Ni nani wa kujibu hoja za Tundu Lissu?

Ametoa HOJA kuwa bandari zetu zote za bara wamepewa waarabu,

Lakini Bandari za Zanzibar hazijaguswa,

HOJA kama hiyo Badala ya kulijibu unaamua kuipuuza kweli?

Halafu akasema kesho Mei Mosi watu wataenda kulia na kumbembeleza Samia awahurumie adha za kikokotoo na mishahara. Kwa sababu mwaka wa 1964 Rais Nyerere alifuta Tanganyika Federation of Labor akaunda NUTA, ndo hii TUCTA , halafu Nyerere akasema kuanzia leo Rais wa NUTA atateuliwa na Rais wa Tanganyika. Ukawa mwisho wa maandamano, mwisho wa haki ya mfanyakazi.

Katiba mpya ikilinda uhuru wa vyama vya wafanyakazi madhila ya kikokotoo na kubembeleza mishahara yatakwisha.

Sasa nani serikalini humu unadhani anaweza kujibu hoja zinazo elucidate the weakening evolution of labor movement across the history of Tanganyika ?

Zahara Yunus ? Gerson Msigwa ? Mwenezi Nchimbi wa CCM masikini ya Mungu. They are in over their heads! It is very unfair and very inconsiderate kuwatupia hawa rookies zigo la kuwajibu wapinzani.
 
Sasa unatushauri Vipi Sukuma Gang..
Maana Bado tuna Machungu Na Rais wetu hatukumfaidi kabisa akafariki
 
Ahsante ndugu Kalamu , Mimi nimeelewa,

Japo ndani ya CCM wapo watu aina ya Judge Warioba wanaopenda kusema Kweli na kujibu HOJA.
 
Lissu mtu ambae anaweza kufanya nae mdahalo ni mzee Warioba tu ila wengine siwaoni
 
HAKUNA MTU WA KUJIBU, maana wakijibu Lissu atawamiminia lisasi 32 zaidi hoja nzito nzito.
 
Lissu mtu ambae anaweza kufanya nae mdahalo ni mzee Warioba tu ila wengine siwaoni
Na mbaya zaidi Judge Warioba Yu pamoja na Lissu katika mstari wa Kweli na HAKI, haezi mjibu Kwa maana ya kumzima Kwa HOJA.
 
it is very simple, observe some technical 48laws of power...

you can't fight them join them and ofoz you will be safe 🐒
Ni Ngumu maana Tunataka Tume Huru ya Uchunguzi wa Kifo cha Kiongozi wetu..
Tumeanza kumtuna Luhaga Mpina ila wengine watakuja Pia
 
Mbona alipokuwa bungeni mlijaribu kumjibu Kwa HOJA?
Akirudi Bungeni atalazimishwa kuongea pointi na atajibiwa kwa pointi na sio kuropoka anakofanya Sasa hivi. Kumbuka ni watu wasio na uelewa tu na "issues" ndio wanamuelewa.
 
Lissu aana tatizo la kisaikolojia baada ya ile ajali yake ya kupigwa risasi na majambazi kwahiyo asichukuliwe siriazi tafadhali.
 
Kumpuuza inatokana na kukosa hoja zenye mashiko za kumjibu
inaweza kua katika mbinu na hisabati ya siasa,

kwani mbaya iko upande gani hoja yako ikipuuzwa na ukuanza kubabaika na kuhangaika mwenywe physically and mentally, that is science in politics 🐒
 
Kwani Ubongo unakaa miguuni alikopatia Ajali?
Ripoti za madaktari zinaonesha Lissu hawezi kuwa sawa tangu alipopata ile ajali kutokana na kumuharibu sana kisaikolojia kwahiyo inashauriwa asichukuliwe seriously kwa mambo anayoongea.
 
Ripoti za madaktari zinaonesha Lissu hawezi kuwa sawa tangu alipopata ile ajali kutokana na kumuharibu sana kisaikolojia kwahiyo inashauriwa asichukuliwe seriously kwa mambo anayoongea.
Kwahiyo wamasai hawakufukuzwa ngorongoro na mbuga kupewa waarabu?

Kwamba bandari zetu ni issue ya Muungano, iweje bandari za bara wapewe wageni, za Zanzibar zisiguswe?

Matokeo ya Urais 2020 kituo Kwa kituo, hayapo kwenye website ya Tume ya Uchaguzi, ni Kweli au Si Kweli?

Kati Yako na Lissu na wewe, nani yafaa apuuzwe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…