Risasi ya nini kaka?! Majasusi wanatumia sumu tu, kama ya :-
Kim Jong-un's half-brother Kim Jong-nam killed after being 'sprayed in face with unknown liquid', possibly by pair of female spies Kim Jong-un's half-brother Kim Jong-nam killed after being 'sprayed in face with unknown liquid', possibly by pair of female spies via @telegraphnews
 
Walioivamia Clouds, walioshambulia ofisi za IMMA, waliokuwa wakimfuatilia Lisu hata Lisu akamjulisha IGP na Mkuu wa Usalama, wanaaminikaje?
 
Nje ya mitandao ya kijamii na baadhi ya wasomi, Magufuli anakubalika na wengi nchini, hasa vijijini ambako kura nyingi ndiko zinakotoka. Waathirika wa sera za Magufuli ni elites pekee.

Sent using Jamii Forums mobile app
Utakuwa unaota ndoto za mchana. Anapoacha watu wakifa njaa vijijini, waathirika wanabaki kuwa ni 'elites' unaowasema au.Napembea vijijini, ndugu kila kona kilio ni Magufuli kuleta maisha magumu.
 
Utakuwa unaota ndoto za mchana. Anapoacha watu wakifa njaa vijijini, waathirika wanabaki kuwa ni 'elites' unaowasema au.Napembea vijijini, ndugu kila kona kilio ni Magufuli kuleta maisha magumu.
Hii nchi mkuu iliharibika sana. Mfumo wote ulikuwa umeoza na ingeendelea hivyo kamwe tusingetoka kwenye dimbwi kubwa la umasikini wakati wachache wakiishi katika utaajiri mkubwa sana utokanao na ufisadi, rushwa, na ubafhilifu wa mali za umma.

Serikali hii imeanza kuinyoosha nchi. Matokeo yake ni kuziba vile vyanzo vyote haramu vya mapato. Hela za wizi (TRA, bandari, watumishi hewa, ukwepaji kodi, n.k.) zinakauka. Hela za madawa ya kulevya zimepungua. Matumizi mabaya ya fedha kwa watumishi wa umma yanapungua. Nchi hii ilionekana kuwa na neema hapo nyuma kwa sababu fedha chafu zilizagaa mitaani.

Wanufaika wa hizi fedha chafu walikuwa baadhi ya hawa elites. Hawa ndio wanaoumia sana sasa. Waliokuwa wanategemea mshahara au mazao yao shambani wanasuasua lakini sio kama wale wapiga dili wakuu.

Watanzania wengi vijijini wanalielewa hili. Sasa kama huniamini kutokana na huo utafiti wako wa vijijini basi tusubiri 2020. Watanzania walichoka na mijizi, wanataka haya mabadiliko.

Lakini pengine sijui ninachosema.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu mtoa mada ametoa uwanja watu wajadili, lakini kila baada ya post mbili anarejea kujibu au kuelekeza. Kaa utulie watu wajadili. Rejea post ya 200. Vinginevyo una motive tofauti.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nikiulizwa swali moja kwa moja ni vema kulijibu. Hapa sitoi maelekezo bali nasoma maoni halafu nachangia. Mimi pia sina majibu ya huu unyama uliofanyika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama mlengwa aliisha vifahamisha vyombo vya usalama kuhusu kufuatiliwa na watu wasiojulikana (jina la kikundi cha ugaidi tanzania), na wakapuuza, kwanini tupate shida kujua wahusika?
 
mangekimambi_Part 1. Naomba niwapeni observation zangu binafsi.

1. Tarehe 5 August Jeshi la Polisi Dar ambalo mwenyekiti wake ni Bashite walitangaza kuwa gari zoooote Zitolewe tinted.
.
2. Tarehe 19 August Tundu Lissu alifanya press conference Na kulalamika kuwa anafatiliwa nyuma Na Watu asiowafahamu kwa muda wa wiki tatu...
.
3. Ukirudi nyuma wiki 3 toka August 19 ni kwamba Lissu alianza kuwindwa around tarehe 29 July. Kwa maana hiyo Lissu aliwekewa watu wakumfatilia nyuma siku 5 kabla ya jeshi la polisi kutangaza watu watoe tinted za magari..... It means waliokuwa wanamfatilia walipeleka feedback kuwa wanapata shida kujua yuko na nani ndani ya gari au wanapata shida kujua kuwa anakaaa upande upi, Au wanapata shida kujua kama kweli yupo ndani ya gari kwamba hawaoni vizuri ndani ya gari, na walipopeleka feedback kuwa vision haileweki ndio polisi wa Bashite walipochukua hatua ya kutangaza tinted zoooote zitolewe....
.
.
Bashite alitengua uamuzi ule sababu ya malalamiko ya Watu na malalamiko hayo yalilenga moja moja Watu kupigwa risasi na majambazi , mnakumbuka lalamiko kubwaaaa Kati ya yooote ilikuwa ni usalama wa Watu na majambazi kujua watu walioko ndani ya gari??? Pale Bashite akaona picha limeungua kabla picha halijachezwa. Can you imagine jinsi wananchi walivyolalamika juu ya tinted kutolewa sababu ya usalama alafu leo Lissu angeuwawa sababu gari Yake haiikuwa na tinted?? Si ingeonekana moja kwa moja ni wao? Ndo maana ikabidi Bashite fastaaaa atengue sababu alishaona picha limeungua na wananchi wameshasema mapemaaaa kuwa kutoa tinted ni kuhatarisha maisha ya wananchi .
.
.
4. Bashite jana kwa Mara ya kwanza kabisaaaaaa hakuwepo Ikulu kwenye hafla kubwa ya kuuza sura kama ile..Je alikuwa wapi kama hakuwa anasimamia zoezi zima la mauwaji ya Lissu....
.
.
.
.
ni jambo la ajabu kabisa..... Sina PhD na nimeweza ku-connect dots zote hizo ila utakuta jitu lina PhD na linakwambia tusubiri uchunguzi. Uchunguzi? Hakuna uchunguzi utakaofanyika na hakuna mtu atakaeshikwa. Issue ndio imeishia hapa......
 
