza la Wawakilishi(BLW), Wana makamu wa Rais kutoka ACT, wana Rais wa Zanzibar na Rais wa JMT ambaye ni Mzanzibar!

Katika neema hii wanaweza kutumia BLW wakavunjilia mbali muungano au Wakamtumia makamo wa Rais wa Zanzibar ACT kushinikiza referendum au kumwambia SSH wakati wetu ni huu tunataka REFERENDUM

Kama kuna mtu anaweza kumtag Jusa na OMO, shime waungwana! neema za Allah zimetremka muda wakulivunja dude ovu muungano ni huu . Silaha zote mnazo!ikiwemo REFERENDUM

Kalamu Allen Kilewella
 
Naona unajichanganya huku umesema waliofukuzwa hawakulinda maslahi ya Chama, halafu unasema Hao walio pande zote Za Muungano walilinda maslahi yao wenyewe
 
Mtetezi wa muungano alikuwa ndugai, kitendo cha kutoka basi hatuna mtetezi mwingine. Ajira in sehemu ndogo sana, anaglia na maeneo mengine
 
...na bado wanapata 4.5% ushuru kila mwaka. Ndiyo sababu rais wa zanzibar kila siku anadai yeye si muumini wa kodi kubwa, hata VAT zanzibar ni 15% anajua pesa itatoka Tanganyika.............gharama ya muungano anayeibeba ni mtanganyika.
 
Mzanzibar gani aliyepo madarakani au kazini hakunufaika na elimu ya bara?
Nitajie kiongozi yoyote wa CUF au ACT aliyewahi kulaani elimu ya juu kuwa suala la muungano
Ukitaka kulijua hili fuatilia maoni ya Wazanzibari baada ya CCM kuirejesha elimu ya juu kwenye muungano baada ya rasimu ya Warioba kuliondoa.
Nadhani ni wale wa ''... Zanzibar na TV za rangi Afrika '.
Masalamu.
Hapa sielewi unachozungumza.
 
...na bado wanapata 4.5% ushuru kila mwaka. Ndiyo sababu rais wa zanzibar kila siku anadai yeye si muumini wa kodi kubwa, hata VAT zanzibar ni 15% anajua pesa itatoka Tanganyika.............gharama ya muungano anayeibeba ni mtanganyika.
Hiyo 4'5% uliitowa wewe ?
Unajua toka 1970s Tanganyika haijalipa kitu? Na imefika matrilioni?
 
Naona unajichanganya huku umesema waliofukuzwa hawakulinda maslahi ya Chama, halafu unasema Hao walio pande zote Za Muungano walilinda maslahi yao wenyewe
Duh,
Mada imekuwa nzito kwako. Pumzika akili itulie kidogo.
 
Duh,
Mada imekuwa nzito kwako. Pumzika akili itulie kidogo.
Wacha kukimbia kiaina , unajichanganya

Mara urukie Samia ,mara waliofukuzwa CCM hawakulinda maslahi ya Chama , hapo hapo unasema Hao walio pande zote Za Muungano walilinda maslahi yao wenyewe, Sasa Kama walilinda maslahi yao wenyewe, hayo maslahi ya Chama waliyalinda wakati gani?
Kweli kijana umechanganyikiwa
 
Sina muda wa kupoteza na kupiga porojo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…