SAIVI KILA MTANZANIA MCHAMBUZI WA HABARI ZA LISSU
 
Safi sana mkuu umeongea bila kuwa upande wowote, katika hili lolote laeza kua kweli, ivi inaezekana kweli upande ule wakataka ishu ya kukabidhiwa ripoti ifunikwe na ishu ya TAL kweli? Ndo hapo unapopata ukakasi wa Ku guess who, tatzo wanaofuatilia kusaka nani mhusika nao kama kuna hesitate laiti wangekua kamili wangemsaidia pia mkulu
 
Mkuu kuna waliotekwa wakawa tortured. Kuna waliotolewa bastola hadharani. Kuna waliovamia studios na silaha kali. Hata Lissu alishasema hadharani alipofuatiliwa akiwa Dar.

Yote unayosema ni a long shot. Haya mengine yangekuwa yameshghulikiwa i.e. Kwa Lissu kupewa ulinzi nk. Maybe ningekubaliana na hoja yako.
 
Sawa, atang'olewa ifikapo 2020. Upinzani usiwe na hofu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwezi kumzuia binadamu kuhisi jambo, na kila binadamu huwa na hisia. Hisia huletwa na ishara au dalili. Na hisia za kweli huzaa ukweli.

Mleta mada wewe una hisi nani anahusika?
Unadhani kwa nini watu wengi wanahisi mhusika ni yuleee?
Ukiniuliza hisia zangu basi ni dhana ya 4.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu mbona kama upande wa sehemu fulani umepuuzia na kuegemea upande mwingine!?? Upo upande gani kati ya hapo!?

Pilato 007
 

Hesitation hii inatokana na precedent ya "unsolved" cases za matukio ya hivi karibuni kama Ben Saanane, Roma, Nape na bastola, n.k.

Tukirudi kwenye hili tukio.

Katika uchunguzi wowote wa mauaji swali la kwanza ni "Huyu Bwana alikuwa na ugomvi na mtu yoyote?".

Hiyo ni kujua motive ya muuaji. Sasa huyu Lisu ni mwanasiasa. Ameshalala ndani na kukwaruzana na Magufuli mara kibao.

Imetokea amepigwa risasi mara moja watu wanamhisi mgomvi wake. It's only natural. Hivyo Magu hawezi kukwepa kuhisiwa.

Ndiyo maana nasema Serikali ilipaswa imlinde Lisu ili ikitokea mtu anataka kuichonganisha Serikali na watu wake asipate nafasi.

Sasa kosa kubwa kama hili utashangaa hakuna kiongozi mkubwa anawajibishwa. Hili ni kosa kubwa sana kama Serikali haina mkono kwenye hili.

Pia kwa sababu tayari Serikali ni mshukiwa wa kwanza basi adui wa hii Serikali anakuwa mshukiwa wa pili. Adui wa pili ni either hao "wazungu" au watu wa serikali zilizopita wanaochafuliwa na kukwaruzana na Magufuli au nchi zisizopenda amani yetu.

Ipi ni rahisi kati ya "mzungu", ex-Government official au "enemy state" kufanya hili tukio leo katika usomaji wa hii ripoti ambayo ni headline.

Ni wazi ex-Government officials kwa sababu (i) sababu wanayo (kuchonganisha Serikali na kuzima hii ripoti) na (ii) wana access na watu wakufanya hii kazi.

Hii ya kusema ni vibaka (hawajaiba kitu) au ni Chadema wenyewe ni far-fetched assumptions tu.

Kwa hali ilivyo sasa upinzani kufanya hivyo ni kujimaliza kisiasa. For one Lisu is their mouth-piece and secondly, Serikali haipendi upinzani na inatafuta sababu yoyote kuwamaliza.

Pia kusema kwa sababu leo ripoti imesomwa basi hili jambo haliwezi kutendwa na Serikali si sawa kwa sababu hili tukio la kusoma ripoti laweza kuwa the perfect alibi for a crime.

Hizi zote ni speculation lakini ni wazi Serikali ina lawama kubwa ya kubeba kwenye hili tukio na matukio ya nyuma. Hapa natofautiana na wale wanaojaribu kukwepesha hii lawama.
 
lissu alifatiliwa kwa wiki tatu na usalama nae akatoa maelezo but serikali ikakaa kimya Leo target imetimia how come unatuambia serikali haihusiki!??ni watu wenye chuki na lissu yes ila ndio hao waliopo ndani ya serikali..!!
 
waachie kazi hii polisi

*Akifa shekhe kazi ya Mungu*
*Akifa mlevi sababu ya Pombe*
 
I never thought of that. Unaweza kuwa sahihi kabisa mkuu. Thanks.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…