Hawatataka hizi scenarios, wao ni JPM na Bashite tu!
Lissu ana maadui ndani ya CHADEMA kuliko nje au kwingine, tulishasema Lissu anakuja kwa kasi ya ajabu kuliko Mwkt wa Kudumu, Lisu ana genge lake na Mwkt pia, its a power struggle, JPM na dola yake hawana shida na Tundu, hes just a talk! Dola ina mizizi na connections kwenye sekta zote, hawahitaji kumuua Lissu kushinda kesi za madini, hawahitaji kumuua yoyote yule anayepingana dola! Pia kuna swala la ACACIA na Barrick, yote haya yawezekana ni issue nzima ya huu unyama aliofanyiwa Lissu..
Ila kila ukiwaeleza hawataki, lakini kwanini washangaa, ni tabia zetu kuamini wachawi, ukiwa na imani hizo basi kila mtu adui, huku wasahau "Zimwi likujualo halikuli likakwisha!
 

Mkuu kwa kuongezea kwenye uchambuzi wako ningependa kukumbusha ya yule daktari aliyetolewa kucha. Watesi wake waliokuwa pia wamepanga kumwua mara kadhaa walikuwa wakimwuliza kwa nini unaisumbua serikali, kwa nini unaisumbua serikali ..... kwa nini unaisumbua serikali? Watu hawa walikuwa na resource nyingi tu hadi maeneo ya kutesea. Ni wazi kuwa hawa si #1 wala #2.

Yawezekana huyu mbunge amekuwa akileta Fyoko fyoko. Yawezekana alilopewa lilikuwa funzo. Yawezekana lengo halikuwa kumwua bali kumtia adabu.

Yu wapi yule daktari? Ni wazi kuwa watesi wake walijua walichokitaka na wako na njia nyingi za kuwanyamazisha wanaoonekana kuisumbua wanayoiita ni serikali.

Panga pangua kama ilivyokuwa kwa watesi wa daktari yule bila shaka hata wa mbunge huyu hawatakaa wafahamike wazi wazi kwa common man.
 
God help you my friend,lets sing the same song please.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu kifo kimeumbwa na kizuri hakidumu we all know it.... so acha uoga... Ajisifiaye akishindwa utamuweka upande upi wako? Me Nilishangaa that day alipokoswa koswa and then akamwaga ugali hadharani its mean ameingia vita na hao watu... ukiuliza polisi utaambiwa ni watu wasiojulikana means hao ni zaidi yao... Kushindana na watu wasijulikana its only in Tanzania hao watu wapo... Hao Watu hawana Mungu elewa... Ial one Day watu watachoka so lets enjoy this Game... Ngangari na Ngunguri... kama Unamuonea Huruma Lissu Mwambieni atulie Maisha aliyofikia yanamtosheleza aache wengine wachukue Nafasi... Sababu anajua kila kitu na Kazi za Kuumbua zinawenyewe asiingilie Majukumu ya Government kila jambo lina wakati wake limepangwa na serikali kutamkwa sasa yeye ndio anajiona mwenye kazi hiyo... ajue anavuruga mipango Mingi nadhani Washamchoka... Ajiombee Mwenyewe Mkuu Matendo yake ndio Yatamfikisha Kwa Mungu au Shetani
 
Kunyoosha nchi ni sawa, nijuavyo mimi ni kutumia sera na ilani uliyoinadi ili kweka mambo sawa huku pia ukihakikisha unatimiza wajibu wa msingi wa kulinda uhai wa kila raia wa nchi; unayempenda na usiyempenda. Inapotokea unanyoosha nchi kwa watu wengine kupotea, kutekwa, kukutwa kwenye viroba wakielea mitoni na baharini, kulipuliwa ofisi zao na kupigwa risasi hadharani, basi hata hao mnaoamini ni wajinga wa vijijini, Mwenyezi Mungu ni mwema, very soon hata maiti zitazungumza!!!
 
Hata makonda mlimshambulia hivi hivi kwa shutuma za kubuni,,, hatimae kashinda vita na anaendelea kuchapa kazi,,, nashauri tusihukumu wala kutoa majibu kwa jambo lililo gizani,,, tuache mamlaka husika zifanye kazi ili badae tuwe na la kusema kwa sana au tuje kufumbwa midomo kabisa kwa majibu kuwa tofauti na tulivodhani

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kagoshima,
Kuna siku mwana JF mmoja hapa alianzisha uzi kuhusu Ikulu kulindwa na Walinzi toka nchi jirani hususan Rwanda! Ajabu ni kwamba uzi ule haukudumu uliifumuliwa haraka sana! Yawezekana kabsa tumeshaiingiliiwaa maanaa kiliichomtokea TL si kawaida.....!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…