Katika barua yake aliyoiandika mwezi machi mwaka huu kwa wanasheria wenzake wakati akigombea nafasi ya urais. Tundu Lissu alisema kuwa wiki hiyo akiwa Dodoma, watu "kutoka nafasi za juu" walimfuata na kumjulisha kuwa kuna mbinu za kumuuwa. Akasema watu wasipuuzie habari hizo zilizokuwa zikosambaa mitandaoni.
Barua hiyo ilikuwa na heading inayosema "People at top aren't acting and thinking rationally anymore"
One thing for sure, Tundu Lissu siyo mwoga hata kidogo. Mbaya zaidi kwa wadhalimu, Mungu amemwepushia kifo, sasa akirudi ni kama Simba aliyejeruhiwa.
Ni matumaini yangu kuwa hao waliompa hizo taarifa watatoa ushirikiano. Ama pengine waanze kutoa ushirikiano. Sidhani kama Lissu ataacha kuwataja given amekoswakoswa. Kama walishamwambia hao wapangaji mipango, basi amini, Lissu atawataja. Kama hakuambiwa majina, basi sasa ndo wakati muafaka.
Mungu andelee kumpatia nafuu mapema, kwasababu yawezekana kuishi kwake ni mpango wake.
Binafsi nilishangazwa sana ni kivipi Lissu anaendelea kuishi, given kuna watu walio kuwa far less dangerous kwa serikali lakini yakawapata ya kuwapata na wengine wametoweka. Ilipelekea hata wengine kudhani ni mtu wa usalama. Lakini kumbe jamaa alikuwa akiruka viunzi vingi tu na serikali haikumpatia ulinzi.